demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,250
- 15,116
Habari zenu wana jamvi.
Ikumbukwe kuwa Mwezi Agosti kutakuwa na mtanange wa Ngao ya Hisani.
Ngao ya hisani ni mtanange unaokutanisha "Bingwa wa LigiKuu Bara" na "Bingwa wa kombe la shirikisho (Azam Sports Confederation Cup)".
Kwa mantiki hiyo sote tunajua kuwa Bingwa wa LigiKuu Tanzania Bara kwa msimu uliopita ni Dar es salaam Young Africans SC na Bingwa wa kombe la shirikisho ni Simba SC. Hivyo mechi inayotarajiwa na wengi ni kati ya Dar Young Africans vs Simba SC.
Nimejikuta napatwa na maswali ya kujiuliza mno kuhusu kama Klabu ya Simba SC itaweza kutokea Uwanjani siku hiyo au la. Ikiwa sote tunakumbuka kuwa Klabu nzima kuanzia uongozi wa juu , wa kati, wachezaji na hata viongozi wa chini walitangaza kutomtambua bingwa yeyote wa LigiKuu msimu wa 2016/17 (na hata kuzigomea medali za mshindi wa pili) mpaka Rufaa yao kutoka FIFA ijibiwe.
Je wataweza kutokea Uwanjani kwa ajili ya kuwavaa Mabingwa wa kihistoria wa VPL Tanzania.... na kuamua "KULA MATAPISHI YAO"?
Au watagoma kutokea kabisa wakisimamia msimamo wao wa kutowatambua Wana Jangwani kama Mabingwa halali wa msimu wa 2016/17?.