Mantombazane
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 579
- 367
Sakata la Escro limeitikisa serikali pamoja na kujidai pesa husika hazikuwa za serikali. Mawaziri na mwanasheria mkuu wamepoteza nyadhifa zao kutokana na kashfa hiyo. Baadhi ya watendaji nao wamechukuliwa hatua.
Kashfa hii ilihusisha hata maaskofu wa kanisa letu tena ni wale tuliowaheshimu sana kutokana na kauli zao za kujidai wanakemea ufisadi. Na mbaya kuliko zote uchafu huu umefanyika kupitia benki yetu ya kanisa.
La ajabu hatujaona kanisa likichukua hatua za kujisafisha badala yake tunaona watuhumiwa wakiendelea kutoa huduma ya kanisa.
Hii imetufanya baadhi yetu tudhani zile pesa kuna zingine walimpa mkuu wao kama wale wa magogoni ambao nao hawajachukuliwa hatua yoyote kwani wengi tunaona ni kama walitumwa tu kuchukua mzigo wa mwenye nyumba.
Vyovyote iwavyo hawa maaskofu wamelichafua kanisa kwani hata utetezi wao haujai hata kwenye kiganja cha mkono. Lakini kwakuwa kanisa limenyamaza kimya na kuwaacha waendelee na huduma ya kanisa, ni wazi kuwa kanisa nalo linajihusisha kutakatisha fedha kupitia kwa watendaji wake kama maaskofu husika na vyombo vyake kama benki ya mkombozi.
Kwakuwa kanisa limeamua kuwa sehemu ya uchafu ulifanyika Escrow, ni vizuri sasa likafunga mdomo kuikemea serikali inapotokea kuna ufisadi ambao kimsingi kanisa ndio wajibu wake kukemea.
Kesho hatutashangaa kuona hata pesa za madawa ya kulevya zinatakatishwa kupita vyombo vya kanisa na kubarikiwa na maaskofu. Tukifika hapo umuhimu wa kanisa unakuwa haupo tena!