Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 972
- 1,150
MASHARTI YAKE..
Kutokusemea Uwongo
Kutokuwa Mzinzi.
Kutokuwa Mchawi
Usiwe Mseng’enyaji.
Usiwe Mlevi.
Usiwe Mwongo
Usilipize kisasi wala kushindwa kusamehe
Usipende MALI na ANASA kuliko NENO lake.
ANAPENDA..
Utafakari na kujifunza NENO lake usiku na Mchana
Umpende kwa Moyo wako wote
Umpende Jirani yako kama Nafsi yako
Uwatembelee Wafungwa hasa walioonewa
Uwaone Wagonjwa
Uwasaidie maskini na Wajane
Uwalishe chakula wenye njaa
Uwavishe maskini
ANASHANGAA..
Vile usemavyo unampenda , kumbe kusema kwako ni mdomoni, lakini moyoni hauko naye.
Ulivyo rahisi kurubuniwa na yule Adui na kukimbilia kwa Waganga wapiga Ramli.
Namna unavyosumbuka na Maisha wewe mwenyewe bila kumshirikisha YEYE wakati ndiye aliyekuumba..
Jinsi unavyopenda sana MALI kuliko NENO lake wakati huna uhakika wa kuiona kesho.
Ulivyoshupaza shingo kujiwekea HAZINA nyingi hapa DUNIANI ambapo Nondo na kutu huviharibu na kisha Wezi huvunja na kuiba.
Jinsi unavyotumia muda mwingi kufanya mzaha mzaha wa mambo na usitumie hata dak 5 kwa siku kumtafakari yeye maana ndiye aliyeyabeba maisha yako kiganjani mwakle.
Kuwa wa Kwanza kumkimbilia jirani ama nduguyo pale unapopatwa na majaribu, wakati Ukifariki leo hii majirani na ndugu zako hao watasema "Yote tumwchie Mungu maana ndiye mjuzi wa yote".
ANAKUTAKA KUFANYA HAYA..
Umkiri yeye kuwa ndiye Bwana na Mwokozi wa Maisha yako
Uache kabisa kutenda dhambi, kufanya mazaha juu yake kwa kumdhihaki..
Umpokee na kumruhusu kuingoza NAFSI yako bila kutegemea akili zako pekee
Ujifunze NENO lake na kulitafakari Usiku na Mchana.
Umrudie yeye na kuyashika maelekezo yake kuhusu MAISHA yako.
Kila Wakati umtafakari yeye, umfanye kuwa nguzo ya Maisha yako Usiku na Mchana.
Uyakabidhi kwake maisha yako, uwe mwaminifu hata Kufa.
Upunguze kuwa busy sana kuhusu maisha haya, kupelekea kumsahau na kumuweka pembeni kwa masuala yote kuhusu wewe, wakati huijui hata kesho yako itakuwaje.
JINSI ALIVYO..
Ni mpole na Mwingi wa Rehema, Husamehe yote wala hakumbuki tena makosa yako baada ya kusamehe. Ni Mfariji wa wajane, Baba wa Yatima, Mwenye kurejesha tumaini palipovunjika Moyo na Mpatanishi.Ndiye aliyeziumba Mbingu na Nchi, Mwenye kujua hatma ya Maisha yako na yangu, Aliyekufanya uwepo leo katika hii Dunia, Mkuu kuliko Wakuu wa Ulimwengu huu.
Si mwingine, bali ni Mungu Baba, aliyeziumba Mbingu na Nchi kwa neno lake, atakayewahukumu Wanadamu WOTE sawasawa na Matendo yao hapa DUNIANI. Na atakayetoa hukumu ya HAKI kwa kila mmoja wetu.
Mwenye Masikio na Asikie.!