Kuhusu Mama Samia Bond za CRDB

Kuhusu Mama Samia Bond za CRDB

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
1,289
Reaction score
2,190
Tulitangaziwa na kuaminishwa na CRDB juu ya Mama Samia Bond kuwa ni uwekezaji mzuri unaotoa faida 13% baada ya miezi mitatu.

Mimi niliona ni fursa na nikaweka fedha zangu mwanzoni mwa Januari, 2025 nikitarajia kuwa baada ya miezi mitatu nitawekewa gawio langu la 13%.

Mpaka leo sijawekewa gawio langu na tayari imepita miezi mitatu.

Ninaiomba CRDB itujibu na kama haiwezekani basi wanirudishie fedha zangu nizielekeze mahali panapoweza kuzalisha faida zaidi kama biashara.

Hii ni taarifa ya mwisho baada ya hapa natarajia kuwachukulia hatua CRDB.
 
Mzee baba hamna hela nyepesi kiasi hicho, yaani ulipwe asilimia 13 ya fedha yako Baada ya miezi 3 hio ni zaidi ya kamba.

Ko 1m una pata laki 1 na 30 ×12=4 time months ni laki 5 na 20, aisee wahindi si ndo wange peleka mabilioni yao chap!

*halafu usi kute uli peleka milioni 2 yako 😂🤣, karudie kusoma kitabu chao Cha vigezo, masharti na mgawanyo wa uwekezaji.

ni 13 percentage kwa Mwaka, inayo lipwa kidogo kidogo kila baada ya miezi 3.
 
Tulitangaziwa na kuaminishwa na CRDB juu ya Mama Samia Bond kuwa ni uwekezaji mzuri unaotoa faida 13% baada ya miezi mitatu. Mimi niliona ni fursa na nikaweka fedha zangu mwanzoni mwa Januari, 2025 nikitarajia kuwa baada ya miezi mitatu nitawekewa gawio langu la 13%. Mpaka leo sijawekewa gawio langu na tayari imepita miezi mitatu. Ninaiomba CRDB itujibu na kama haiwezekani basi wanirudishie fedha zangu nizielekeze mahali panapoweza kuzalisha faida zaidi kama biashara. Hii ni taarifa ya mwisho baada ya hapa natarajia kuwachukulia hatua CRDB.
Lete mkataba unaosema watakupa 13%
 
Kuna 100M yangu nimeweka humu january naona hawajalipa gawio 3M April kuna aliyefanikiwa kutoa hela humu.
 
Tulitangaziwa na kuaminishwa na CRDB juu ya Mama Samia Bond kuwa ni uwekezaji mzuri unaotoa faida 13% baada ya miezi mitatu. Mimi niliona ni fursa na nikaweka fedha zangu mwanzoni mwa Januari, 2025 nikitarajia kuwa baada ya miezi mitatu nitawekewa gawio langu la 13%. Mpaka leo sijawekewa gawio langu na tayari imepita miezi mitatu. Ninaiomba CRDB itujibu na kama haiwezekani basi wanirudishie fedha zangu nizielekeze mahali panapoweza kuzalisha faida zaidi kama biashara. Hii ni taarifa ya mwisho baada ya hapa natarajia kuwachukulia hatua CRDB.
Hakuna riba za 13% kwa miezi mitatu nchi hii.

Hiyo 13% ni ya mwaka.

Labda useme mliambiwa mtakuwa mnapewa gawio la pesa yako kila baada ya miezi 3, ila ujue 13% ya pesa huongezeka baada ya mwaka.
 
Back
Top Bottom