Kuhusu Ngao Ya Hisani: Je Simba SC wataamua kumeza matapishi yao wenyewe?

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Habari zenu wana jamvi.

Ikumbukwe kuwa Mwezi Agosti kutakuwa na mtanange wa Ngao ya Hisani.

Ngao ya hisani ni mtanange unaokutanisha "Bingwa wa LigiKuu Bara" na "Bingwa wa kombe la shirikisho (Azam Sports Confederation Cup)".

Kwa mantiki hiyo sote tunajua kuwa Bingwa wa LigiKuu Tanzania Bara kwa msimu uliopita ni Dar es salaam Young Africans SC na Bingwa wa kombe la shirikisho ni Simba SC. Hivyo mechi inayotarajiwa na wengi ni kati ya Dar Young Africans vs Simba SC.

Nimejikuta napatwa na maswali ya kujiuliza mno kuhusu kama Klabu ya Simba SC itaweza kutokea Uwanjani siku hiyo au la. Ikiwa sote tunakumbuka kuwa Klabu nzima kuanzia uongozi wa juu , wa kati, wachezaji na hata viongozi wa chini walitangaza kutomtambua bingwa yeyote wa LigiKuu msimu wa 2016/17 (na hata kuzigomea medali za mshindi wa pili) mpaka Rufaa yao kutoka FIFA ijibiwe.

Je wataweza kutokea Uwanjani kwa ajili ya kuwavaa Mabingwa wa kihistoria wa VPL Tanzania.... na kuamua "KULA MATAPISHI YAO"?
Au watagoma kutokea kabisa wakisimamia msimamo wao wa kutowatambua Wana Jangwani kama Mabingwa halali wa msimu wa 2016/17?
.
 
Yaani kila ishu bongo ni siasa tu mikia walisema hatuwezi kuchukua medali ya mshindi wa pili ilhali wao ndio mabingwa na wakasema kupitia Domo lao chafu Mnara kuwa yanga wamefanya sherehe hivyo ijiandae kufanya sherehe ya kurudisha kombe msimbazi na medali sasa vyote hivyo havijarudishwa swali linakuwa palepale mikia italamba matapishi yake na kama ni hivyo basi Haji mnara aombe radhi watu wa football kwa ujinga aliouongea hapo nitamuona kidogo amestaarabika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zamani tulikuwa na mtani Jembe,yanga wakapigwa 5 na Mnyama.mkemia awapime Yanga unaweza kukuta mkojo wake umechanganyika na wa Simba,sio kwa kojo lile
 
Ile ilikuwa janja ya viongozi wakiongozwa na Hans ili kukwepa mapinduzi.... mikia wanadanganywa mno na viongozi wao.Saiv washasahaulishwa kwa kumsajili Niyonzima
 
Watashiriki kama mabingwa na Yanga kama mshindi wa pili, shida ni nini?
Hujui ulisemalo.

Hiyo mechi ni ya Bingwa wa Ligi Kuu na Bingwa wa Kombe la Shirikisho, hivyo basi kama Simba wanadai kuwa wao ndio mabingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho, wanastahili kucheza na Makamu Bingwa wa Kombe la Shirikisho ambaye ni Mbao FC na siyo Yanga.

Endapo Simba wataingiza timu dhidi ya Yanga, wajue kuwa wanamtambua Yanga kama Bingwa wa Ligi Kuu na si vinginevyo.

Nawashauri Simba walambe matapishi yao waje uwanjani siku hiyo tuwaoneshe kazi hadi waanze kufikiria kufumua kikosi chao cha wazee.

Go go - Young Africans SC International.
 
Habari zenu wana jamvi.

Ikumbukwe kuwa Mwezi Agosti kutakuwa na mtanange wa Ngao ya Hisani.

Ngao ya hisani ni mtanange unaokutanisha "Bingwa wa LigiKuu Bara" na "Bingwa wa kombe la shirikisho (Azam Sports Confederation Cup)".

Kwa mantiki hiyo sote tunajua kuwa Bingwa wa LigiKuu Tanzania Bara kwa msimu uliopita ni Dar es salaam Young Africans SC na Bingwa wa kombe la shirikisho ni Simba SC. Hivyo mechi inayotarajiwa na wengi ni kati ya Dar Young Africans vs Simba SC.

Nimejikuta napatwa na maswali ya kujiuliza mno kuhusu kama Klabu ya Simba SC itaweza kutokea Uwanjani siku hiyo au la. Ikiwa sote tunakumbuka kuwa Klabu nzima kuanzia uongozi wa juu , wa kati, wachezaji na hata viongozi wa chini walitangaza kutomtambua bingwa yeyote wa LigiKuu msimu wa 2016/17 (na hata kuzigomea medali za mshindi wa pili) mpaka Rufaa yao kutoka FIFA ijibiwe.

Je wataweza kutokea Uwanjani kwa ajili ya kuwavaa Mabingwa wa kihistoria wa VPL Tanzania.... na kuamua "KULA MATAPISHI YAO"?
Au watagoma kutokea kabisa wakisimamia msimamo wao wa kutowatambua Wana Jangwani kama Mabingwa halali wa msimu wa 2016/17?.
Kwani kanuni zinasemaje wakisusia huo mchezo?
 
Back
Top Bottom