Kuhusu miradi mikubwa wilaya ya Chato

Miradi mingine huwa inaamuliwa na taifa?
Nielewe mimi sikupinga miradi kwenda huko hata kama miradi yote itasimama kwanza tukajenga Chato ni sawa tuu lkn tuamue kama Taifa na si kikundi kidogo cha watu
 
Kuna habari kwamba kuna miradi mbali mbali inayoendelea wilayani Chato kwa yule anaefaham anisaidie yafuatayo:

1 Aina ya Mradi
2 Gharama zilizotumika/zinazotumika
3 Utaratibu ulotumika utowaji wa tenda
4 Kikao cha bunge kilichopitisha miradi hiyo/utaratibu uliotumika kuichagua
5 Vipi miradi hiyo itakavyotusaidia kujikwamua kiuchumi
Ni hayo tuu.
Acha wivu. Mbona huulizi kuhusu miradi ya sehemu zingine kama Kigamboni, Arusha, Mbeya etc
 
Hivi Chato wanaishi nyani??? Mbona hamtaki wao wapate maendeleo yoyote?

Wapate lakini kwa utaratibu mzuri unaozingatia vigezo vya kiuchumi; sasa ukijenga International airport pale unategemea tija ipi pale, wasafiri wa kimataifa watakwenda Chato kufanya nini kitongoji kidogo kama kile na uchumi wake duni vile!
 
Hivyo vyote ulivyouliza bado, ila miradi itatekelezwa tuu, mtake msitake...

Hapa kazi tu, kuhojiana baadae...

Cc: mahondaw
 
Kuna habari kwamba kuna miradi mbali mbali inayoendelea wilayani Chato kwa yule anaefaham anisaidie yafuatayo:

1 Aina ya Mradi
2 Gharama zilizotumika/zinazotumika
3 Utaratibu ulotumika utowaji wa tenda
4 Kikao cha bunge kilichopitisha miradi hiyo/utaratibu uliotumika kuichagua
5 Vipi miradi hiyo itakavyotusaidia kujikwamua kiuchumi
Ni hayo tuu.
Kwani chato ipo kenya?mbona mishipa.ya shingo inakutoka sana
Tafuta kitabu cha bajeti ya Tamisemi 2015/16,16/17,17/18 na 18/19 utapata majibu yako
Mnawaandama watanzania wenzenu kama vile hawastahili chochote?au kutoa Rais imekua nongwa?
 
Hakuna shaka yotote naendeleo makubwa kwenda kule,ila ingekua kwetu mlele halafu mimi ndio Pope,cha kwanza kufanya ni kuhakikisha wakulima wote wanalima kilimo chenye tija cha umwagiliaji mara mbili kwa mwaka,Wakulima wapate pesa za kuendesha maisha yao...ili walipe kodi vizuri.
 
Hivi Chato wanaishi nyani??? Mbona hamtaki wao wapate maendeleo yoyote?
Kwani wanaoishi kijijini kwenu wao sio waTanzania. Mbona hujawapelekea taa za kuendeshea punda. Au hapo kijijini hamna punda?

Basi nenda kaombe mpewe 'flyover' za kupitisha mikokoteni. Si kupanga ni kuchagua tu mkuu, au unasemaje!

Mimi kwetu nimewaeleza waTanzania hawa, kipaumbele chetu kikuu hapa ni njia za baiskeli. Hatuhitaji lami, ni njia tu nzuri za kuendeshea baiskeli zetu. Nina'wish' nami ningekuwa na sauti ya kuamru tu na yakawa kama mwanakijiji toka Chato aliyonayo. Nisingehitaji taratibu zozote za mizungusho inayotuchelewesha kutimiza miradi hiyo.
 
Kuna habari kwamba kuna miradi mbali mbali inayoendelea wilayani Chato kwa yule anaefaham anisaidie yafuatayo:

1 Aina ya Mradi
2 Gharama zilizotumika/zinazotumika
3 Utaratibu ulotumika utowaji wa tenda
4 Kikao cha bunge kilichopitisha miradi hiyo/utaratibu uliotumika kuichagua
5 Vipi miradi hiyo itakavyotusaidia kujikwamua kiuchumi
Ni hayo tuu.
We una mradi gani wa kukufanya japo toilet uione ama umejipa u watch dog wa miradi ya chato
 
Kwani chato ipo kenya?mbona mishipa.ya shingo inakutoka sana
Tafuta kitabu cha bajeti ya Tamisemi 2015/16,16/17,17/18 na 18/19 utapata majibu yako
Mnawaandama watanzania wenzenu kama vile hawastahili chochote?au kutoa Rais imekua nongwa?
Majibu haya hayaondoi harufu mbaya inayoambatana na miradi ya namna hiyo.

Sasa ngoja nikupe mkakati na ukamweleze. Akitimiza hivi, nami nitaungana nawe kushangilia licha ya kuwepo harufu mbaya:

WaTanzania wengi wa Chato ni wakulima na wavuvi/wafugaji.

Kamwambie atenge fungu, kama bilioni moja tu hivi ya pesa za madafu. Aamuru wizara ya kilimo itoe wataalam 'Grade one' wanaojua vyema kilimo cha mazao wanayolima hawa waTanzania wenzetu wa Chato. Awape hawa wataalam muda wa miaka miwili/mitatu wafanye kazi na wakulima wa Chato na pawe na "Mashamba Darasa katika kata zote za Wilaya hiyo

Hawa wataalam, yeyote atakayeshindwa kuwaelimisha wakulima kilimo chenye tija katika muda huo anatumbuliwa.

Haya nenda kamueleze hayo, huenda nawe unaweza ukaambulia chochote, maana tunakuona humu mda mrefu ukipiga zumari tu lakini njaa ipo palepale.
 
Mradi huu unaujua!? Na wanyama wanasombwa na magari kutoka hifadhini kwenda Burigi hapo
IMG_20190613_010858.jpeg
 
Tatizo kuna watu mnaamini mikoa mingine ni watu mafukura wasio stahili maendeleo yoyote, kwamba ikijengwa hospitali ya wilaya Chato ni nongwa? Wakati huo huo kuna wilaya zaidi ya 65 zimejengewa hospitali ndani ya awamu ya Magu.

Wakijenga bandari ndogo Chato kwa ajili ya usafiri wa meli na uvuvi nongwa pia, mkoa mzima unapakana na ziwa ila hauna usafiri wa uhakika, acheni roho za chuki na ubaguzi.

Aliye na chuki na mbaguzi katokea chato_OVER
 
Back
Top Bottom