Kuhusu Umasikini au Hali Duni ya Uchumi

Nundu_Tanzania

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
811
349
Umasikini ni hali ya mtu, familia au jamii kushindwa kumudu mahitaji ya lazima ya chakula, mavazi na malazi.

Umasikini, hatahivyo unapofafanuliwa hauwezi kuacha kuhusishwa na "Akili" na "Mwili".

Katika mtu, kilicho cha lazima ni Akili pasipo kutenganishwa na mwili kwa ajili ya manufaa yake na ya wote.

Manufaa ya mtu na ya wote hayatokani na mwili wake au wao, lakini akili.

Pasipo Akili mwili hauna chochote cha manufaa. Hivyo ni bure. Kazi ya mwili pasipo akili siyo ya manufaa.

Umasikini katika hali zake mbali mbali pia ngazi zake siyo jambo la bahati mbaya, siyo laana, wala siyo mkosi, lakini ni makosa dhidi ya akili.

Makosa dhidi ya akili yana chanzo chake katika wazazi yaani watangulizi au mtu mwenyewe.

Kushughulika na mwili ili kuondoa umasikini ni suala lisilowezekana kwa sababu mwili hutegemea akili. Mwili usipotunzwa inavyotakiwa huharibu akili.

Makosa dhidi ya akili ni yale yanayoharibu au jeruhi " Ukweli wa Imani" na "Ukweli wa Ndoa".

Uharibifu katika imani na katika ndoa hufanya uharibifu katika uchumi. Hivyo umasikini au hali duni ya uchumi.

Licha ya kwamba umasikini chanzo chake ni makosa dhidi ya akili, lakini una ngazi ya familia, jamii au taifa.

Katika ngazi ya familia kama ilivyo ngazi ya jamii au taifa kwa sababu ni kosa dhidi ya akili, umasikini unahusu mfumo wa maisha unaopanuka zaidi wa wana familia au ndugu wa damu moja upande wa ukoo wa baba na wa mama.

Suala la kuwa na uchumi, uwezo wa uchumi haliwezi kufikiwa kwa juhudi ya mtu mmoja peke yake pasipo matengenezo ya mfumo wa kufaa kiakili na kimwili wa ndugu wa damu moja upande wa ukoo wa baba na wa mama.

Katika hili mwelekeo ni kutafiti mambo ambayo kwa kuyaishi au kuyatekeleza au kuyaendea yanaharibu au yanajeruhi akili.

Pasipo kufanya utafiti na kubaini mambo ambayo kwa yenyewe au moja kwa moja au siyo moja kwa moja kwa kuyaishi yanaharibu akili haiwezekani kuondokana na umasikini.

Familia ndiyo sehemu ya kwanza kabisa ambapo utafiti wa mambo yapi kwa yenyewe, moja kwa moja au siyo moja kwa moja kwa kuyaishi au kiyaendea au kuyatekeleza yanaharibu akili.

Pasipo kwanza familia kuishi mfumo ulio wa mafaa ya kiakili na kimwili haiwezekani kwa familia yenyewe, jamii na taifa kupata maendeleo.

Umasikini au hali duni ya uchumi ya taifa haiwezi kufafanuliwa au kuchunguzwa bila kutazama mifumo ya familia moja moja ya taifa hilo inavyoandaa watu wake kiakili na kimwili.

Ni vigumu na kwa kweli haiwezekani kuondokana na umasikini au kupata maendeleo pasipo kutatua mambo yote au mifumo ambayo kwayo na kwa jinsi yake inaharibu akili.

Hatuwezi kukataa kuwa ndoa ndiyo chanzo cha familia. Hili kwa lenyewe ni jambo jema na takatifu.

Lakini je, mfumo wa ndoa katika jamii zetu kwa jinsi yake unaandaa watoto kiakili na kimwili?

Mfumo wa ndoa ni jambo nyeti sana kwa ustawi wa jamii. Mfumo wa ndoa kwa jinsi yake kama hautokani na misingi na mafundisho yanayokubalika kiakili na kimwili huharibu moja kwa moja akili ya watoto wanaozaliwa.

Mfumo wa ndoa usiyotokana na misingi na mafundisho yanayokubalika kimaadilia au na akili, kwa wenyewe ni umasikini na katika taifa lililo katika mfumo huo haiwezekani kuondoa umasikini.

Umasikini uwe ni wa mtu au familia au jamii au taifa haiwezekani kuutenga na makosa dhidi ya akili.

Nyajibu za kwanza za mtu mmoja mmoja, familia na viongozi katika kuondoa umasikini, hali duni ya uchumi zinapaswa ziwe zile zinazotafuta na kutafiti mambo au mifumo ambayo kwa kuishi au kuiendea au kuitekeleza ina haribu akili.

Kama ambavyo umasikini chanzo chake ni makosa dhidi ya akili ndivyo pia uchumi hauwezekani pasipo imani.

Suala la imani linaeleweka kwa namna mbali mbali hivi kwamba kuna mgawanyiko wa imani na mafundisho ya imani.

Imani kwa yenyewe ni moja isiyo gawanyika au isiyo mbali mbali. Imani inahusu Mungu.

Ni makosa au upotofu kufikiri imani sawa na saikolojia au sayansi.

Kwa kukosa elimu na uelewa wa mambo watu wanaelewa mambo ya saikolojia au sayansi kama imani.

Sayansi au saikolojia hizi kwa zenyewe ni rasilimali ambazo haziwezi kuwa chanzo cha mtu, isipokuwa ni kwa ajili ya kumsaidia na kumwendeleza mtu katika mahitaji yake na ya wote.

Kama ilivyo kwa saikolojia au sayansi chanzo chake ni imani kwa Mungu. Ndivyo pia uchumi hauwezi kupatikana nje ya imani.

Kama akili ya ufahamu isivyoweza kutenganishwa na milango ya fahamu pia akili ya kina haiwezi kutenganishwa na imani.
 
Umasikini husababishwa na vitu vikuu vitatu,
1.Kudumaa kwa akili.-Watu hubaki kuwa masikini kwa kutojiendeleza kitaaluma,hivyo akili hudumaa na hali finyu ya uoni wa maisha na kutekwa na mazingira yaliyomzunguka.

2.Kudumaa kwa Serikali.-Serikali inaweza kuwaongoza raia wake kuzinduka kwa kuwatengeneze mazingira wezeshi ya kuondoa umasikini ikiwemo kuwapa gawio la mapato watu maalumu kama walemavu,wagonjwa na wasio na kipato kwa kukosa kazi.

4.Makadirio ya Mungu mwenyewe-
Yote hayo hapo juu, kwa nchi za kiafrika ni kama kumpigia mbuzi gita.Sisi uwezo wetu wa kufikiri na kuendesha mambo ni duni mno .Na inapotokea tumesoma ndo inakuwa mbaya zaidi maana wengi wetu hupata kichaa .
Mtawala bora wa kiafrika ni bora wale machifu na watu wasiokwenda shule.Hutumia elimu za jadi kuendeshea mambo kiafrika.
Haya ni maumbile,Umasikini kwetu ni Maumbile hata kama tuna Rasilimali za kutosha kwa kuwa hatuna kabisa AKILI na uwezo wa kuzimudu hizo rasilimali.
 
ivi kwan pombe aileti umaskini
Unwaji pombe ni sehemu ya kudumaa kwa akili,
Mtu mwenye akili timamu hawezi kuacha matumizi ya muhimu ya familia na maisha yake na akawa cha pombe, ila akili yake inamapungufu na huko ndo kudumaa kwenyewe.

Matajiri hunywa pombe ili kuzimua ukichaa wa akili zao pia,badala ya kuwasaidia watu wenye shida huelemea kwenye starehe na ulevi,huko nako ni kudumaa pia. Pesa unazo lakini Maisha ni ya kilevi levi, wako hata wasomi na madaktari bingwa walevi ,nao hao pia wamedumaa akili.
 
Umasikini husababishwa na vitu vikuu vitatu,
1.Kudumaa kwa akili.-Watu hubaki kuwa masikini kwa kutojiendeleza kitaaluma,hivyo akili hudumaa na hali finyu ya uoni wa maisha na kutekwa na mazingira yaliyomzunguka.

2.Kudumaa kwa Serikali.-Serikali inaweza kuwaongoza raia wake kuzinduka kwa kuwatengeneze mazingira wezeshi ya kuondo
Ni kweli "Kudumaa kwa Akili" ndio husababisha umasikini.

Lakini, bila shaka kuna sababu za kudumaa kwa akili.
 
Back
Top Bottom