Kuhusu utaratibu: Chadema yatangaza kufanya mikutano nchi nzima wataanzia vijijini, je mikutano ya kisiasa imeruhusiwa?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,034
Kumbukumbu zangu zinanijulisha kuna katazo la kufanyika kwa mikutano holela ya kisiasa isipokuwa ile tu inayohusisha wabunge katika majimbo yao ya uchaguzi.

Sasa Chadema ambayo haina wabunge nchi nzima imetangaza kufanya mikutano nchini kote, wadau hii imekaaje?

Maendeleo hayana vyama!
 
Tukuulize wewe Johnthebaptist kuwa akina Dr Bashiru na Polepole wanaofanya mikutano nchi nzima, je wao wameruhusiwa??

Je wao ni wabunge wa Chama gani??

Kama wao wameruhusiwa, ni kwanini wazuiwe kufanya mikutano hiyo viongozi wa Chadema pekee??

Kama mbwali na iwe mbwali!
 
Wale nilisikia wanafanya mikutano ya ndani!
 
mikutano haijawahi kukatazwa mkuu... katazo lolote linatolewa kwa mujibu wa sheria huyo kichaa alitamka kwa kuwa hakuwa amemeza zile dawa mbona polepole na yule bashiru hujawahi uliza utaratibu
 
mikutano haijawahi kukatazwa mkuu... katazo lolote linatolewa kwa mujibu wa sheria huyo kichaa alitamka kwa kuwa hakuwa amemeza zile dawa mbona polepole na yule bashiru hujawahi uliza utaratibu
Polepole na Bashiru walitangaza lini?
 
CDM ni wakuonewa huruma. Tamko la Zanzibar limefikia wapi? Huyu kaimu mwenyekiti akiongea wala hamna chembe ya karisma. Naye kaishia kupotosha eti CAG kuitwa bungeni ni sakata la upotevu wa 2.4 Trillioni kasahau ustadhi prof mwenzake alichoongea redio UNO na kumsababishia usumbufu usio kuwa wa lazima/epukika.

Wako viongozi vijana vipaji vyao vinapotelea CDM. Mnyika na Silinde chukueni hatua haraka Taifa hili linawahitaji huko mliko mnapoteza muda wenu bure.

Enzi zile za CDM DR Slaa na sisi wengine thubutu yake.
 
Chakubanga na Bashiru ni wabunge wa wapi??
 
Katazo ni batili kwahiyo wana uhalali wa kuli-defy
 
Kwani Bashiru na Polepole ni wabunge wa majimbo yapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mikutano iko kikatiba,chadema wasihofu kitu,Mahakama ya ICC ipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…