Kuhusu dawa za MSD zilizoshindikana kupelekwa Muhimbili tangia mwaka 2012 , ukweli ni huu!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,598
36,023
CAG katika ripoti yake ameibua tuhuma nzito kuhusu MSD kushindwa kupeleka Muhimbili dawa za Tshs bilioni mbili tangia mwaka 2012. G Sam bila kupepesa nakuletea ukweli wa mambo!

Kwanza CAG alichogundua pale MSD ni kidogo sana! Kama ingekuwa uhalisia basi kuna dawa za zaidi ya Tshs bilioni sita tena zilizotakiwa kusambazwa kwenye hospitali za serikali tangia mwaka huo wa 2012 hazikusambazwa. Mnakumbuka sakata la dawa kupungua na nyingine kutokomea kabisa mahospitalini katika kipindi hicho? Nini kilichopo nyuma ya pazia?

Mwaka huo wa 2012 MSD ilitoa tenda ya kusambaziwa dawa kutoka katika viwanda vya ndani vinavyozalisha dawa za binadamu ikiwemo TPI na viwanda vingine (Kama mtakumbuka sakata la ARV feki)

Miongoni mwa dawa hizo zilizotakiwa ni dawa za "Bulk packaging" au dawa zinazopakiwa katika makopo ambazo ni dawa za vidonge. Hizo ndizo hasa na si nyingine alizogundua CAG ambazo zilikuwa na thamani ya Tshs bilioni sita (6) kwa pamoja.

Dawa hizo zilipofika MSD kutoka kwa waliopewa tenda zilichelewa pale MSD kwa muda kusubiri serikali itoe hela ili wazisambaze (Kama mtakumbuka sakata hili lilipigiwa sana kelele bungeni wakati huo! Kila mbunge kelele ilikuwa deni la MSD hadi waziri akakwamishiwa bajeti bungeni ili kushinikiza hela zitolewe. Nadhani kulikuwa na msukumo)

Wakati dawa hizo zikiwa pale MSD wafanyakazi (baadhi wengi wao) wakafanya ujanja kufungua makopo na kuiba dawa nyingi sana huku nyingine zikibakizwa kidogokidogo ndani ya makopo! Uongozi kuja kutahamaki dawa za makopo ndani ya bohari zimepungua mno! Watazisambazaje wakati ziko pungufu? Zitapokelewa? Mchawi akatafutwa! Waliopewa tenda wakashinikizwa kuwa walisambaza dawa pungufu ndani ya MSD! Imagine baada ya miaka miwili eti suppliers ndo wanaambiwa kuwa dawa za makopo walizosambaza MSD zilikuwa pungufu ndani ya makopo. (Hapa kuna nini? )

Kwakweli sakata hili lilisababisha fujo sana baina ya MSD na wasambazaji! Wapo walioingia mkenge wakapokea dawa hivyo zikarudishwa viwandani ili kuongeza zilizopelea na wapo waliokatalia mbali jambo hilo! Kwa hatua hiyo MSD wakawa wamefanikiwa kuukwepa mtego wa bilioni nne. Sasa huo wa bilioni mbili nadhani ulikosa mchawi na CAG akawakuta nao.

Katika kipindi hicho ndipo wafanyakazi wengi wa MSD walipata utajiri wa ghafla!

Mkurugenzi wao akashushwa cheo na aliyekuwa rais Kikwete.

Dawa kwenye mahospitali zikawa ni za shida sana kutokana na sakata hilo.

Hakuna jambo la kawaida ambalo lingezuia usambazaji wa dawa hizo. Lazima kulikuwa na shida na shida yenyewe ni hiyo!
 
Ukweli bila jina la huyo supplier
labda kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sawa , mmoja wa wasambazaji ametajwa hapo anaitwa TPI huyu ni wa arusha , ndiye alipata ile kashfa iliyotikisa dunia , ile ya kuwalisha waathirika mihogo badala ya ARV , baada ya hapo akafikishwa mahakamani , si unajua yaliyo mahakamani hayajadiliwi vijiweni ? basi tuishie hapa .
 
Mwambie bavicha mwenzako afute thread!
 
Kwa kawaida katika kupokea mizigo kutoka kwa mzabuni huwa kuna ukaguzi na mara nyingi hufanywa na kamati ya ukaguzi (inspection committee) na baadae 'inspection inspection certificate' inatolewa ili kuruhusu mzigo kupokelewa, suala la kujiuliza je huo mzigo ulikaguliwa na kupokelewa kwa mujibu wa taratibu?
Kama haukupokelewa kwa kufuata taratibu ni nani alilipia hizo dawa bila kufuata taratibu za upokeaji mizigo? Na kama hizo dawa zililipwa, je MSD walilipa kwa kutumia nyaraka zipi kama uthibitisho wa kupokea hizo dawa? Au mkataba uliruhusu dawa zilipwe kabla ya kupokea mzigo?
 
Inspection ilifanyika kwenye maboksi mkuu! Baada ya hapo wajanja wakafungua!
 
Tupe ushahidi wa delivery note kutoka kwa vendor kwenda MSD huo mwaka 2012 na pia tupe mawasiliano ya after two years kutoka MSD kusema dawa zilikuwa na mapungufu.

Kama huna hivi vitu basi hukufanya home work vizuri.
 
Back
Top Bottom