Makame
JF-Expert Member
- Jan 3, 2008
- 512
- 60
USHURU WA SARUJI IAGIZWAYO KUTOKA NJE KWA SASA NI 25%; na VAt ni 18%.
ushuru umewekwa kwenye saruji ili kulinda uzalishaji wa viwanda vyetu vya ndani; kwani Saruji kutoka nje inaingia kwenye soko letu katika mazingiza ya ushindani usio halali. Nasema hivyo kwa sababu saruji izalishwayo nje na kuletwa kwenye soko letu inapata ruzuku huko itokako. Endapo Serikali itaruhusu saruji hio kuingia nchini bila ya kutozwa ushuru itakua na athari zifuatazo.
1. Uzalishaji wa ndani utadumaa na hatimaye kufa.
2. Ajira za ndani zitapotea.
3. Mapato ya serikali yatapotea (Both ya Ushuru na mapato ya ndani kutoka kwenye uzalishaji wa ndani).
4. Uzalishaji wa ndani ukifa; saruji iagizwayo kutoka nje itapandishwa bei; kwa kuwa itakuwa ishaua uzalishaji wa ndani; hivyo watakuwa na ukiritimba.
KIMSINGI KUFUTA USHURU HAKUWEZI KUSHUSHA BEI YA SARUJI; bali kutaangamiza uzalishaji wa ndani, ajira, mapato na hatimaye kujengea mabepari wanaoagiza saruji kutoka nje MONOPOLY.
AIDHA
kufuta ushuru wa saruji ni kuenda kinyume na utekelezaji wa Itifaki ya Umoja wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; hivyo kimsingi maanake ni kuelekea kujitoa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Sasa kusema kuwa unafuta ushuru kwenye saruji ni kujitoa kwenye Jumuiya; ambapo VYAMA VYOTE VINASEMA KWENYE ILANI ZAO KUWA WANAUNGA MKONO MTANGAMANO WA AFRIKA MASHARIKI.
SASA DKT SLAA ALIKUWA ANAWADANGANYA WATANZANIA AU ALIKUWA HAJUI ANACHOKISEMA?