Kugombania maiti

Kugombania maiti

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
1,403
Reaction score
2,549
Habari zenu wakuu...

Huku kwetu kuna mgogoro wa kidini na issue yenyewe iko hivi...

Huyu dada alikubali kubadili dini ili apate cheo cha "mrs" . Alikubali kujifunika kichwa. Ndoa yao ilikuwa ya kisasa na watu tulikula na kunywa na kusaza siku hiyo.

Kama mjuavyo ndoa sio harusi, hawa wapendanao walichokana. Sijui sababu iliyowafanya wachokane ila nahisi ni ugumba wa huyu mgalatia. Hivyo walitengana kila mmoja akashika hamsini zake.

Dada wa watu amepumua pumzi yake ya mwisho ghafla hivi karibuni. Na hapo ndo mgogoro umeanza. Mmewe anataka azike kwao kwa taratibu za dini yake. Nduguze na mwanamke hawataki mtoto wao awekwe alazwe mwandani.

Unaambiwa pande zote zimechachamaa....wagalatia na wasaudia wanataka kupigana kisa maiti. Serikali imeingilia kati, tunasubiri uamuzi wa serikali.

Hivi kuna faida gani kugombania mtu mfu?

NB. Usioe wala kuolewa na mtu asie wa dini yako!

ASANTENI

Feedback: Mwanamke atazikwa kwao.
 
Kama walipeana talaka ndugu wa marehemu wana haki ya kuzika kwa dini yao.

Kama walitengana tuu basi mume ana haki ya kuzika kwa dini yake.

Unforgetable
 
"Acha wafu waziikane..." Vitabu vyasema..
 
Huyo aliukana Ukristu, wamzike tu kwa imani yake mpya.

Kama aliukana Ukristo hata akizikwa Kikristu haibadilishi hatima yake baada ya maisha ya hapa duniani.

Labda kama walipoachana alitubu akarudi kwenye Ukristu.
 
Bahati mbaya marehemu hana kauli shenzi hao wana chelewesha marehemu kuzikwa kama marehemu alibadili dini na akaachana na aliyekuwa mmewe na akurudi dini ya awali azikwe kwa imani yake
 
Kama waliachana kwa talaka basi ndugu wa mwanamke wana halali ya kumzika marehemu kwa imani yao

Halafu una uhakika gani kuwa alikuwa mgumba? Je kama huyo mwanaume ndiye mgumba?
Tatizo binadamu wabishi sana
 
Nimekuelewa sana, kuna jamaa alikuwa alikuwa akimsakama sana mkewe kuwa anajichelewesha kum bebea mimba ama ni mgumba, yule dada akahangaika anavyojua yeye, alilia, alisali na kufanya kila ajualo yeye mwisho wa siku akashika mimba, furaha ikarudi ndani ya nyumba na yule bi dada akafanikiwa kujifungua mtoto wa kike, bahat mbaya alipofikisha miaka mitano yule mtoto akawa na kansa, walihangaika sana na jamaa alikuwa na kipato kizur tuu, lakin mwisho wa yote mtoto alifariki, ilikuwa ni huzun isiyoelezeka sasa wakaanza harakat za kutafta mtoto mwingine, walihangaika sana, ila sfar hii mke akamwambia mumewe waende wote hospital, jamaa mwanzo alikataa kata kata ila mwisho akakubali, walipofika majibu yalikuwa tofauti sana, ni haya hapa, daktari alimwambia jamaa mkewe hana tatizo lakin yeye ndio ana tatizo na mbegu zake hazina uwezo wa kutungisha mimba milele, dah jamaa akapaniki, inawezekanaje nawalishapata mtoto, ilikuwa ni USA, Lakin mshikajia alienda mpaka Iran na India kutafta majib tofauti ila jibu lilikuwa lilelile yaan yeye anaweza kugonga ila ishu ya kuzalisha haiwezekan na haitowah kutokea..dah mchiz alidata na alifukuzwa kazi kwenye kitengo sababu alikuwa mwenye maamuz ya hasira na yeye ndiye kiongozi.
Kama waliachana kwa talaka basi ndugu wa mwanamke wana halali ya kumzika marehemu kwa imani yao

Halafu una uhakika gani kuwa alikuwa mgumba? Je kama huyo mwanaume ndiye mgumba?
 
Katika hili swala la ugumba asilia jinsia ya kiume ndo inaongoza kuliko ya kike ni vile tu mfumo dume ulishajiwekea kinga katika hili shutuma dhihaka na matusi humwangukia mwanamke

Sijui kwanini wanawake nao huchelewa kujiongeza.
 
Wote hao wana shida na wanapenda ligi...
kama mke umemuacha....hupaswi kugombea kumzika
Ndugu zake watamzika...

Na ndugu kama ndugu yenu alibadili dini..na hadi anakufa hakurudi dini yake ya zamani mnapaswa kuheshimu maamuzi yake na kumzika kwa dini yake mpya
 
Kama waliachana kwa talaka basi ndugu wa mwanamke wana halali ya kumzika marehemu kwa imani yao

Halafu una uhakika gani kuwa alikuwa mgumba? Je kama huyo mwanaume ndiye mgumba?
Nani kasema mwanamke alikuwa mgumba?
 
Back
Top Bottom