Kuhusu Kigali - Rwanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuhusu Kigali - Rwanda

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mgombezi, Jan 18, 2012.

 1. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wana JF.

  Kwa yeyote ambaye ameshawahi kutembelea Kigali - Rwanda au wenyeji wa huko wanaweza kunijulisha juu ya haya yafuatayo:
  1. Usafiri wa kuelekea huko kwa njia ya barabara (basi) kutokea Dar, Je unapatikana ?, Basi gani, ratiba, nauli, muda wa safari na mengineyo muhimu.
  2. Huduma za malazi; kiasi gani, guest house nzuri na salama, bei ya vyakula na mengineyo muhimu kufahamu.
  3. Sehemu za kutembelea (vivutio) na sehemu nyinginezo muhimu ambazo naweza kutembelea kwa kujifunza.
  Natanguliza shukrani kwa maoni yenu.
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu, long time no see you
   
 3. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu, we acha tu. Nimemiss sana jukwaa hili kwa muda kidogo. But now I'm back.
   
 4. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Mkuu sijawahi kwenda kwa Bus ila nimekua Kigali several times..ni mji mzuri msafi sana..nimekua naenda na Rwanda Air..sehemu nzuri za kutembelea na nyama choma na bia ni Carwash..hilo ni eneo limetulia sana na jina linaitwa hivo hivo sijui kwanini..

  Kingne hotel pale ni aghali sana nenda fikia Impala ni safi na salama ina internet na mambo yote ya kisasa dola 40 per nite.
   
 5. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante Mkuu, ningependa kwenda kwa barabara (basi) napata ku-explore mambo mengi. Sifahamu Impala itakuwa ni star ngapi, naweza kupata accommodation ya USD10 - 20, sihitaji sana mambo ya kisasa, nataka usalama tu. Kuhusu internet naweza kutumia modem?, mtandao gani huko?
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Ukirudi toka huko utwambie ma-deal tafadhali.
   
 7. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ndiyo natafuta taarifa muhimu nione kama naweza kujipanga na kutembelea huko, sitaacha kukupasha mkuu.
   
 8. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wana JF hakuna wanaoishi Rwanda humu?
   
 9. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,093
  Likes Received: 1,264
  Trophy Points: 280
  Karibu mkuu..

  Rwanda ni pazuri,salama na wala usipate hofu...
   
 10. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante Mtu Chake, ningeshukuru sana kama ungeweza kunipa jambo dondoo mojawapo katika haya maswali yangu, sitaki kukurupuka;

  • Usafiri wa kuelekea huko kwa njia ya barabara (basi) kutokea Dar, Je unapatikana ?, Basi gani, ratiba, nauli, muda wa safari na mengineyo muhimu.
  • Huduma za malazi; kiasi gani, guest house nzuri na salama, bei ya vyakula na mengineyo muhimu kufahamu.
  • Sehemu za kutembelea (vivutio) na sehemu nyinginezo muhimu ambazo naweza kutembelea kwa kujifunza.
   
 11. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,093
  Likes Received: 1,264
  Trophy Points: 280
  Mie pia cjawahai kwenda Kigali kwa Bus...zaidi ya KQ au Rwanda Air
  ila ni mjini mzuri wenye baridi kdg...kuhusu malazi inategemea na hotel unayofikia mm huwa nafikia Alpha palace au Sports View

  sehemu za kutembelea ni Gisenyi na Kivu kwa utalii...maeneo hayo kuna Ndege wanapatikana rwanda wanaitwa Inyange na Pia unaweza kuona sokwe mtu...Rwanda ni Nchi ya Milima na Mabonde...pia unaweza kutembelea ziwa kivu..njian utaona vitu vingi sana..mlima Kivu ambao ni volcano hai..inafuka moshi hadi leo  Sehemu za kuruka disco usiku kuna sehemu inaitwa KBC.....(Kigali Bussiness Centre)...Au Cardrac ambayo iko karibu na Carwash
  pia si mbaya ukitembelea Kigali Memorial Centre ukajionea kumbukumbu ya Mauji ya Kimbari...Jengo la Bunge la Rwanda ambapo ndiko kikosi cha kwanza cha jeshi la RPF lilikaa kusubiri muaafaka wa Arusha ..kabla ya ndege ya Rais kulipuliwa...

  we fika mkuu utajufunza vitu vingi sana

  na Kigali kuna warembo wazuri balaa

  Ni hayo tu mkuu
   
 12. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mimi nimetumia njia zote. Ndege na basi kwa nyakati tofauti. Kwa ndege lazima kupitia Uganda/Entebbe au Nairobi. Mbali ya Rwanda Air pia KQ na ndege moja ya Uganda inakwenda huko.
  Kwa njia ya basi, nenda Ubungo. Kama unapanda basi la moja kwa moja utachoka..unless wewe hupendi ku-view sites. Ila uzuri panda gari pale Ubungo la kwenda Kahama. Unalala pale Kahama. Asubuhi unapanda vipanya hadi eneo linaitwa Benaco (just 15kms from Tanzania Rwanda Border -Rusumo). Kutoka Kahama hadi Benaco ni masaa matatu hadi matatu na nusu. Pale Benaco unaweza kupanda taxi (za jumla ya watu4),gharama haizidi elfu3. Ukifika Border unapanda basi za Kigali. Kawaida ni mwendo wa masaa 3-5 kwa gari la abiria kutoka mpakani (Rusumo) hadi Mjini Kigali. Majina ya mabasi ni vigumu, lakini recently basi la TAWAQAL lilikuwa linaenda huko tokea Dar (Ubungo), sijui inawezekana yapo mengine pia. Kwa vyovyote vile lazima unalala Kahama
   
 13. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante sana Mtu Chake, kwa maelezo haya. Japokuwa hujaweka gharama za hoteli ulizofikia, ungefanya hivyo ningeshukuru zaidi. Nitaka ku-plan safari yangu, hivyo ni vyema nifahamu itanigharimu kiasi gani?
   
 14. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,093
  Likes Received: 1,264
  Trophy Points: 280
  hotel nilizofikia kdg ziko juu..Alpha Palce ni Dola 55,na Sports View ni dola 80..hapa nilihama baada ya kupata ya dola 55
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  4 army generals are under house arrest today. That is the business which pays alot more than any other business in that place.
   
 16. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante Sana BUBE kwa maelezo haya, nitashukuru kama utaweza kuniwekea bayana gharama za usafiri zifuatazo:

  DAR - KAHAMA = .................. (Japokuwa naweza kuuliza Ubungo)
  KAHAMA - BENACO = .....................
  BENACO - RUSUMO = Tsh 3000 ok
  RUSUMO - KIGALI = .................

  Natanguliza shukrani, ukipata wasaa unaweza kunipa dondoo nyinginezo ukioanisha na gharama zake.
   
 17. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nashukuru!
   
 18. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Thanks 4 info!
   
 19. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [Mgombezi

  Tafadhali angalia majibu yangu kuhusu Nauli. QUOTE=Mgombezi;3164479]Asante Sana BUBE kwa maelezo haya, nitashukuru kama utaweza kuniwekea bayana gharama za usafiri zifuatazo:

  DAR - KAHAMA = ...Tzs 35,000............... (Japokuwa naweza kuuliza Ubungo)
  KAHAMA - BENACO = Tzs 12,000.....................
  BENACO - RUSUMO = Tsh 3000 ok
  RUSUMO - KIGALI = ..Hapa sijui na kumbuka franks za Rwanda ni strong kuliko madafu ya kitz. Btn Airtel inafanyakazi kule! Unless kumbebadilika siku za karibuni.

  Natanguliza shukrani, ukipata wasaa unaweza kunipa dondoo nyinginezo ukioanisha na gharama zake.[/QUOTE]
   
 20. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  [/QUOTE]

  Asante sana kwa taarifa hii ya muhimu sana, umekuwa msaada sana katika plan yangu, ukikumbuka jambo lolote la muhimu kunijuza tafadhali nidondoshehe hapa.
   
Loading...