Net group solution, Deep Green, Meremeta, RITES, Richmond, Buzwagi, Ushirika wa Celtel na TTCL, na ubinafsishaji wa viwanda vya ngozi, nguo, mahoteli ya serikali, uuzaji wa nyumba za serikali zilikuwa na utafiti wa kina?
Kwa heshima na taadhima kubwa.
1. Hapa tunazungumzia SARUJI na Kuhusu ushuru wa Saruji kufutwa kwenye bidhaa hio.
2. Suala la TTCL, TRC, ATC, TICTS, TBL, TDL, NBC and what ever case you may know of; ni out of the THREAD. Ukitaka kuyazungumzia hayo, anzisha thread nyengine; tusitoke nje ya mada. Aidha, kila moja ya hizo ni different case scenario na kuna maelezo yake.
3.Mtu anapofanya maamuzi huwa hafanyi kwa kufanya OVERVIEW ANALYSIS ya mambo, kinachotakiwa ni INDEPTH ANALYSIS. Sasa kama kuna safari ndefu, ni kweli; hilo silikatai. Na Inapaswa ianze kwa watu wenye kubwabwaja kuthamini ANALYSIS, ambazo zinapelekea waamuzi kufanya maamuzi yalikuwa informed.
4. Mimi wala sijajiaibisha, kwani I have made my case; you want to encounter that; go ahead; ila iwe kwa HOJA. USIKURUPUKE TU; au ndio unafanya mambo KIJESHI JESHI [IDDI AMIN] kwa hiyo Uniform kwenye profile?
USHURU WA SARUJI IAGIZWAYO KUTOKA NJE KWA SASA NI 25%; na VAt ni 18%.
ushuru umewekwa kwenye saruji ili kulinda uzalishaji wa viwanda vyetu vya ndani; kwani Saruji kutoka nje inaingia kwenye soko letu katika mazingiza ya ushindani usio halali. Nasema hivyo kwa sababu saruji izalishwayo nje na kuletwa kwenye soko letu inapata ruzuku huko itokako. Endapo Serikali itaruhusu saruji hio kuingia nchini bila ya kutozwa ushuru itakua na athari zifuatazo.
1. Uzalishaji wa ndani utadumaa na hatimaye kufa.
2. Ajira za ndani zitapotea.
3. Mapato ya serikali yatapotea (Both ya Ushuru na mapato ya ndani kutoka kwenye uzalishaji wa ndani).
4. Uzalishaji wa ndani ukifa; saruji iagizwayo kutoka nje itapandishwa bei; kwa kuwa itakuwa ishaua uzalishaji wa ndani; hivyo watakuwa na ukiritimba.
KIMSINGI KUFUTA USHURU HAKUWEZI KUSHUSHA BEI YA SARUJI; bali kutaangamiza uzalishaji wa ndani, ajira, mapato na hatimaye kujengea mabepari wanaoagiza saruji kutoka nje MONOPOLY.
AIDHA
kufuta ushuru wa saruji ni kuenda kinyume na utekelezaji wa Itifaki ya Umoja wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; hivyo kimsingi maanake ni kuelekea kujitoa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.