MENGELENI KWETU
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 9,552
- 24,164
Katika Gazeti la MwanaHalisi la leo kuna taarifa yenye kichwa cha habari KIKWETE KUFURU, kwamba wakati wa utawala wa JK kulikuwa na tabia ya kufuja pesa za walipa kodi kwa njia za FEDHEHA.
Katika moja ya safari chache za ndani ya Nchi mapema mwaka huu, ofisa mmoja wa Ikulu aliyekuwa kwenye msafara wa Rais alitumia pesa Tshs 821,997.24 kwa MASAJI peke yake (kukandwa na kutomaswa mwili) akiwa katika hotel ya kifahari iliyopo ndani ya mbuga ya Serengeti ya FOUR SEASONS SAFARI LODGE. Kiasi hicho cha pesa kililipwa na Ikulu.
Ofisa huyo wa Ikulu alifika Arusha akiwa katika msafara wa JK na kwenda moja kwa moja kwenye Hoteli hiyo kwa usiku mmoja na alikuwa katika chumba no 9017 na kwa ujumla kwa usiku huo mmoja gharama zote zilikuwa Tshs 3,862,997.24 zikiwa ni gharama za Masaji, Kufua Nguo, Kula, Kunywa na Kulala kwa usiku mmoja huo wa April 17.
Gharama za ufuaji wa nguo za ofisa huyo wa Ikulu pamoja na mwanamke aliyekuwa nae kwa siku hiyo jumla ni Tshs 676,000/=.
Gharama zote tajwa hapo juu zimelipwa na Ikulu.
Chanzi: MwanaHalisi la leo, Toleo 318.
My Take:
Awamu ya nne haikuwa na chembe ya huruma kwa wananchi wake.