Zinduna
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 2,377
- 3,394
Kwa takribana mwezi mzima nimekuwa nikitafakari kuhusu kuanzisha kipindi kipya cha Hard Talk. Kipindi hicho kitajikita zaidi kwenye maswali magumu kuhusiana na Mapenzi, Mahusiano na Urafiki.
Hapa mshiriki atakuwa na wakati mgumu wa kujibu maswali magumu na yenye kuumiza kichwa kutoka kwangu na kwa wadau wa MMU. Mada itategemea zaidi kuhusu tukio lolote lililowahi kuwekwa humu MMU likaumiza watu vichwa au maisha ya ndoa au mahusiano ya mshiriki.
Kitatofuatiana sana na Zinduna Talk Show na kitakuwa kikirushwa hewani kila Ijumaa.
Hebu wana JF nipeni maoni yenu kuhusu kipindi hicho kwamba mngependa kiendeshwe vipi?