Kugombania daladala

Kugombania daladala

Watanzania ustaarabu hatuna na sijui ni lini watu watabadilika. Mbona nchi za wenzetu watu wanaweza kupanga foleni? Hapa Johanesburg SA watu wanapanda daladala kwa foleni na zaidi ya yote, hakuna konda...na watu wanakusanya pesa wenyewe na kumpa dereva....
Ah..naichukia sana Dar linapofikia jambo hilo la usafiri wa daladala!!!

Wakulaumiwa ni wananchi wenyewe. Kwani daladala ikija na watu wakajipanga vema ktk mstari bila kugombea tatizo liko wapi? Hakuna haja ya polisi ama serikali kuingilia hili, hapa ustaarabu miongoni mwa wananchi wenyewe unatakiwa. Sio kugombea daladala tu bali hata uendeshaji wetu wa magari barabarani ni hovyooo kabisa. Kila mtu anataka kuwahi atokeo yake ni kuchomekeana na kuongeza foleni zisizo na msingi. Hata zikijengwa beltways kumi Dar, kama ustarabu wa kuendesha hakuna basi foleni hazitaisha hadi Jesus atakaporudi.
Third world ni third world tu hata iweje!
 
haya mie nina mawazo mgando, wewe mwenye MAWAZO MYEYUKO BIN MMIMINIKO endelea kuhamasisha watu............. Kama unadhani bila kuwapo kwa sheria na kanuni na usimamiaji inawezekana, bila kuwa na uboreshaji wa usafiri wa uma bado inawezekana...... Mfano Kwani hao mateja abiria na makonda hawakuwa wakikemea kutowapa hela? Wamefanikiwa na kuhamasishana kwao?
Acha nikapige tizi nijiandae kupitia dirishani kesho


Sifikiri kama kila jambo tunasubiri serikali kuchukua hatua, kuna mambo tunaweza kuhamasishana na kuchukua hatua. Jambo la msingi ni kila mmoja wetu kumuona mweziwe ni bora kuliko yeye, kama kuwahi nyumbani basi mpe kipaumbele mwingine, swala sio kuwa na msuli; hata wewe huo msuli unaoringia leo kuna siku utakuwa huwezi. Watu wengine wana matatizo ya kiafya, kunakuwa na watoto, kuna kuwa na wamama wajawazito, kuna kuwa na wazee; hivi makundi yote haya wataweza kugombania usafiri. Halafu tuache hii tabia ya kusema kila jambo haliwezekani bongo, sasa tunaweza nini; HAYO NI MAWAZO MGANDO.
 
hili la kukombania daladala, kuwahi katika foleni za benki (kisa unamjua cashier), etc..

Ni mambo ya kijinga na ubinafsi ambao hauhitaji serikali ni mtu binafsi asijione bora zaidi kupita wengine..
 
kwanza usafiri wa daladala uboreshwe,
daladala ziwe nyingi za kutosha
miundo mbinu ya barabara za mijini iboreshwe kupunguza foleni ibuniwe kusudi daladala ziende na kurudi fasta,

huko kwenye utaratibu wa foleni, usafiri wao wa umma wameuboresha pamoja na miundo mbinu ya barabara za mijini.

upo kkoo/posta wakati wa jioni, inakuja daladala moja kituoni na unakuta kuna abiria zaidi ya 500, hapo hiyo foleni itapangwa vipi kama sio vurugu??? ndicho kinachotokea hapa dar ama daladala chache au foleni zilizokithiri zinafanya daladala zichelewe kwenda na kugeuza fasta, hujiulizi mbona mikoani hakuna huko kupanga foleni na watu hawagombanii kwa fujo kupanda daladala?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom