EllySkyWilly
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 2,204
- 2,086
Habari za wakati na wasaa huu ndugu zangu.
Wakuu gharama ya usafiri ya kupitisha pipa moja la mafuta kwenye bomba kutoka Uganda mpaka Tanga ni dola 12.25 Yaani hiyo ndio nauli yake.
Katika hiyo nauli sasa ambayo ni dola 12.25 Tanzania atapata asilimia 60 alafu uganda atapata asilimia 40 ya nauli.
Kwanini sisi tutapata gawio kubwa la nauli.
kwasababu kilometa nyingi za bomba zipo upande wa Tanzania hivyo gharama za uendeshaji zitakua nyingi zaidi upande wa Tanzania.
Lakini pia bomba linapita katika mikoa mingi na wilaya nyingi zaidi katika ardhi ya Tanzania hivyo risk nyingi zitakuwa upande wa Tanzania. Mfano wa risk zinaweza kuwa kupasuka kwa bomba au risk nyingine yoyote inayoweza kuathiri afya au maisha ya Watanzania na hata viumbe vyovyote vilivyopo kwenye ardhi yet.
Hivyo lazima Uganda wapate asilimia chache.
Gharama za kuuziana mafuta sisi hazituhusu ni za wao wenyewe wenye mali na wawawekazaji wao.
Uganda watauza pipa zao za mafuta sisi tunawasafirishia kwa bomba hivyo sisi wanatupa pesa ya usafiri.
Ndugu zangu nawaombeni sana tusiwe tunapinga kila linalo fanywa na serikali. Huu mradi unafaida kubwa sana kwa watanzania na vizazi vyetu vijavyo. Hiyo asilimia 60 tutakayo ipata ni pesa nyingi sana. Na bado kuna ajira hapo zitakazo patikana ni nyingi mnoo.
Bado pia huko mradi unakopita pia wafanyabiashara mbalimbali mfano wa vyakula, vinywaji, nyumba za kulala wageni wote watafaidika na huo mradi.
Hivyo ndivyo maisha yanavyokwenda duniani tuache Jamani kuwa wapinzani wa mambo muhimu na ya maendeleo. Tuache kukosoa kosoa mambo muhimu na ya maendeleo.
Bali tujikite kuingalia Tanzania ya kesho itakuwaje kwaajili ya vizazi vyetu vijavyo na tuache kupoteza muda wa kukosoa Rais wetu bali tujikite kwenye kuungana naye ili maono aliyo nayo yaweze kutimia. Mambo anayofanya Mh. Rais ni makubwa mno na anastahili pongezi kwakweli.
Mambo ya kujenga na kuimarisha miundo mbinu ndio mambo muhimu duniani hilo ndilo walilo lifanya China miaka ya nyuma ndio sababu uchumi wao unakimbia kwa kasi sana.
Miundombinu ya uhakika na imara inaharakisha maendeleo ya nchi. Naomba tumwaachie Rais wetu Magufuli hii nchi hakika nawambia tutafika mbali sana. Huyu Rais ana akili nyingi mnoo.
Kama kuna mtu anaweza kufanya rushwa na asikamatwe Tanzania ya leo naomba ajitokeze na ajaribu kufanya.
Kama kuna mtu yeyote anaweza kufanya ufisadi kwenye taasisi yeyote ya serikali katika Tanzania ya leo naomba ajitokeze na ajaribu tuone kama hata julikana.
Ametumia akili nyingi mno Mhe. Rais , anastahili pongezi nyingi mno.
Basi nichukue fursa hii ndugu zangu na watanzania wenzangu kumwombea kura Rais Magufuli. Mitano tena kwa Magufuli.