Kuhusu simu za kichina TECNO HD Series

Kuhusu simu za kichina TECNO HD Series

alsaidy

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2009
Posts
334
Reaction score
90
Wadau naomba kuwakilisha kama ifuatavyo:

Nilikuwa natafuta simu aina ya samsung double line, nilipofika dukani muuzaji akaanza kunisifia kuhusu toleo jipya la TECNO HD na akanipa modeli HD 51 kwa kweli i was so impressed na performance yake kila kitu basic kipo na camera yake ni 1.3 mega pixel lakini quality ya picha yake it's amaizing very clear.

Simu inakuja na battrey 2,earphone,charger pamoja na cover yake original. Baada ya kuanza kuzifuatilia kwa umakini nikakuta watu wengi wanatumia hii brand ya TECNO katika simu za kichina kushinda brand yoyote ile. Nchi ya jiran kenya hususan Mombasa zimeteka soko kubwa la watumiaji wa simu.

Ukiacha mambo mengine ina kamata internet bila ya matatizo yoyote na ina java ambayo unapata software nyingi za ku down load kwenye neti.

Wenye experience zaidi watujuze kuhusu hizi simu na upatikanaji wake kwa wingi hasa hizi HD series
 
ulinunua bei gani mkuu.nimevuthwa nayo.
 
Mchina ni mchina tu!!
kuna jamaa mmoja akiuzaga gari anaanza kukuambia lina kiti, kiti, una adjust, adjust mbele na nyuma, lina side mirror, side mirror una adjust, taa zaidi ya moja, yaaani makorokoro kibao ambayo ni ya kawaida tu mkuu!!
Simu inategemea na matumizi na hobby yako.
 
ulinunua bei gani mkuu.nimevuthwa nayo.

Mkuu nilinunua 98,000 ila maduka mengine mpaka 110,000 unatakiwa utembee maduka mengi upate kuelewa bei nzuri.

Nimenunua bei hiyo kwa Tanga lakini kwa dar nina hakika itakuwa pungufu ya hapo.
 
Mchina ni mchina tu!!
kuna jamaa mmoja akiuzaga gari anaanza kukuambia lina kiti, kiti, una adjust, adjust mbele na nyuma, lina side mirror, side mirror una adjust, taa zaidi ya moja, yaaani makorokoro kibao ambayo ni ya kawaida tu mkuu!!
Simu inategemea na matumizi na hobby yako.

To be honest sio kila anachotengeneza mchina ni kibovu kuna vengine vina ubora unaostahili.

Najua mkuu unazungumza hivyo kwa kuwa hujawahi kuitia mkononi hiyo simu ninayozungumzia ila katika pita pita zako madukani ijaribu kidogo then utarialize in terms of quality.

Pikipiki yangu mchina aina ya sanya ambayo pia imechukua soko kubwa hasa mwanza kutokana na kuwa na ubora unaostahili.

Kwa msimamo huu sio kwanba nakataa kabisa kwamba mchina sio fake ila kuna baadhi za bidhaa wanazotengeneza zina ubora unaostahili.

Hili halina shaka kwani naamini wadau wengi wataniunga mkono.
 
Mchina ni mchina tu. Ina kelele kama Sub woofer

Unafikiri hii simu ninayozungumza iko kama hizo zinazopiga kelele??

Za kelele sio kama hazipo ila sio kwa brand ya TECNO hususan toleo hili la HD. Ni mchunguzaji mzuri wa simu na nina interest hasa katika maswala haya.

I have to admit hizi simu za TECNO HD series nimezikubali.
 
Alsaidy tuwekee picha ya hiyo cm hapa,wewe utakuwa mwarabu unapromote biashara,ndo una tenda ya kuzileta nchini au?
 
umeshainunua sifa yake si utainona mwenyewe, au unataka tukupe shavu?.
 
To be honest sio kila anachotengeneza mchina ni kibovu kuna vengine vina ubora unaostahili.

Najua mkuu unazungumza hivyo kwa kuwa hujawahi kuitia mkononi hiyo simu ninayozungumzia ila katika pita pita zako madukani ijaribu kidogo then utarialize in terms of quality.

Pikipiki yangu mchina aina ya sanya ambayo pia imechukua soko kubwa hasa mwanza kutokana na kuwa na ubora unaostahili.

Kwa msimamo huu sio kwanba nakataa kabisa kwamba mchina sio fake ila kuna baadhi za bidhaa wanazotengeneza zina ubora unaostahili.

Hili halina shaka kwani naamini wadau wengi wataniunga mkono.

Mkuu upo sahihi, mchina anatafuta pesa, atakutengenezea kitu ubora mdogo kwa sababu akikutengenezea cha ubora mzuri huwezi nunua, lakini bado hata hiyo hela yako ndogo anaitaka.
Bidhaa za mchina ambazo ni bora zinauzwa zaidi US na Ulaya. sisi tutabaki kulaumu mchina feki, kumbe tunataka vya bei rahisi.
 
Ebana hiyo Mi simu ya Techno inaboa kinoma! KARIAKOO nzima imejaa! Hadi Mid-com sikuizi haipo pale mtaa wa kongo wapo hao Techno.
 
Alsaidy tuwekee picha ya hiyo cm hapa,wewe utakuwa mwarabu unapromote biashara,ndo una tenda ya kuzileta nchini au?

Wenye experience zaidi watujuze kuhusu hizi simu na upatikanaji wake kwa wingi hasa hizi HD series

Mkuu naona hukupata maudhui ya kuanzisha forum hii................

Tafadhali kuwa makini siku nyingine usidandie gari kwa mbele...
 
Tuwekee picha

HD51-d.jpg

Haya mkuu picha hiyo......

Kwa maelezo zaidi http://www.tecnotelecom.com/SeriesProducts.htm
 
kiukwel hii cm ni nzuri na haina kelele kama cm zingine za kichina.
 
Back
Top Bottom