Kuhusu hali ya kiuchumi, Serikali ifanyeje?

Kuhusu hali ya kiuchumi, Serikali ifanyeje?

Nijitahidi kuepuka kurudia yaliyochangiwa na wengine. Sababu zingine ninafikiri ni pamoja na
1. Social unrest (hali ya wasiwasi katika nchi)
■ watu hawafanyi shughuri za uzalishaji ipasavyo sababu ya mambo ya bomoabomoa inayoendelea nchi nzima, mauaji yasiyo na maelezo, malumbano yasiyo na tija kati ya serikali na vyama vikubwa vya upinzani, nk
■ watu kukwepa kodi na hii kuifanya TRA itumie fedha nyingi ili kukusanya kodi (kitaalamu hali hii haitakiwi), mitambo ya Tra mara nyingi imeonekana kuwakera walipa kodi wengi, wafanya biashara hutumia zaidi ya siku moja kwenye kufuatilia mambo ya kodi.
2. Unemployment
■ majipu bila ajira kuziba mapengo baada ya kutumbua, lakini pia majipu mengine ni vipele, mfano zoezi la vyeti feki!
■ wafanyabiashara wakubwa kutokuwa na uhakika wa hatima zao, wengine kupunguza shughuri na kupunguza wafanyakazi, au kufunga biashara kabisa.
■ serikali kutoajiri kwa wakati kwa muda mrefu, ingawa watu wanaendelea kustaafu, kufariki, kuacha na kuachishwa kazi.
■ mishahara kiduchu/hafifu wakati mfumko wa bei za vitu muhimu uko juu, walaji wanalazimika kupunguza ulaji wa baadhi ya vitu
Katika mambo haya yote uwezo wa kununua (purchasing power) unakuwa mdogo kwa hiyo vitu vinavyokosa wanunuzi vinatoweka sokoni na kutengeneza unemployment.
3. Kukosekana kwa uongozi bora (No good governance). Hii inadhihirishwa kwa kutokuwepo uwazi ndani ya serikali, kukwepa uwajibikaji, kutokubali kukosolewa, nk. Matokeo
■ utalii ambao umewahi kuwa chanzo kikubwa cha mapato kudorora
■ kuweka vipaumbele kwa mambo yasiyo na nguvu kubwa ya kuamsha vichochezi vya ukuaji wa uchumi, mf wakuu wa mikoa kujihusisha zaidi na mambo ya kukijenga chama badala ya kukuza uchumi
■ kusababisha watendaji wamuogope mtu mmoja badala ya kuwahofu wananchi, mfano bunge kutotangazwa live, mawaziri hawawajibiki kwa wananchi kwa majibu wanayotoa.
■ kushindwa kuweka mikakati ya kuzuia ubadhilifu na badala yake kushughurikia matokeo baada ya hasara kutokea. Ruhusu upinzani ufanye kazi ya kupiga firimbi.

Zamani zile mwalimu wangu aliwahi kuniambia kuwa katika uchumi kuna kitu kinaitwa "multiplier effect". Mtihani ni kuifafanua katika kiswahili kitakacho eleweka. Kwa ufupi ni kwamba kila jambo dogo linalofanyika kuathiri uchumi (kwa kukuza au kupunguza) matokeo yake hujizidisha kwa msururu fulani. Mfano, ikiwa umemfukuza kazi mtu wa mshahara wa shg 400,000 maana yake ni kwamba umewafukuza kazi wale wote waliokuwa wakizalisha vitu ambavyo mtu huyu alikuwa akinunua kwao, lakini pia huko alikokuwa akinunua nao walizitumia kununua bidhaa kwa fedha hiyo nao kwa vile watashindwa kununua, mlolongo wa wazalishaji kutozalisha utaendelea. Sasa fikiria ufukuze watu milioni?
 
Nimefuatilia mnavyobishana......

Well, yeye Zitto ni mwanasiasa na alichokisema labda kipo biased na hana supporting datas na kwa lugha rahisi ni mwongo kwa maana ya kwamba kiwango cha collection ya mapato yetu hakijashuka to that extent i.e around Tshs 600bn for consecutively two months I. e July & August...

Likely, wewe ni mtumishi wa serikali na pengine ktk Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA ama Mnikulu wa Magufuli na kwa hiyo unaelewa makusanyo ya mapato halisi ya miezi hiyo ya July & august na mpaka wa jana, Septemba.....

Tuanikie hapa mkubwa kukata kilimilimi cha uongo wa wanasiasa wa jamii ya Zitto Kabwe.... Nimejaribu kucheki ktk website ya mamlaka, sijaona kitu na wala mbwembwe za kutangaza hata hazipo tena kitambo kirefu....

Inawezekana mnaweka ktk notebooks zenu mkubwa, tujulishe na sisi ili tumpuuze ZZK..!!
Mimi sina inside scoop yeyote. Ila, kwa kutumia ujuzi tu wa kawaida, unaweza kutambua kama Hazina ipo mufilis kwa kuangali soko la hati fungani kwa mfano. .
Financial markets zinaweza kukupa picha ya mzunguko wa fedha serikalini. Ukiangalia, kwenye website ya BOT utaona bei ya 10-year treasury bond kwa mfano ni kubwa kwa mwaka huu kuliko mwaka 2016 August na offers zilikuwa the same bilioni 111. Hii inamaanisha serikali haihitaji fedha kwa udi na ubani. It can trade at a higher price and not succumb to crappy deals.

upload_2017-10-9_16-22-4.png


Mwaka 2016, August bei ya hati hiyohiyo ilikuwa shilingi 71.3 kwa shilingi 100.

upload_2017-10-9_16-46-34.png
 
Nimefuatilia Comment ya Zitto kwenye page yake ya facebook na maudhui yake yaliyoletwa hapa JF, Zitto anaonya kwamba kwa mujibu wa source zake makusanyo na mapato ya serikali yameshuka kufikia around billion 600.
Nimesoma pahala kwamba humuamini Zitto, kwa nini unafuatilia comment zake? Na je unataka tujadili nini hapa JF...uongo wa Zitto?
Kusema kweli nimekuwa shocked, nikaona ni vyema kuanzisha uzi hapa JF nikiamini kuwa tunaweza kutoa mawazo yetu
Serikali ya awamu hii kupewa ushauri...tafadhali acha utani!
 
Nimefuatilia Comment ya Zitto kwenye page yake ya facebook na maudhui yake yaliyoletwa hapa JF, Zitto anaonya kwamba kwa mujibu wa source zake makusanyo na mapato ya serikali yameshuka kufikia around billion 600.

Kusema kweli nimekuwa shocked, nikaona ni vyema kuanzisha uzi hapa JF nikiamini kuwa tunaweza kutoa mawazo yetu Constructively ili kama yatawapendeza wenye maamuzi basi watachukua hili na lile ili kulifanyia kazi, na lau kama hayafai au hayatoshi basi sisi raia tutakuwa tumetimiza wajibu wetu wa kutoa mawazo na maoni yetu kwa mujibu wa katiba inavyoturuhusu.

Swali la Msingi je ni nini hasa huenda kimepelekea hali ya mapato kupungua

Na Je Tufanyeje sasa kama nchi na serikali ili mapato yaweze kuongezeka?

Nakaribisha mjadala!
Ninachompenda Zitto ni km kasuku wa kurudia vitu vya wazi na km mchina akiba au kusikia technologi aya mtu anawahi ktk soko na bidhaa cheap na ya low quality ya hiyo technologia. SASA ZITO KATOA ONYO KTK RESULT AMBAZO NI OBVIOUS? KUWA HELA INAYOKUSANYWA NI KIASI HIKI NA MATUMIZI NI KIASI HIKI? HUYU DOGO KM SIO CCM KUMTENGENEZA SIJUI KM KUNA KITU HAPA..

ONYO ANGETOA MIEZI KADHAA KWA KUANGALIA TRENDS ZENYE VIASHIRIA VYA KUUA MAPATO YA MBELENI NA KUONGEZA MATUMIZI MBELENI KISHA AWAPE ONYO KUWA KINACHOFUATIA KM HAWATABADILISHA MOJA MBILI TATU,WATAISHIA SEHEMU GANI. Sishangai km anasoma vitabu vinachoita mambo yaliyotendeka ni utabiri.
 
...lakini unamuamini uchwara na uongo wake alipoingia madarakani kilo ya sukari ilikuwa 5,000, kuna Wafanyajazi wa Serikali wanalipwa milioni 40 kwa mwezi aliyekuwa msajili wa hazina Lawrence Mafuru alivyokanusha na kusema yeye anaijua mishahara yote Serikalini na hakuna mfanyakazi anayelipwa 40 million akaishia kufukuzwa kazi.
Mimi sijaanza leo wala jana. Ni mjuvi na mara kenda kati ya kumi huwa the last man standing kwenye nyuzi nyingi tu. Look how irrelevant this thread is, in less than 24hrs. Tatizo hamtajifunza, ndiyo maana huwa mnapuuzwa tu.
 
Huna ujuvi wowote wewe zaidi ya kutetea uongo wa miaka nenda miaka rudi. Uchumi wa nchi unakua lakini hali halisi ya mtaani haionyeshi hivyo. Uongo uliokithiri miaka nenda miaka rudi na bajeti hewa.

Mimi sijaanza leo wala jana. Ni mjuvi na mara kenda kati ya kumi huwa the last man standing kwenye nyuzi nyingi tu. Look how irrelevant this thread is, in less than 24hrs. Tatizo hamtajifunza, ndiyo maana huwa mnapuuzwa tu.
 
Mimi nililoliona hasa na nasubiri Utafiti wa Wataalamu kuthibitisha null Hypothesis yangu ni kwamba:

Uamuzi wa kuhamia Dodoma utakuwa umetingisha Imani ya Investments ( Hususan Investors wa ndani), Wafanyabiashara waliokuwa wameinvest Dar hawana uhakika kama biashara zao zitaendelea kuchanua iwapo Maofisi na Watumishi wa Serikali wengi watahama kutoka Dar kwenda Dodoma, hii ni kutokana na kwamba Uchumi wa Dar kiasi kikubwa unachangiwa na serikali kuwepo hapa, kwa hiyo mzunguuko wa fedha ni mkubwa hapa, Watumishi wengi wa serikali wako hapa, hawa kutokana na mishahara yao na marupurupu yao bila shaka biashara kwa Dar zilikuwa zinaenda vizuri na hivyo Serikali kukusanya kodi ya kutosha kutoka mkoa huu!.

Sasa kitendo cha kuhamia Dodoma kwa ghafla au dhana tu ya kuhamia Dodoma, basi imefanya wafanyabiashara wa ndani kuscale back biashara zao, na Watu wamegeuka kuwa " Wahifadhi akiba zaidi kuliko watumiaji".

Kwa hiyo hii imepelekea wafanyabiashara kupunguza importation, matokeo yake lazima mzigo bandarini utapungua na serikali kukosa hela!!

What is the way forward?
Ni lazima serikali itoe incentive za kikodi ( importation) ili Wananchi waresume importation hususan kutoka China ili kuzinusuru biashara za sasa hivi zinazopumulia mashine na kurevive zile ambazo zimekufa, Hali ikishastabilize then serikali inaweza kurudi polepole katika tax regime yake ( importation taxes).

Serikali ikifanya hivi itakuwa ni kama Stimulus package kupitia unafuu wa kodi za forodha!

Busara ya kale inasema, Ili umkamue ngombe atoe maziwa mengi kesho, basi mlishe vizuri leo!!!

Watakufahamu wenye akili.
 
Huna ujuvi wowote wewe zaidi ya kutetea uongo wa miaka nenda miaka rudi. Uchumi wa nchi unakua lakini hali halisi ya mtaani haionyeshi hivyo. Uongo uliokithiri miaka nenda miaka rudi na bajeti hewa.
Basi wewe mwamini Ayatollah.
 
Mimi sina inside scoop yeyote. Ila, kwa kutumia ujuzi tu wa kawaida, unaweza kutambua kama Hazina ipo mufilis kwa kuangali soko la hati fungani kwa mfano. .
Financial markets zinaweza kukupa picha ya mzunguko wa fedha serikalini. Ukiangalia, kwenye website ya BOT utaona bei ya 10-year treasury bond kwa mfano ni kubwa kwa mwaka huu kuliko mwaka 2016 August na offers zilikuwa the same bilioni 111. Hii inamaanisha serikali haihitaji fedha kwa udi na ubani. It can trade at a higher price and not succumb to crappy deals.

View attachment 605950

Mwaka 2016, August bei ya hati hiyohiyo ilikuwa shilingi 71.3 kwa shilingi 100.

View attachment 605982

Sublime! Asante nimefaidika na elimu yako. Hii tu ndiyo inanipa fikra ya mwelekeo wa uchumi kuliko yote yaliyoandikwa hapa.
 
Tia akili kichwani achana na nyimbo za alinacha za uchumi kukua kwa namba za kupikwa huku Wananchi walio wengi wakiona hakuna mabadiliko yoyote na wakati mwingine hali kuzidi kuwa mbaya.

Basi wewe mwamini Ayatollah.
 
Thank
Hahahaha you made my day when failure comes it comes in ugly way

a
Thank you Bababikko I was just trying to think how things have been made ugly in this lovely land by cowards in leadership positions. Where will they hide together with their cronies over their ugly and shameful acts done against innocent political leaders once they are no longer in leadership position? How will they uproot the ugly seed of hatred they have planted in people's hearts and mind? Why don't they concentrate on issues that are important to the development of this beautiful nation with beautiful, polite, and humble people? The propagation of ungodly and undemocratic acts are the ones that are leading us to that ugly and shameful end.
 
Mimi nashauri serikali ifanye kila mbinu kuhakikisha hakuna diwani wala mbunge was chadema ataendelea kuwa madarakani na pia hakuna bunge live maana ndio chanzo hasa cha uchumi wa nchi kudumaa ,pia vyombo vya habari vinavyokosoa juhudi za kukuza uchumi vifungiwe milele maana ndio kikwazo kikubwa,kwa kuzingatia hayo uchumi utapaa kwa kasi ya kimbunga
 
Suala sio serikali ifanye nini? Suala ni wananchi wafanye nini?

Jawabu langu nitakwambia, tuache kupiga deals na tulipe kodi!
 
Suala sio serikali ifanye nini? Suala ni wananchi wafanye nini?

Jawabu langu nitakwambia, tuache kupiga deals na tulipe kodi!
Wananchi tunajuwa cha kufanya...tar 26 april beba biblia au msaafu ingia road mpaka kieleweke zaidi ya hapo serikali ituambie imefanya nini kabla ya tar 26 maana tunayo list ya vitu mbadala ila italazimu wakati tunafanya wao wawe watazamaji tu...
 
Back
Top Bottom