Kuhusu huyu Baba Jamani.!

Kuhusu huyu Baba Jamani.!

mkuu piga picha kama angeonekana hapa duniani yeye mmoja tu. halafu watu wote duniani wana shida zao wanahitaji awatatulie. wapange foleni !!
Ni baba yao lakini,hawezi kuwashindwa na hata zamu ikiwa sana 8 usiku mie ningesubiri tu. Au vipi.
 
Ni baba yao lakini,hawezi kuwashindwa na hata zamu ikiwa sana 8 usiku mie ningesubiri tu. Au vipi.
mkuu kwa mtazamo wako uko sahihi, niliongelea huyo jamaa aliesema kwamba haonekani. na mimi nikamuhoji, je endapo kama angeonekana kama jinsi tulivyo mimi au wewe, halafu binadamu wamfuate kila mmoja na shida zake..!!
 
MASHARTI YAKE..

Kutokusemea Uwongo

Kutokuwa Mzinzi.

Kutokuwa Mchawi

Usiwe Mseng’enyaji.

Usiwe Mlevi.

Usiwe Mwongo

Usilipize kisasi wala kushindwa kusamehe

Usipende MALI na ANASA kuliko NENO lake.

ANAPENDA..

Utafakari na kujifunza NENO lake usiku na Mchana

Umpende kwa Moyo wako wote

Umpende Jirani yako kama Nafsi yako

Uwatembelee Wafungwa hasa walioonewa

Uwaone Wagonjwa

Uwasaidie maskini na Wajane

Uwalishe chakula wenye njaa

Uwavishe maskini

ANASHANGAA..

Vile usemavyo unampenda , kumbe kusema kwako ni mdomoni, lakini moyoni hauko naye.

Ulivyo rahisi kurubuniwa na yule Adui na kukimbilia kwa Waganga wapiga Ramli.

Namna unavyosumbuka na Maisha wewe mwenyewe bila kumshirikisha YEYE wakati ndiye aliyekuumba..

Jinsi unavyopenda sana MALI kuliko NENO lake wakati huna uhakika wa kuiona kesho.

Ulivyoshupaza shingo kujiwekea HAZINA nyingi hapa DUNIANI ambapo Nondo na kutu huviharibu na kisha Wezi huvunja na kuiba.

Jinsi unavyotumia muda mwingi kufanya mzaha mzaha wa mambo na usitumie hata dak 5 kwa siku kumtafakari yeye maana ndiye aliyeyabeba maisha yako kiganjani mwakle.

Kuwa wa Kwanza kumkimbilia jirani ama nduguyo pale unapopatwa na majaribu, wakati Ukifariki leo hii majirani na ndugu zako hao watasema "Yote tumwchie Mungu maana ndiye mjuzi wa yote".

ANAKUTAKA KUFANYA HAYA..

Umkiri yeye kuwa ndiye Bwana na Mwokozi wa Maisha yako

Uache kabisa kutenda dhambi, kufanya mazaha juu yake kwa kumdhihaki..

Umpokee na kumruhusu kuingoza NAFSI yako bila kutegemea akili zako pekee

Ujifunze NENO lake na kulitafakari Usiku na Mchana.

Umrudie yeye na kuyashika maelekezo yake kuhusu MAISHA yako.

Kila Wakati umtafakari yeye, umfanye kuwa nguzo ya Maisha yako Usiku na Mchana.

Uyakabidhi kwake maisha yako, uwe mwaminifu hata Kufa.

Upunguze kuwa busy sana kuhusu maisha haya, kupelekea kumsahau na kumuweka pembeni kwa masuala yote kuhusu wewe, wakati huijui hata kesho yako itakuwaje.

JINSI ALIVYO..
Ni mpole na Mwingi wa Rehema, Husamehe yote wala hakumbuki tena makosa yako baada ya kusamehe. Ni Mfariji wa wajane, Baba wa Yatima, Mwenye kurejesha tumaini palipovunjika Moyo na Mpatanishi.Ndiye aliyeziumba Mbingu na Nchi, Mwenye kujua hatma ya Maisha yako na yangu, Aliyekufanya uwepo leo katika hii Dunia, Mkuu kuliko Wakuu wa Ulimwengu huu.

Si mwingine, bali ni Mungu Baba, aliyeziumba Mbingu na Nchi kwa neno lake, atakayewahukumu Wanadamu WOTE sawasawa na Matendo yao hapa DUNIANI. Na atakayetoa hukumu ya HAKI kwa kila mmoja wetu.

Mwenye Masikio na Asikie.!
Khaa! hili nalo.
 
Tatizo la huyu baba ni moja tu,huwa haonekani anatenda,anaagiza,anaamuru,lakini humuoni ng'o.
Let's assume leo hii aonekane, Duniani patakalika? Yaani kama Malaika wake tu wakishuka toka Mbinguni Dunia hutetemeka, kwa tetemeko, vipi mwenyewe sasa?!
 
Huyu baba ana tatizo moja kubwa sana.... Ni baba mwenye wivu, anataka apendwe yeye tu na wala tusiwe na mababa wengine
 
Let's assume leo hii aonekane, Duniani patakalika? Yaani kama Malaika wake tu wakishuka toka Mbinguni Dunia hutetemeka, kwa tetemeko, vipi mwenyewe sasa?!
Patakalika tu,si ni baba anawatembelea wanae,nini matetemeko mbona yapo tu mkuu,aje aone shida zetu.
 
Huyu baba ana tatizo moja kubwa sana.... Ni baba mwenye wivu, anataka apendwe yeye tu na wala tusiwe na mababa wengine
Tena anasema hivi.."Usijifanyie sanamu kwa ajili yako mwenyewe kwa mfano wowote mbinguni wala duniani au katika chini ya maji. Wala kujiinamisha mbele yao au ibada yao, kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. "
 
Bora umeshusha hicho kifungu kabisa. Sasa hapa najiuliza sisi wanae tutajifunza nini sasa toka kwake? maana nijuavyo mini wivu hauna maana yeyote
 
Bora umeshusha hicho kifungu kabisa. Sasa hapa najiuliza sisi wanae tutajifunza nini sasa toka kwake? maana nijuavyo mini wivu hauna maana yeyote
Ni muhimu kuelewa jinsi neno “wivu” lilivyotumika. Matumizi yake katika Kutoka 20:5 katika kuelezea Mungu ni tofauti na jinsi limetumika kuelezea dhambi ya wivu (Wagalatia 5:20). Wakati sisi tunalitumia neno “wivu”, tunalitumia kuwa na maana ya tama ya kitu cha mtu ambacho hatuna. Mtu anaweza kuwa na wivu au kumwonea wivu mtu mwingine kwa sababu yeye ana gari zuri au nyumba (miliki). Au mtu anaweza kuwa na wivu au tamani mtu mwingine kwa sababu ya baadhi ya uwezo au ujuzi huyo mtu mwingine anao (kama vile uwezo wa riadha). Mfano mwingine ni ule kwamba mtu mmoja anaweza kuwa na wivu au tamaa ya mwingine kwa sababu ya urembo wake.

Katika Kutoka 20:05, siyo kwamba Mungu ana wivu au tamaa kwa sababu mtu ana kitu ambacho anahitaji. Kutoka 20:4-5 inasema, “Usijifanyie sanamu kwa ajili yako mwenyewe kwa mfano wowote mbinguni wala duniani au katika chini ya maji. Wala kujiinamisha mbele yao au ibada yao, kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu ...” Onyo ni kwamba Mungu ni wa wivu wakati mtu anatoa kitu kwa mwingine ambacho ni haki kwake.

Katika mistari hii, Mungu anazungumza juu ya watu wanaotengeneza sanamu na kuziinamia kwa kuziabudu badala ya kumpa Mungu ibada anayostahili peke yake. Mungu anamiliki ibada na huduma ambayo ni yake. Ni dhambi (kama Mungu anavyosema katika amri hii) kuabudu au kutumikia kitu kingine chochote zaidi ya Mungu.

Chanzo :Ni kwa nini Mungu ni Mungu wa wivu?
 
Ahsante sana ndugu, sasa ninaelewa kwa nini Mungu ana wivu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom