Kuhusu Wizi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha

The Next MP

Member
Nov 15, 2023
37
43
Miezi miwili iliyopita niliandika kuhusu Wizi unaofanywa na Halmashauri ya Manispaa ya Mji wa Kibaha.

Nikabainisha kwamba wizi huo wa urasimishwaji wa makazi Katika kata ya Pangani mitaa ya LUMUMBA, KIDIMU NA MKOMBOZI unafanywa kwa kuwatishia wananchi kwamba wasipolipia kiasi Cha 1.6million kwa eneo lenye ukubwa wa 20x20 watabomolewa makazi yao na eneo atauziwa mtu mwingine. Kwahiyo kiwango hicho Cha malipo kinapanda kulingana na eneo alilonalo mwananchi.

Kibaya zaidi ni kwamba malipo hayo yanawekwa kwenye account maalum ambayo Kila mkazi wa maeneo tajwa hupatiwa. Anapewa kiasi kikubwa Cha kuwekwa kwenye account halafu kidogo ataweka kwenye Control number ambayo atapewa baada ya kukamilisha malipo makubwa.

Account namba nimeambatanisha (attachment) Watu wa Sheria tupeni ufafanuzi kuhusu utaratibu wa malipo serikalini.

Hivi ninapoweka huu Uzi KUNA nyumba kadhaa zimebomolewa kwa wale waliokaidi kulipa. Na tayari kwa tetesi ni kwamba Kuna zaidi bilioni moja imewekwa kwenye hiyo account. AaTAKUKURU msiseme hatujawaambia.
Screenshot_20240110-222130.jpg
Screenshot_20240110-223011.jpg
 
Back
Top Bottom