Kuhusu Kiwanda cha Sukari Mtibwa-Mvomero-Morogoro

Kuhusu Kiwanda cha Sukari Mtibwa-Mvomero-Morogoro

muta ngegi

Senior Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
191
Reaction score
161
Salaam Wanajamiiforum!
Ndugu Wanajamii forum,bila kupoteza muda naomba kuuliza Nina ndugu yangu anataka kwenda kuomba kazi ya shambani Mtibwa(Kama kibarua),sasa kaja kwangu kuuliza kuwa msimu unaanza lini na unaisha lini.

Jibu nikawa sina,hivyo nimekuja kwenu kuomba anayejua aniambie na utaratibu wa kuomba kazi za vibarua shambani upoje ili niweze kumpa majibu sahihi.

Natanguliza shukrani.
 
Mwambie aende dakawa kuna kiwanda kipya mashamba ya miwa yapo sehemu inaitwa mkulazi atakimbia mwenyewe kazi za kumwaga
 
Mwambie aende dakawa kuna kiwanda kipya mashamba ya miwa yapo sehemu inaitwa mkulazi atakimbia mwenyewe kazi za kumwaga
Shukrani sana Kiongozi,ndo maana jamii forum ni kisima cha mambo mengi
 
Back
Top Bottom