Kuhusu suala hili la madini kama ni kweli Rais ana njia njema angeanza kuwachukulia wahusika hawa

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Kuhusu suala hili la madini. Tatizo kubwa katika sekta ya madini ni sheria.
Kama ni kweli Raisi ana njia njema katika kuwachukulia wahusika wote angeanza wahusika hawa.

Wanasheria wote waliowahi kuhudumu wizara husika na wanasheria wakuu wa serikali kutoka 1998 mpaka leo wachunguzwe.
Mawaziri wote waliowahi kuhudumu wizara ya nishati na madini tangu mwaka 1998 mpaka leo wachunguzwe kuhusu kuhusika ama kutokuhusika kwao.
Makatibu wakuu waliowahi kuhudumu wizara husika tangu mwaka 1998 mpaka leo. Wachukuliwe hatua stahiki
 
Hawezi kufanya hivyo kwasabababu anachofanya sasa hivi ni sarakasi tu za siasa. Kwa kifupi jamaa nchi imemshinda. Mkapa ndie mwizi mkubwa aanze naye. Yeye atawale tu asitufanye watototo wadogo
 
Back
Top Bottom