permanides
JF-Expert Member
- May 18, 2013
- 10,069
- 11,268
Simba kwa ujinga ni pipa na mfuniko. Hivi unaikumuisha vipi timu ya nchi nyingine kwenye ligi yako?Tumesikia mipango ipo mbioni kuijumuisha timu ya Al Hilal ya Sudan katika ratiba ya NBC kuanzia msimu ujao. Kuna wakati niliwahi kuwaza hili jambo nilipoona wakati ule wanatanga tanga, nikataka kushauri hili kufanyika na nimefurahi kujua kumbe pale TFF kuna watu wana uwezo wa kufikiria mambo yenye tija kwa ligi yetu.
Nakumbuka mwezi January nilishangaa kwa nini hawakujumuishwa katika mashindano yaliyopita ya Kombe la Mapinduzi wakati walikuwepo hapa hapa.
Pamoja na kwamba maelezo ya kina hayajatangazwa isipokuwa tumeambiwa matokeo ya mechi zao hayatajumuishwa katika msimamo wa ligi, ningeshauri pia ikiwezekana katika makubaliano yatakayofikiwa na Al Hilal, wachaguliwe vijana kadhaa, hata kama ni 3 walio katika vikosi vya taifa vya U-17 au U-20 na wawe tayari kuwaingiza katika kikosi chao kama sehemu ya vijana hao kupata mafunzo na uzoefu.
Big up sana kwa TFF kwa hili jambo. Kwenye hili mmeupiga mwingi.
Cha nyongeza, hivi hiyo vita ya Sudan mbona kama ipo kimya kimya sana maana sisikii kabisa kashkash zake?
Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app