Kugombania daladala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kugombania daladala

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by HAKUNA, Mar 22, 2012.

 1. H

  HAKUNA Senior Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Imekuwa ni tabia ya kawaida kwa watu kugombania kupanda daladala na sijawahi kusikia Serikali au Taasisi yeyote ile kuliwekea utaratibu na msimamo jambo hili. Watu wamekuwa wakiibiwa, kuumizwa na vitendo vinginevyo ambavyo wanadamu asingependa kutendewa.

  Najiuliza, Hivi haiwezekani kuweka foleni wakati wa kusubiri basi na tukaingia kwa utaratibu mzuri, basi likijaa tunasubiri. Tunahitaji kujifunza kanuni ya FIFO - First In, Firts Out. Nafikri mambo mengine inabidi tubadilike tu, sio tunaishi kama wanyama, hatuna utaratibu.

  Unafikiri nini kifanyike ili kuleta utamaduni wa kupanga foleni?

  daladala.jpg View attachment 49915
   
 2. C

  Cape city Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watanzania ustaarabu hatuna na sijui ni lini watu watabadilika. Mbona nchi za wenzetu watu wanaweza kupanga foleni? Hapa Johanesburg SA watu wanapanda daladala kwa foleni na zaidi ya yote, hakuna konda...na watu wanakusanya pesa wenyewe na kumpa dereva....
  Ah..naichukia sana Dar linapofikia jambo hilo la usafiri wa daladala!!!
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  You stole my thunder! I was about to say the same thing.
   
 4. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  ndio kwanza kova na team yake wanakaa kwenye vyombo vya habari kuzungumzia eti wamefanikiwa kukamata machangudoa kadhaa wakati mateja yamejaa vituoni kuibia abiria
   
 5. H

  HAKUNA Senior Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hili nalo ni moja kati ya majanga ya kitaifa, sehemu nyingi ambazo watu mnasubiri huduma ya aina moja, kila mmoja anataka kuwahi na hii inatokana na kwamba watanzania hatujali maisha ya mwingine kila mmoja anajali mambo yake; naweza kusema asilimia kumbwa ya watanzania ni MAFISADI.
   
 6. H

  HAKUNA Senior Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tena hawa polisi kuna genge wanaliendeleza ambalo baadae litakuwa na madhara makumbwa kwa jamii; vituo vya mabasi vimekuwa na wamiliki (vijana wala unga na wanachukua fedha kwa kila daladala), genge hili linawajibika kwa polisi kwa kupeleka hesabu kwa wakuu wa vituo. Genge hili lina baraka zote za polisi eti wanajita polisi jamii.
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,148
  Trophy Points: 280
  Mwanamke akiwezeshwa anaweza
  [​IMG]
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  ndugu wewe piga tizi tu upate msuli wa kugombea daladala, jifuhze kupitia madirishani na kupiga abiria wenzio vikumbo.......

  hayo mambo ya kupanga foleni tz ni ndoto....na wahusika wao wanatembelea ma-v8 foleni haziwahusu.......
   
 9. Invoice

  Invoice Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 15
  Aah! Kumbe ni hapa hapa dar! Nilidhani ni kwingineko. Mbona kwa dar ni jambo la kawaida ni sawa na kwenda bar akakuta wahudumu wote ni wakike.
   
 10. H

  HAKUNA Senior Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sifikiri kama kila jambo tunasubiri serikali kuchukua hatua, kuna mambo tunaweza kuhamasishana na kuchukua hatua. Jambo la msingi ni kila mmoja wetu kumuona mweziwe ni bora kuliko yeye, kama kuwahi nyumbani basi mpe kipaumbele mwingine, swala sio kuwa na msuli; hata wewe huo msuli unaoringia leo kuna siku utakuwa huwezi. Watu wengine wana matatizo ya kiafya, kunakuwa na watoto, kuna kuwa na wamama wajawazito, kuna kuwa na wazee; hivi makundi yote haya wataweza kugombania usafiri. Halafu tuache hii tabia ya kusema kila jambo haliwezekani bongo, sasa tunaweza nini; HAYO NI MAWAZO MGANDO.
   
 11. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,230
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  fifo? du watu mkishajifunza tu darasan mnataka yatumike haya inakuwaje hiyo?
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hii ni nchi ya watu wa hovyo kabisa, hakuna utaratibu wala ustaarabu labda mpaka aguswe mkubwa fulani sheria na taratibu ndio zitafuatwa. Pengine hata sisi wenyewe tunaolalama hapa kuhusu kugombea usafiri, ndio waharibifu wakubwa ktk engo nyingine, mathalan, kutapisha vyoo, kutupa taka hovyo, kumiliki grocery na kuzitumia kama nightclubs kiasi kwamba watoto wa shule, wagonjwa na watu wengine wanashindwa kulala kwa sababu ya makelele kisa tamaa ya pesa ya mpumbav mmoja, kukwapua maeneo ya wazi, kutokuwajibika ktk ofisi za umma tulizopewa dhamana mbalimbali etc etc. Wa kulaumiwa wa kwanza ni serikali yenyewe ya magamba, kuna low-costs solutions nyingi sana ktk kuendesha miji lakini ukiuliza lolote utaambiwa pesa hamna, au 'tupo kwene mchakato'..nchi ya ajabu sana hii, siku mkiskia nimepasua mtu kichwa na kummwaga ubongo msishangae.
   
 13. H

  HAKUNA Senior Member

  #13
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kweli safari bado ni ndefu, tuna tatizo zaidi ya watu wanavyofikiri; wengi wanafikiri nchi hii inakwamishwa na wana-siasa; sio kweli. Kama watu wanakuwa wanaona kila jambo ni la kawaida na inabidi tu liendelee kuwa hivyo itakuwa ngumu sana kupiga hatua, kwa mtazamo huu ndio maana hata viongozi wanatumia udhaifu huu na kutuburuza kwa sababu wanajua kila kitu tunaona ni kawaida. CCM kushinda ndio kawaida na inabidi iwe hivyo....kwa mtazamo wako.
   
 14. H

  HAKUNA Senior Member

  #14
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  sasa nini maana ya kujifunza?, unaona janga jingine la kitaifa; watu wanaenda shule kupata maarifa ambayo wanatakiwa ku-apply katika maisha, badala yake usanii unatumia zaidi. Ndio maana nchi yetu ina wasomi ambao wameshindwa kutatua matatizo. FIFO - Fisrt Inn, First Out; kwamba wa kwanza kufika kituoni ndio anapaswa kuwa wa kwanza kuingia kwenye daladala au sehemu yeyote ya huduma.
   
 15. H

  HAKUNA Senior Member

  #15
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Uko sahihi, ni kweli elimu inahitajika, lakini eneo zuri ambalo watoto wetu wanaweza kujifunza ni kutoka katika familia zetu, kama leo hii wewe na watoto wako mnaenda kituoni halafu mnaanza kugombania daladala nae atakuwa akifikiri hivyo ndivyo ambavyo wanadamu wanapaswa kuishi. Wazazi tunapaswa kuanza kubadilika ili tujenge msingi mzuri kwa kizazi kijacho.
   
 16. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Suluhisho
  1. Elimu- watoto wafundishwe civility, public conduct and public order mashuleni
  2. Madrassa- elimu hii iwe standardized ili kuepuka tabia za chuki, dharau, kutoheshimu watu wengine na mali zao kwa kigezo cha imani. Graduate wa elimu hii wana biased attitude towards other people na hawaoni ubaya wowote kumkanyaga, kumwibia au kumtia madole mtu tofauti nao
  3. Tabia za uswahilini- kuwepo na kampeni kupitia vyomujue bo vya habari, wasanii, wanasiasa na wanaharakati kuielimisha jamii ujue tabia hizo zimepitwa na wakati
  4. Viongozi - mabalozi madiwani nk wapewe semina juu ya ustaraab wa jamii
  5. Vyombo vya usafiri- kuwe na viwango vinavyokubalika ni salama na user friendly
  6. Self confidence ana image- mara nyingi waafrika hasa watanzania tuna tabia ya kujishusha na kudhani eti mambo mazuri ni ya wazungu, huu ulemavu wa fikira unachangia kwa kiasi kikubwa ubovu wa huduma kwa jamii
   
 17. H

  HAKUNA Senior Member

  #17
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mawazo mazuri....!!!
   
 18. JS

  JS JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Pia ubinafsi uliokithiri unachangia sana katika hili tatizo....ubinafsi ni kitu kibaya sana kwani mtu unajiona bora zaidi ya mwingine na ikija kwenye daladala regardless of your status in the society unaishia kugombania kuingia kwenye daladala kisa wataka kuwahi upate kiti eti as if wengine hawana haki ya kupata hivyo viti..inatia sana aibu kwa kweli....
   
 19. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kwakweli mi naona kudhani hili tatizo linaweza kuisha kwa kufundishana ustaarabu ni ndoto.
  Watu wataendelea kugombania mpaka pale mfumo mzima wa huu usafiri utakapobadilishwa.
  Hata hivyo Tanzania ilipo leo itatuchukua miaka mingi kwa usafiri wetu wa jumuia kuwa wa kiastaarabu kama ilivyo katika nchi za wenzanu zilizoendelea.
  Ili watu wasigombanie inabidi serikali iwekeze pesa nyingi sana(ambazo najua hazipo) katika kuleta mabasi makubwa na ya kutosha katika kila route,ikiwezekana hata treni zakutumika daladala pia ziletwe.
  Pia inabidi hii sekta isiendeshwe na watu binafsi bali yawe ni magari ya serikali yanayopita vituoni kulingana na ratiba maalum zilizopangwa vizuri.
  Mfano katika nchi zilizoendelea mabasi ya usafiri wa jumuia yanamilikiwa na serikali,pia yanapita katika vituo kila baada ya dakika 10 au 15 kwa mfano.
  Likikuta abiria mmoja linambeba linaondoka hata kama basi ni tupu,na litafika ktk vituo vyote mpaka kituo cha mwisho kwa muda ule uliotakiwa bila kujali lina abiria mmoja au limejaa.
  Dunia kwa sasa iko kwenye kampeni ya kushawishi watu kutumia usafiri wa jumuia hasa treni ili kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa lkn Tanzania yetu kila mtu akipata kamkopo anachukua kagari,jambo ambalo linazidisha kero hata kwa wenye magari binafsi kwa foleni ambazo sijawahi kuziona nchi nyingine yeyote zaidi ya Tanzania yangu,magari mengi wakati barabara ni zile zile za enzi ya ujamaa na kujitegemea.
  Hili tatizo si dogo kama tunavyolichukulia,na ninasikitika kusema halitaisha leo,na tukicheza hata vizazi vyetu vijavyo vitaishia kugombania daladala.
  Kwanza serikali ikisema ichukue huu mradi,inamaanisha kuhatarisha maslahi ya matajiri wengi ambao wanamiliki daladala,na hao wamiliki wa daladala wengi wao ndio hao hao wenye maamuzi huko serikalini,sasa unafikiri ikiletwa hoja ya serikali kuchukua hii sekta si lazima wataleta vikwazo kuhakikisha wanalinda maslahi yao.
  Tukija kwenye swala la eti tufundishane utamaduni wa ustaarabu wa kupanga foleni hiyo ni rahisi kusema kwa maneno lkn ktk hali halisi haiwezekani,chukulia mfano mim ni mama mpanda daladala,hii ni saa 12 jion sijamuona mwanangu mdogo tokea nilivyoondoka asubuhi saa 11,tena nimemuacha ana homa,halafu mnanambia nipange foleni wakati najua basi hili likiondoka lingine linalokuja itakua shida zaidi kuingia,hapo sitamuelewa mtu,nitagombania tu ili nikamuwahi mwanangu.
  Tukubalini tu kugombea daladala ni sehemu ya maisha ya mtanzania wa kipato cha chini,na tutaendelea kugombea hadi siku tutakapofanikiwa kupata rais asiye fisadi.
   
 20. H

  HAKUNA Senior Member

  #20
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuna mambo ambayo yanapaswa kuangaliwa kama ni majanga ya taifa na kuibua mijadala ya kitaifa, mojawapo ni hili la UBINAFSI, hili ndilo linalozaa UFISADI. UBINAFSI ukichukua mimba huzaa UFISADI; kama ambovyo biblia isemavyoa TAMAA IKICHUKUA MIMBA HUZAA DHAMBI, NA DHAMBI IKISHAKOMAA HUZAA MAUTI. Tunahitaji kuanza kuchukua hatua, kwa kuanza na discipline ya Queue katika sehemu ambazo wote tunahitaji huduma zetu; unaweza kuwa na ubavu wa kugombania daladala na ukawinnie, lakini kumbuka kuna siku utakwenda hospitali wakati unasubiri huduma na pale hazitakiwi nguvu kuingia kwa daktari (kwanza unakuwa huna nguvu hizo) mwingine atakuja kutumia nguvu ya pesa kuua haki yako ya wewe kupata huduma kwanza.
   
Loading...