Kuhusu hali ya kiuchumi, Serikali ifanyeje?

Kuhusu hali ya kiuchumi, Serikali ifanyeje?

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2007
Posts
7,038
Reaction score
9,353
Nimefuatilia Comment ya Zitto kwenye page yake ya facebook na maudhui yake yaliyoletwa hapa JF, Zitto anaonya kwamba kwa mujibu wa source zake makusanyo na mapato ya serikali yameshuka kufikia around billion 600.

Kusema kweli nimekuwa shocked, nikaona ni vyema kuanzisha uzi hapa JF nikiamini kuwa tunaweza kutoa mawazo yetu Constructively ili kama yatawapendeza wenye maamuzi basi watachukua hili na lile ili kulifanyia kazi, na lau kama hayafai au hayatoshi basi sisi raia tutakuwa tumetimiza wajibu wetu wa kutoa mawazo na maoni yetu kwa mujibu wa katiba inavyoturuhusu.

Swali la Msingi je ni nini hasa huenda kimepelekea hali ya mapato kupungua

Na Je Tufanyeje sasa kama nchi na serikali ili mapato yaweze kuongezeka?

Nakaribisha mjadala!
 
Serikali inawatisha wawekezaji wakubwa na wafanya biashara unategemea nn? Wapo wafanyabisahara wameamua kusimamisha expansion ya biashara zao ili kusoma upepo kwanza maaana hawajui kesho serikali itaamua nini.

Mtu kama Bakharesa au Dewji akiona aliyofanyiwa Manji hata kama ana investment aliyotaka kufanya ni lazina ashike break.

Serikali ijilaumu yenyewe..na tunakoelekea hali itakuwa mbaya zaidi
 
Simuamini Zitto.
Unamuamini Rais??.....asingekuja na hizo figure na umeona hata TRA na serikali.....wameufyata kama wanabisha walete data hapa....!! Hali ni mbaya sana....utaona Dr Mpango ataondoka kwenda kukopa soon maana baada salary hakuna kinachobakia OC zote na pesa maendeleo hazipo tena!! Bajeti itasimama...kama mwaka jana.....hakuna kituu!!!
 
Mimi nililoliona hasa na nasubiri Utafiti wa Wataalamu kuthibitisha null Hypothesis yangu ni kwamba:

Uamuzi wa kuhamia Dodoma utakuwa umetingisha Imani ya Investments ( Hususan Investors wa ndani), Wafanyabiashara waliokuwa wameinvest Dar hawana uhakika kama biashara zao zitaendelea kuchanua iwapo Maofisi na Watumishi wa Serikali wengi watahama kutoka Dar kwenda Dodoma, hii ni kutokana na kwamba Uchumi wa Dar kiasi kikubwa unachangiwa na serikali kuwepo hapa, kwa hiyo mzunguuko wa fedha ni mkubwa hapa, Watumishi wengi wa serikali wako hapa, hawa kutokana na mishahara yao na marupurupu yao bila shaka biashara kwa Dar zilikuwa zinaenda vizuri na hivyo Serikali kukusanya kodi ya kutosha kutoka mkoa huu!.

Sasa kitendo cha kuhamia Dodoma kwa ghafla au dhana tu ya kuhamia Dodoma, basi imefanya wafanyabiashara wa ndani kuscale back biashara zao, na Watu wamegeuka kuwa " Wahifadhi akiba zaidi kuliko watumiaji".

Kwa hiyo hii imepelekea wafanyabiashara kupunguza importation, matokeo yake lazima mzigo bandarini utapungua na serikali kukosa hela!!

What is the way forward?
Ni lazima serikali itoe incentive za kikodi ( importation) ili Wananchi waresume importation hususan kutoka China ili kuzinusuru biashara za sasa hivi zinazopumulia mashine na kurevive zile ambazo zimekufa, Hali ikishastabilize then serikali inaweza kurudi polepole katika tax regime yake ( importation taxes).

Serikali ikifanya hivi itakuwa ni kama Stimulus package kupitia unafuu wa kodi za forodha!

Busara ya kale inasema, Ili umkamue ngombe atoe maziwa mengi kesho, basi mlishe vizuri leo!!!
 
MAGU hawezi kubali kitu kama hicho,

Utasikia fungeni tuu biashara
 
Tunaambiwa uchumi unapanda.ila ukiangalia dola 1ni sh 2000 na kitu.
Sasa najiuliza tangu magufuli aingie madarakani ni uchumi gani uliopanda.
Ameikuta dola sh 2000 na kitu.na mpaka sasa ipo hivyo hivyo.huu uchumi unapanda vipi?
 
nilizani kaongea asubuhi hii na kavideo unako

ila ni page umeiokota huko fb inst sijui.

mbona hata mimi naweza nkaanzisha page nkaweka pc za zito na mkanifollow km hamjielewi kumbe.

endeleeni kudis vitu hewa.
 
Serikali waache kutuaminisha uongo.

Swissme
 
Economic principles must be treated as economic principles and not political principles, ukikosea miiko ya uchumi tegemea anguko la kiuchumi, sehemu yoyote huwezi kuwachukia matajiri ili uwapandishe maskini never, tuna kila sababu ya kuahakikisha wachumi wanafanya kazi yao tena kwa uhuru, else tutaendelea kulia.
 
Unamuamini Sizonje??.....asingekuja na hizo figure na umeona hata TRA na serikali.....wameufyata kama wanabisha walete data hapa....!! Hali ni mbaya sana....utaona Dr Mpango ataondoka kwenda kukopa soon maana baada salary hakuna kinachobakia OC zote na pesa maendeleo hazipo tena!! Bajeti itasimama...kama mwaka jana.....hakuna kituu!!!
tukuamini wewe
Ila unaamini kilo ya sukari ilikuwa 5000 na Magu kaishusha mpaka 2500
Kwa hiyo nyie mnakubali na mnaamini makusanyo ya kodi yamepungua mpaka bilioni 600 kwa mwezi? That's absurd! Hamna kielelezo chochote mnachotumia zaidi ya majungu.
 
Wananchi wote wakipewa tax break, say VAT ishushwe kwa muda wa mwaka mmoja hivi to virtually 5% uchumi wa kila mwananchi utaongezeka kwa factor of the savings he will be enjoying from tax brake!
Mfano, wewe kwa mwaka unanunua bidhaa na hudumuma (household expenditure) zenye thamani ya milioni 20,000,000 ambazo unazilipia Vat ya karibu milioni nne. Unapopewa tax break (VAT:18%-5%=13%), ina maanisha utaweza kununua huduma nyingine zaidi na hivyo kuongeza mauzo ya biashara nyingine au utaweza kufanya Savings= Investment=2,600,000 na utaweza kufanya miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo itakuingizia fedha zaidi...
This is theoretically true. Shida inakuja, Iwapo wananchi watapewa tax break ya VAT, serikali itapata wapi mapato?
 
Kwa hiyo nyie mnakubali na mnaamini makusanyo ya kodi yamepungua mpaka bilioni 600 kwa mwezi? That's absurd! Hamna kielelezo chochote mnachotumia zaidi ya majungu.
Jibu kwanza,unaamini sukari ilikuwa 5000 na Magu kaishusha?
 
Swali la Msingi je ni nini hasa huenda kimepelekea hali ya mapato kupungua
Mapato yamepungua kwa kuwa transaction taxes ie VAT and the like zimepungua.
Kumbuka, the more you buy goods and services, the more govt makes money...
Wachumi wanasema kuna elacticity of demand. Baada ya serikali kukazania kukusanya kodi, bidhaa nyingi zilipanda bei hivyo watu wengi kupunguza kuzinunua. Hata Wakongo waliokuwa wananunua mali zao Kariakoo, nao nasikia walipunguza kununua bidhaa kutokana na ughali wake.
Kwa hiyo hapo there are two things involved. Serikali kupitia TRA ingeweka refund desk pale Kariakoo na pamoja na mpakani ili wale Wakongo wanaponunua bidhaa, waweze kuwa refund zile kodi walizolipia huku ili kushusha bei ya bidhaa. Hii itachochea kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa kariakooo.
The other thing cha kufanyika ni serikali kuangalia uwezekano wa kuwapa wananchi likizo ya kulipa kodi ya VAT kwa mda wa mwaka mmoja (kwa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi) ili kuchochea kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa hasa zile zinazozalishwa ndani ya nchi...
Hii pia itachochea ukuaji wa sekta ya uzalishaji wa bidhaa za ndani ya nchi... Tax holiday hiyo iwe ya kupunguza VAT from 18% to say 5% kwa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi kwa muda wa mwaka mmoja.
Hili pia litachochea kuongezeka kwa ajira maana viwanda na sekta ya uzalishaji itaweza kuongeza sales (uzalishaji) kitu ambacho kitafanya sekta ya uzalishaji kutoa ajira nyingi zaidi...
The net benefit kwa serikali kwenye hili itaweza kureflect kwenye corporate tax maana sekta ya uzalishaji itaweza kupata faida zaidi!
Lakini pia, if sales figures raises, the govt make more money aggregately.
Tufanye soda moja kwa sasa inauzwa Tsh 500, na wananchi wananunua say kreti laki moja kwa mwezi.
VAT kwenye soda itakapopungua Soda hiyo ingeweza kuuzwa Tsh 435! Na kungekuwa na uwezekano wa kuuza kreti laki moja na nusu kwa mwezi kutokana na punguzo hilo.
So iwapo kwa kreti laki moja, serikali ingepata VAT ya Tsh 2000*100,0000 =200,000,000
Kwa rate ya 5% VAT ingeweza kuwa Tsh 75,000,000! But with this VAT figure, we d expect the corporate profit to increase and compensate for the difference!
 
Back
Top Bottom