Kufuru: Kikwete alitumia takribani Milioni 4 kwa siku moja hotelini Serengeti

hotel za Serengeti zipo za USD 1200 kwa siku hivyo hata mtu wa kawaida ukiamua kwenda kupumzika huko lazima ujiandae kwa 5m na kuendelea iwapo utalala hotel za aina hiyo. swala la kushangaa hizo garama ni swala la ushamba tu wa mtu kutojua garama za hotel za serengeti. kwa wale waliyowahi kuja huku hawawezi kushangaa hata kidogo labda kama kuna uthibitisho kuwa hela iliyotumika ilikuwa ya ikulu na kwamba haikuwa halali kwa mtu huyo kutumia.inawezekana pia mtu huyo alienda kikazi na mwenye kustahili kulala hotel kama hiyo au pia mtu wa usalama ambaye alikuwa hapo kikazi.
 
Mode kwanza rekebisha heading, heading inamtaja JK, contents zinamtaja ofisa wa Ikulu!.

Kila zama na zama zake!, zama za JK zimepita, mwacheni JK apumzike kwa amani, ajilie pensheni yake kwa utulivu!, sasa ni zama za Magufuli!.

Hata Mwalimu alipompisha Mwinyi, alipageuza Ikulu kuwa ni pango la walanguzi!. Mkapa alipoingia hakumsumbua wala kumsakama Mwinyi!. Hata JK alipotinga ikulu, alikuta tuhuma za Ben kufanya biashara Ikulu, JK akatusisitiza tumuache Mkapa astaafu kwa amani!.

Watanzania ni watu wa kulalamika sana bila kuchukua hatua zozote!. Huu sasa sio wakati wa kulalamika tena, huu sasa ni wakati wa kuchapa tuu kazi!.

Pasco

Sasa hiyo tabia ya kunyamaza eti kwa kuwa kila zama na zama zake ndio yanayoharibu nchi. Mabaya na ya hovyo kwa vile wanakinga ya kushtakiwa basi walao yakemewe sana na waaibishwe kwa maovu hayo ili kuwafanya wanaowaachia madaraka basi waone aibu kuyafanya na wao.
Tunaona nchi za wenzetu walio endelea hayo mambo ya kinga hakuna na kule ambako yapo ni wakati mtu akiwa madarakani tuu. Waweza kukuta leo hii mtu anashtakiwa kwa tuhuma za mambo yaliyogundulika kutendwa miaka ya 1980 na kesi inanguruma.
Lazima tuseme, nani anajua hatima ya JPM huko mbeleni? Maana naye ni binadamu tuu, na historia inasema wazi kuwa wale walioingia madarakani na KUSIFIWA SANA huwa na kawaida ya kuishia vibaya sana. Mungu aepushie mbali hilo kwetu na kiongozi wetu afanye yaliyo mema kwa nchi.
Lakini pia Pasco, hivi watu wakubwa kama Kamishna jenerali wa TRA, GM wa Bandari, mzee mzima wa PCCB na wengine wengi wataofata tunawawajibisha kwa uzembe au tuhuma nyingine nyingi lakini yule ambaye walikuwa wanajikuta wakati mwingi wanawajibika kwake naye anatoa maagizo kwao yaliyoleta tuhuma hizo hafanywi chochote kwa vile anakinga ni sawa hiyo? Basi hata kinga ya kusemwa kama hana asisemwe eti aachwe apumzike? Hakuna bwana acheni asemwe naye walao ajisikie kauchungu kidogo! Amekuwa Mungu ambaye hakosolewi?
 
Last edited by a moderator:
hivi kwa nn mnaletaga topic za hilo jitu mmeshaharibu siku yangu km kuna mtu namchukia mungu anisamehe ni huyo mliyemtaja sina hata haja kuandika jina lake

ulivyomzuri hivyo ngoja akujie na kiswahili cha msoga " sichomoi sijakuchomeka"
 
Katika Gazeti la MwanaHalisi la leo kuna taarifa yenye kichwa cha habari KIKWETE KUFURU, kwamba wakati wa utawala wa JK kulikuwa na tabia ya kufuja pesa za walipa kodi kwa njia za FEDHEHA.

Katika moja ya safari chache za ndani ya Nchi mapema mwaka huu, ofisa mmoja wa Ikulu aliyekuwa kwenye msafara wa Rais alitumia pesa Tshs 821,997.24 kwa MASAJI peke yake (kukandwa na kutomaswa mwili) akiwa katika hotel ya kifahari iliyopo ndani ya mbuga ya Serengeti ya FOUR SEASONS SAFARI LODGE. Kiasi hicho cha pesa kililipwa na Ikulu.

Ofisa huyo wa Ikulu alifika Arusha akiwa katika msafara wa JK na kwenda moja kwa moja kwenye Hoteli hiyo kwa usiku mmoja na alikuwa katika chumba no 9017 na kwa ujumla kwa usiku huo mmoja gharama zote zilikuwa Tshs 3,862,997.24 zikiwa ni gharama za Masaji, Kufua Nguo, Kula, Kunywa na Kulala kwa usiku mmoja huo wa April 17.

Gharama za ufuaji wa nguo za ofisa huyo wa Ikulu pamoja na mwanamke aliyekuwa nae kwa siku hiyo jumla ni Tshs 676,000/=.
Gharama zote tajwa hapo juu zimelipwa na Ikulu.

Chanzi: MwanaHalisi la leo, Toleo 318.

My Take:
Awamu ya nne haikuwa na chembe ya huruma kwa wananchi wake.

Kiwete na washikaji wake walikuwa wasanii na mafuska wasio na haibu wala faida kwa taifa. Inabidi Mwakyembe apitishe sheria ya kunyonga marais wote waliopita na mawaziri wao kisha kuwataifisha mali.
 
nimeona hii habari kwenye gazeti la mwanahalisi

nape hembu fatilia kama hakuna ukweli chikua hatua!
 
Kweli unachukulia kawaida matumizi ya shilingi 4000000 kwa usiku mmoja?pesa za walipakodi maskini ambao hawajui kuwa watakunywanini asubuhi,watakula nini mchana na jioni?alafu wengine waseme kuwa nipesa ya kawaida?kuna kila sababu ya kuwepo kwa hospitali nyingi aina ya mirembe kwa kila kijiji.
 
kwa matumizi ya rais na ujumbe wake hiyo mbona hela ndogo sana...kwa aina hiyo ya hotel..Mimi na familia yangu msimu huu wa sikuku tunalala hotel moja pale Bagamoyo kwa gharama za mara mbili ya hiyo
Wewe unalala pamoja na familia nzima, mwenzako peke yake tu anatomaswa
 
mbona kichwa cha habari na habari husika havifanani? au ulikuwa na nia gani wewe mngese?

kwa matumizi ya rais na ujumbe wake hiyo mbona hela ndogo sana...kwa aina hiyo ya hotel..Mimi na familia yangu msimu huu wa sikuku tunalala hotel moja pale Bagamoyo kwa gharama za mara mbili ya hiyo

alie tumia hizo hela ni JK au afisa wa Ikulu? Mbona hueleweki.

Katika Gazeti la MwanaHalisi la leo kuna taarifa yenye kichwa cha habari KIKWETE KUFURU, kwamba wakati wa utawala wa JK kulikuwa na tabia ya kufuja pesa za walipa kodi kwa njia za FEDHEHA.

Katika moja ya safari chache za ndani ya Nchi mapema mwaka huu, ofisa mmoja wa Ikulu aliyekuwa kwenye msafara wa Rais alitumia pesa Tshs 821,997.24 kwa MASAJI peke yake (kukandwa na kutomaswa mwili) akiwa katika hotel ya kifahari iliyopo ndani ya mbuga ya Serengeti ya FOUR SEASONS SAFARI LODGE. Kiasi hicho cha pesa kililipwa na Ikulu.

Ofisa huyo wa Ikulu alifika Arusha akiwa katika msafara wa JK na kwenda moja kwa moja kwenye Hoteli hiyo kwa usiku mmoja na alikuwa katika chumba no 9017 na kwa ujumla kwa usiku huo mmoja gharama zote zilikuwa Tshs 3,862,997.24 zikiwa ni gharama za Masaji, Kufua Nguo, Kula, Kunywa na Kulala kwa usiku mmoja huo wa April 17.

Gharama za ufuaji wa nguo za ofisa huyo wa Ikulu pamoja na mwanamke aliyekuwa nae kwa siku hiyo jumla ni Tshs 676,000/=.
Gharama zote tajwa hapo juu zimelipwa na Ikulu.

Chanzi: MwanaHalisi la leo, Toleo 318.

My Take:
Awamu ya nne haikuwa na chembe ya huruma kwa wananchi wake.
 
Mbona pesa ya kawaida tu,ingekuwa kila siku sawa.Kenyata shushaini viatu dola mia mbili.raisi raisi tu hawezi kuwa kama wewe.Sasa nenda kwa Zuma ndio utachoka.Kubenea si Mbunge onyesha njia punguza posho ya 300000 na mshahara wa 1300000.
 
Akili za vitungu Swaum Hata Miami, Floorida Gharama Haziwezi kufikia Hapo Massages na Sauna kwenye Hotel ya 7 Stars na Hata Mkiwa Watu 50 Ukisikia Uandishi KIAZI Ndio huu Majungu ndio Mtaji Mliobakia nao
 
Khaa!! Kama Kubenea atapinga posho za kufuru za wabunge nitamkubali bila ya hivyo nitaendelea kumuona kahaba tu wa kisiasa kama makahaba wengine :cool:
 
Kikwete ni sadist.How can we just sit and lough at him wakati amesababisha shida mbalimbali na vifo vya maelfu vya watanzania wenzetu.Hapana,ni lazima yeye na na makuadi wenzie wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.Rais Magufuli tunaomba utusaidie katika hili.
Katika Gazeti la MwanaHalisi la leo kuna taarifa yenye kichwa cha habari KIKWETE KUFURU, kwamba wakati wa utawala wa JK kulikuwa na tabia ya kufuja pesa za walipa kodi kwa njia za FEDHEHA.

Katika moja ya safari chache za ndani ya Nchi mapema mwaka huu, ofisa mmoja wa Ikulu aliyekuwa kwenye msafara wa Rais alitumia pesa Tshs 821,997.24 kwa MASAJI peke yake (kukandwa na kutomaswa mwili) akiwa katika hotel ya kifahari iliyopo ndani ya mbuga ya Serengeti ya FOUR SEASONS SAFARI LODGE. Kiasi hicho cha pesa kililipwa na Ikulu.

Ofisa huyo wa Ikulu alifika Arusha akiwa katika msafara wa JK na kwenda moja kwa moja kwenye Hoteli hiyo kwa usiku mmoja na alikuwa katika chumba no 9017 na kwa ujumla kwa usiku huo mmoja gharama zote zilikuwa Tshs 3,862,997.24 zikiwa ni gharama za Masaji, Kufua Nguo, Kula, Kunywa na Kulala kwa usiku mmoja huo wa April 17.

Gharama za ufuaji wa nguo za ofisa huyo wa Ikulu pamoja na mwanamke aliyekuwa nae kwa siku hiyo jumla ni Tshs 676,000/=.
Gharama zote tajwa hapo juu zimelipwa na Ikulu.

Chanzi: MwanaHalisi la leo, Toleo 318.

My Take:
Awamu ya nne haikuwa na chembe ya huruma kwa wananchi wake.
 
Sasa walitaka afisa wa Ikulu alale guest house!? Hayo mambo ya massage ni part of the package. Mtu unafanya kazi ngumu unapaswa ufanyiwe massage. Millioni 4 ni pesa ya kawaida tu.

Mbona wakati Lowassa anatumia million 200 kwenye harambee moja tu (pesa za wananchi alizopata kupitia ufisadi) mlimsema weeeeeh...ila leo mnamtetea!?

Kwa ufupi, Mwanahalisi na UKAWA kwa ujumla wenu ni wakupuuzwa tu.

kazi ngumu alikua analima mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom