Boniphace Kichonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 1,606
- 1,956
Wadau tumeshuhudia nchi jirani kama Rwanda wakifanya utaratibu wa kupiga kura ya maoni kwa lengo lakuongeza kipindi cha kukaa madarakani kwa Rais wa Rwanda. Naamini waliofanya hivyo walitumia haki yao ya kidemokrasia na hasa baada ya kuridhishwa na utendaji kazi mzuri wa Kiongozi wao mpendwa Mhesh. Paul Kagame. Kwa kuzingatia sababu hizo kwanini Tanzania tusiige mfano wa jirani zetu ili kumuwezesha Kiongozi wetu mpendwa kupata muda wa kutosha kutuletea maendeleo nchi yetu na kutuondoa kwenye umaskini? Nawasilisha