Kuishi Kifukara, Kuzikwa Kiheshima

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Salaam Wakuu,
Siku kadhaa zilizopita tulishuhudia mtu anayesemekana kuchora nembo ya taifa ya Bibi na Bwana yenye caption ya Uhuru na Umoja ,mzee Francis Kanyasu Ngosha, akiishi maisha duni na dhalili huku akiugua. Picha zilioneshwa na kituo cha televisheni cha ITV. Aidha Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Malapa, Buguruni, alijitolea kumpeleka hospitali. Baada ya muda kidogo Serikali ilichukua jukumu la kusimamia matibabu yake Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mzee Kanyasu hakudumu nasi, alifariki na amezikwa leo kijijini kwake Wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza.
Kinachofikirisha ni aina ya maisha ya kifukara aliyoishi kwa muda mrefu bila kutambuliwa na kuenziwa kwa mchango wake kwa taifa la Tanzania. Ameibuliwa muda mfupi kabla ya kufikia mwisho wa maisha yake. Pamoja na kuishi kifukara ameweza kushi zaidi ya miaka 80.Nina hakika angetunzwa angeweza kuishi zaidi ya hapo. Hivi kuna wangapi wamesahauliwa kama mzee huyo?
Serikali ina wajibu wa kutunza watu walioliletea taifa heshma hususan wazee. Jeneza zuri na mazishi ya heshma yaliyohudhuriwa na viongozi wa Serikali waliotoa matamko haviwezi kumpa heshma aliyostahili kwa kuwa hayupo kuipokea. Haimsaidii zaidi ya kuliwaza ndugu.
Kama ana watoto watafutwe ili wapate na kupokea heshima ya baba yao. Kuishi kifukara na kuzikwa kiheshima hakusaidii. Tujadili.
 
Hiyo ndio CCM hata Mzee Timothy Apiyo Na Mzee Davd Wakati amekufa huku anadai Kiinua mgongo chake
 
Serikali hupendelea watu wenye tabia ya kujipeleka peleka, kujionyesha, kuuza sura na kijipendekeza kwa wenye madaraka. kama wewe ni mtu wa kuuchuna hakuna wa kukujali mpaka mauti yakufike
 
Aisee CCM ni janga la kitaifa lakini vijana wao kama kina Polepole, Magoiga, Zimmema wanafiki kupita kiwango cha lami CCM haijawahi kumuacha mtanzania salama kabisa
 
Aisee CCM ni janga la kitaifa lakini vijana wao kama kina Polepole, Magoiga, Zimmema wanafiki kupita kiwango cha lami CCM haijawahi kumuacha mtanzania salama kabisa
Ni kama mfano wa shetani, atajifanya kukuinua ila anguko lako ni kuu na anakuwa kesha kuacha
 
Kuna haja ya kuweka wazi jinsi kuwahudumia hawa mashujaa wetu ila hapo kati serikali ilipoteza kabisa uzalendo kwa mashujaa wetu!! Anzia waliopigana vita Kagera wengine waliishia kuomba na kufa kwa magonjwa na njaa....wako wengi sana ni wahanga wa hilo!!
 
Jukumu la kutunza wazee linaanza na familia kwanza, siku hizi Vifo vya wazee vingi ni sabb ya "elderly neglect" na tatizo hili linazidi kuwa kubwa ktk familia nyingi, serikali inabebeshwa mzigo usio wake, tuwatunze wazee wetu majumbani mwetu tuache kujifanya hatuna muda.
 
Back
Top Bottom