Kuingia kwa dawa bandia za kurefusha maisha (ARVs) serikali inapaswa kuwajibika kwa vitendo...

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,209
42,070
Ikumbukwe kwamba Maelfu ya watu wana tumia dawa za kurefusha maisha,lakini cha kushangaza imebainika kuingizwa dawa bandia za kuferusha maisha. Hivyo mamlaka ya dawa imeagiza ziondolewe mahospitalini, zimebainika zina jenga usugu kwa virusi vya UKIMWI.

Maelfu ya watu walioathirika kwa ugonjwa wa ukimwi ambao kwa sasa wanatumia Dawa za kurefusha maisha (ARVs) nchini wapo hatarini kufupisha maisha yao baada ya kubainika kuwa toleo mojawapo la dawa hizo la machi 2011 ni bandia.


Uchunguzi unaonesha kuwa dawa hizo zilizosambaa katika mikoa ya Dares-salaam, Tanga na Mara zilianza kusambazwa tangu Mei mwaka huu na hadi sasa bado zipo sokoni,jambo lilio ilazimu Mamlaka ya Chakula na dawa Tanzania (TFDA) Kuagiza zirudishwe Bohari kuu ya Dawa (MSD).

MSD wame ahidi kutoa taarifa leo kuhusu kiasi cha dawa bandia zilizo sambazwa kwa wananchi wakati huohuo ni zaidi ya watu zaidi 400,000 wameshatumia hizi dawa.

Ni wakati umefika kwa serikali kuonesha uwajibikaji wa wazi katika mambo ya msingi na kuondokana na tabia ya kulindana huku wananchi wakizidi kuteketezwa kwa uzembe wa watu wachache.

Tunaweza kujiuliza nini kazi ya TFDA kama dawa feki zinapita kirahisi namna hii?

TFDA wamefanya uzembe wa kuruhusu dawa feki na kujidai kushituka wakati dawa zimesha samba nchini, je walikuwa wapi sikuzote na kwa nini hawakufanyia uchunguzi wa kina dawa hizi kabla ya kuruhusu kusambazwa?

Tujiulize ni nani na ni kiwanda gani kimetengeneza dawa hizi?

Ni nani aliye ruhusu dawa hizi kuwa zina faa kutumika kama siyo hawa hawa TFDA?

Ni vyema katika swala hili siasa ikawekwa pembeni na serkali kuwawa jibisha yeyote aliye husika katka uingizwaji wa dawa hizi bandia, na serikali inatakiwa ijue imeanza kuonesha kwa vitendo inavyo leta michezo ya kubahatisha kwenye maisha ya watu.

Source: Mwanachi
 
Ndio hapo mwenye macho anaweza kuona tuna serikali ya namna gani!
Serikali inayo hamua kuteketeza wananchi wake kwa uzembe tuuu!
nashindwa hata la kusema.....serikali hii ni janga
 
Wanachotaka ni kutuua au kutudumaza akili walileta dawa feki za kifua kikuu,dawa feki za malaria,dawa feki za kupimia virusi vya ukimwi sasa dawa feki za kurefusha maisha hawana nia njema serikali ya majini,majambazi,mabazazi,hata sielewi kwa nini hawapishi unaambiwa hata vifaa vya maabara kupima magonjwa kama typhoid,kifua kikuu,minyoo,njia za uzazi ya mwanamke na prostate kwa wanaume zote feki
yaani ni mtaji wa mganga mkuu pale wizarani,ofisi ya waziri mkuu na MSD na kula na kutumia pesa ya umma kwa manufaa yao na watoto wao huku wakiangamiza robotatu ya watanzania ambao hawana uwezo wa kuenda india
 
Uchuuzi kila mahali hapa bongo hadi kwenye afya za watu wanafanya uchuuzi tena bila hata woga kweli tuna safari ndefu sana ya kufikia huko tunakotaka kwenda kwa mtindo huu na hapo ni hizo ARVs tu je madawa mengine kama ya malaria,typhoid,homa et al si kitu cha kushangaza viongozi wetu karibu wote walikimbilia Samunge kupata kikombe cha babu kutokana na mambo kama haya magumashi kila sehemu.
 
Kesi kama izi ndo huwa zanifanya China niwakumbuke na kale kasheria kao kwa Kunyonga
 
Kwa kweli kwa watu ambao hawana huruma kwa wenzao wana stahili adhabu hii!
Kesi kama izi ndo huwa zanifanya China niwakumbuke na kale kasheria kao kwa Kunyonga
 
Hii ni ishara tosha kuwa tumekuwa tukitumia dawa bandia kila kukicha alaf TDA wana kula mishahara ya bure.

Na usishangae wakaunda tume kuchunguza badala ya wahusika kujiuzulu.

Uchuuzi kila mahali hapa bongo hadi kwenye afya za watu wanafanya uchuuzi tena bila hata woga kweli tuna safari ndefu sana ya kufikia huko tunakotaka kwenda kwa mtindo huu na hapo ni hizo ARVs tu je madawa mengine kama ya malaria,typhoid,homa et al si kitu cha kushangaza viongozi wetu karibu wote walikimbilia Samunge kupata kikombe cha babu kutokana na mambo kama haya magumashi kila sehemu.
 
Du kutoka March mwaka jana ndio wamekuja kustukia jana?? Kweli TBS,TFDA na Wizara ya Afya wamelala usingizi wa pono.
 
nashindwa hata la kusema.....serikali hii ni janga

BADILI TABIA, changamoto za serikali sasa ni kubwa kuliko hasa kutoka nchi za nje. Tunahitaji umakini wa hali ya juu sana, hawa jamaa tunaowaita wanatusaidia ndio mimi naamini ndio wanotuuwa kabisa. Hawana huruma na binadamu zaidi ya rasimali za nchi. Hizi dawa zilitakiwa ziwe zinatengezewa nchini. Lakini ndiyo hivyo tena. Utasikia Condoms fake, panadol fake, nini maana yake. Taifa linalotegemea misaada huhatarisha uhuru na usalama wa wananchi wake.
 
Kuna idara za serikali wamelala usingizi wa pono! Yaani dawa fake zimeingia MSD March, 2012 wanakuja kuzuia matumizi September! Ni wangapi wamekwisha dhurika kwa hizo dawa? Kisha watu wakilalamika atatokea mfalme mmoja na kusema kuna watu wana viwanda vya kusema uongo! Tanzania kuna mambo yanatia hasira sana!
 
Serikali dhaifu baada ya kushindwa kuwaletea maisha bora watanzania imeamua kuwapunguza kimtindo.
 
Nilipoanza kusoma kichwa cha mada nikadhani labda kinachozungumziwa ni zile dawa za kurefusha uume.
 
Kuna idara za serikali wamelala usingizi wa pono! Yaani dawa fake zimeingia MSD March, 2012 wanakuja kuzuia matumizi September! Ni wangapi wamekwisha dhurika kwa hizo dawa? Kisha watu wakilalamika atatokea mfalme mmoja na kusema kuna watu wana viwanda vya kusema uongo! Tanzania kuna mambo yanatia hasira sana!

yan haya mambo yanasikitisha sana TFDA kwa nini walii idhinisha matumizi ya dawa feki hapo ndipo tujiulize! Kuna mchezo gani hapa na mmaisha ya watu?

Na inaonesha TFDA waliwaandikia MSD toka mwezi wa nane kuhusu hizi dawa!
 
Yaani mpaka Serikali dhaifu hii ije kung'oka madarakani, tutakuwa tumepigwa majanga ya kufa mtu. Cha kushangaza utakuja kukuta kuingizwa huku dawa feki ni dili la wafanyabiashara wasio waaminifu wakishirikiana na watumishi hao hao wa serikali hii dhaifu. Kila kitu ni dili tu.
 
Back
Top Bottom