maiyanga1
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 1,317
- 1,790
Kama ilivyokuwa kwa wapiga debe kwenye stand mbalimbali nchini walivyoanza taratibu kujiingiza kwenye udalali wa kugombea abiria kiasi cha abiria kupelekwa gari nyingine na mizigo yake gari nyingine na sasa hawadhibitiki tena, ikaja kwa machinga ambao nao sasa haiwezekani tena kuwadhibiti kwa jinsi walivyojimilikisha maeneo mbalimbali ya kufanyia biashara.
Na sasa kuna tatizo kubwa la boda boda kutozingatia sheria za barabarani kiasi kwamba wanasabisha ajali. Mifano ipo mingi watu wanavyogongwa kwenye taa za barabarani au kwenye vivuko vya wenda kwa miguu. Pia sasa hata watoto wanaendesha bodaboda, lakini mbaya zaidi bodaboda wamekuwa waporaji. Kipindi cha Lugola ndio alitoa maelekezo kwamba bodaboda wasikamatwe na ni marufuku polisi kushikilia pikipiki vituoni.
Kwako Simbachawene bodaboda ni bomu jingine ambalo halitaweza kudhibitika.
Kauli ya "Tii sheria bila shuruti" iwahusu pia bodaboda.