Kuhusu kutumia single cpu with mult monitor

james marco

JF-Expert Member
Aug 2, 2017
208
167
Jamani napenda kuwauliza kuhusu kutumia CPU moja kwenye monitors tofauti ili kila moja ili kila client aweze ku access services mbalimbali make hapa nipo hapa nataka kufungua internet cafe msaada jamani
 
Unatumia software za virtualization, sema hizi zinafanya machine iwe slow hasa hizi desktop za kizamani. Mifano ya software Ni Kama

-Ibik aster
-softxpand mini frame
-Vmware workstation etc

Ila hakuna maajabu Kama desktop ipo slow ukiweka multi user wateja wako watapata speed ya konokono na desktop zenye nguvu Bei Ni ghali.

Mfano desktop nzuri yenye processor ya kisasa unaipata kwa around laki 4 mpaka 5 kkoo, Bei hio hio unaweza nunua desktop za kawaida 3 ama 4, na huwezi ukatumia desktop ya kawaida ku serve watu wengi.
 
Kama walivyoeleza hapo juu, lazima uwe na mashine yenye specs zilizoshiba,
Cha kuongezea ukiachana na Virtual machine softwares kama vmware, virtual box na nyenginezo za kaliba hiyo zina limitation kadha wa kadha.
Kuna kitu inaitwa KVM hii ni Kernel Based Virtual Machine, siwezi nikaelezea kernel kwa ufupi ukaelewa ila hii kvm imekuwa merged na kernel ya linux ina uwezo mkubwa sana na features nyingi ukilinganisha na hizo virtual machines nyengine kama vmware.
Mfano
Unaweza kupass hardware kwenye guest os, mfano pc yako ina graphics card 3, unaweza set card ya kwanza ikae kwenye OS labda windows 7, card ya pili ikae kwenye windows 8 na card ya 3 ikae kwenye windows 10 na zote zina function simultaneously bila kutegemea os yoyote, hayo ni kwa ufupi unaweza fatilia zaidi.
Kingine ni resolution unapata full resolution ya card husika tofauti na vm za kawaida zinazotumia shared video memory kwa baadhi ya OS.
 
Back
Top Bottom