Kuhama chuo binafsi kwenda cha serikali

Kuhama chuo binafsi kwenda cha serikali

Joined
Feb 14, 2022
Posts
68
Reaction score
105
Habari wakuu, naomba msaada
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika kozi ya diploma in Clinical Dentistry nikiendelea na masomo yangu katika Kigamboni City College of Health and Allied Sciences. Ni mnufaika wa mkopo kutoka HESLB.

Kutokana na gharama kuwa nyingi chuo hiki Cha private Nina nia ya kuhamia katika chuo cha serikali mwaka wa pili, haswa chuo cha Lugalo Military Medical School kwa ajili ya kuendelea na kozi hiyo hiyo.

Naomba kufahamu yafuatayo:

1. Mchakato wa kuhama kutoka chuo binafsi kwenda chuo cha serikali ukoje? Kuna taratibu gani rasmi zinazopaswa kufuatwa?

2. Kwa upande wa mkopo wa HESLB, nikiendelea na kozi hiyo hiyo katika chuo cha serikali, nitakuwa na nafasi ya kuendelea kupokea mkopo kama kawaida au kuna hatua maalum zinazopaswa kuchukuliwa?

Naomba msaada kwa yeyote mwenye uzoefu au taarifa sahihi kuhusu hili. Nawashukuru sana wakuu kwa msaada wenu na ushauri wenu wa kitaalamu.
 
Okay sasa ngoja nikupe msaada hapa.

1.Kuhamia Lugalo kama huna refaree ni ngumu sawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano. Lugalo ni miongoni mwa vyuo bora vinavyotoa hii kozi lakini hawachukui wanafunzi wengi mfano mwaka huu yupo janja nilijaribu kumpambania apate nafasi pale tena hapo kuna bi mother anafanya kazi Lugalo hospital na ana mazoea na viongozi wa pale ila ikagonga mwamba.

2.Kuhusu gharama za ada , Lugalo ni goverment lakini kipo chini ya jeshi hivyo ada yao wanajipangia wenyewe na gharama ya mwaka kama sikosei 2.72M ukiangalia ada ni sawa na hiko chuo chako.

3.Ndio ukihama utaendelea kunufaika na mkopo wako kama kawaida.

Ushauri wangu ni huu.

1.kwakua una mkopo nashauri tafuta chuo cha serikali achana na Lugalo ,kuna Mbeya,Iringa,Tanga nk vyote wanatoa elimu bora kwa gharama nafuu na ni rahisi kupata

2.Kuna chuo cha private kinaitwa Bulongwa kipo makete ni chuo bora sana kwa hiyo elimu kinamilikiwa na kanisa ila ada nafuu sana na elimu bora na ni chuo kikongwe ukitoka pale umeiva. Ada inacheza 1.6M kila kitu.

3.Kwa sasa focus na masomo ili ufaulu bila ya iupata supp usije ukaishia njiani. Maana kama utapata supp hutaweza kuhama mpaka uclear kimeo hiko.

Kila la kheri
 
Kila la kheriAsanteni sana wakuu kwa maelezo yenu ya kina na ushauri mzuri.
Nimeelewa kuhusu ugumu wa kuingia Lugalo, gharama zake, na hali ya mkopo. Nashukuru pia kwa kupendekeza vyuo mbadala kama Mbeya, Iringa, Tanga na Bulongwa.
Nitajikita kwenye masomo ili nifaulu vizuri na pia nianze kufuatilia vyuo vingine vya serikali kwa ajili ya kuhama.

Nawashukuru sana kwa msaada wenu. Mungu awabarik🙏
 
Kila la kheri nafikiri utawashauri vizuri wadogo zako waache kwenda vyuo vya ujanja ujanja.
 
Habari wakuu, naomba msaada
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika kozi ya diploma in Clinical Dentistry nikiendelea na masomo yangu katika Kigamboni City College of Health and Allied Sciences. Ni mnufaika wa mkopo kutoka HESLB.

Kutokana na gharama kuwa nyingi chuo hiki Cha private Nina nia ya kuhamia katika chuo cha serikali mwaka wa pili, haswa chuo cha Lugalo Military Medical School kwa ajili ya kuendelea na kozi hiyo hiyo.

Naomba kufahamu yafuatayo:

1. Mchakato wa kuhama kutoka chuo binafsi kwenda chuo cha serikali ukoje? Kuna taratibu gani rasmi zinazopaswa kufuatwa?

2. Kwa upande wa mkopo wa HESLB, nikiendelea na kozi hiyo hiyo katika chuo cha serikali, nitakuwa na nafasi ya kuendelea kupokea mkopo kama kawaida au kuna hatua maalum zinazopaswa kuchukuliwa?

Naomba msaada kwa yeyote mwenye uzoefu au taarifa sahihi kuhusu hili. Nawashukuru sana wakuu kwa msaada wenu na ushauri wenu wa kitaalamu.
Ingia www.nactvet.go.tz omba kuhama. Unaweza hamia chuo cha Mbeya pia nasikia pazuri. Uhamisho unafanyika mara 2 kwa mwaka. October wanapoanza semester 1 na April wanapoanza semester 2.
 
Habari wakuu, naomba msaada
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika kozi ya diploma in Clinical Dentistry nikiendelea na masomo yangu katika Kigamboni City College of Health and Allied Sciences. Ni mnufaika wa mkopo kutoka HESLB.

Kutokana na gharama kuwa nyingi chuo hiki Cha private Nina nia ya kuhamia katika chuo cha serikali mwaka wa pili, haswa chuo cha Lugalo Military Medical School kwa ajili ya kuendelea na kozi hiyo hiyo.

Naomba kufahamu yafuatayo:

1. Mchakato wa kuhama kutoka chuo binafsi kwenda chuo cha serikali ukoje? Kuna taratibu gani rasmi zinazopaswa kufuatwa?

2. Kwa upande wa mkopo wa HESLB, nikiendelea na kozi hiyo hiyo katika chuo cha serikali, nitakuwa na nafasi ya kuendelea kupokea mkopo kama kawaida au kuna hatua maalum zinazopaswa kuchukuliwa?

Naomba msaada kwa yeyote mwenye uzoefu au taarifa sahihi kuhusu hili. Nawashukuru sana wakuu kwa msaada wenu na ushauri wenu wa kitaalamu.
Bei gani tukuchangie
 
Back
Top Bottom