Kufungiwa mshahara

charles ogopa tapeli

Senior Member
Jul 15, 2013
122
49
Mimi ni mwalimu katika shule moja morogoro wilaya ya mvomero,
Nilifungiwa mshahara wangu tangu mwezi wa tisa.
Kosa langu lilikua ni kutofika kazini kwa siku 20, lakini walinisamehe kwa kunionya na adhabu yangu ikaisha mwezi wa 12 mwaka jana,
Tangu mwezi wa 12 mshahara wangu sijaupata na sasa hivi mshahara wa mwezi wa pili sijapata,.
Nimefuatilia halmashauri mara nyingi napewa majibu mepesi ambayo hayaendani na maswali yangu.
Ambao mnauelewa kuhusu hili naombeni msaada wangu ili niweze pokea pesa zangu za miezi miwili,.Kwa maana nipitie njia gani niweze pata hela yangu kiwepesi.
Natanguliza shukrani kwa wanajamvi wote mtakao guswa na kuweza nisaidia kimawazo kuhusu hili.
Karibuni wanajamvi.
 
Hujatuambia huko halmashauri ulimuona nani! afisa elimu,afisa utumishi, mkurugenzi? hao ndio wenye majibu sahihi na taarifa sahihi kwa nini mshahara wako hauwekwi kwenue akaunti yako.

Na vipi kuhusu mkuu wako wa shule umemshirikisha? na amekuelewa? ikibidi na kukusamehe? maana huyo ndiye aliyeandika barua ya kuku
onyesha wewe ni mtoro na hivyo usitishiwe mshahara!!

Ukishindwa hapo jaribu kumuona afisa elimu mkoa kabla ya kukimbilia Tamisemi; na wakati wote huo jitahidi tu kuwa mpole na majibu watakayokuwa wanakupa.

Pole sana mwalimu kwa changamoto unazopitia. Ukishinda haya majaribu yako basi utupe na mrejesho pia.
 
Sasa ndugu yangu mambo mengune sidhani kama huku JF utapata msaada, wewe ulifanya makosa inabidi uwe mpole ufuata unaweza ukashauliwa vibaya halafu ukajikuta unapata matatizo. Je bado upo ktk payroll na huo mshahara ulirudishwa hazina? Kama umerudi hazina usiende popote piga kazi, process za kurudi ni miezi kama si miaka
 
Chukua barua yako uliyosamehewa na kupewa onyo kutoka TSD, wafuate watu wawili tu Afisa utumishi anayehusika na Idara yako , na wa pili ni mtu anayehusika na LAWSON wapo hapo na hujificha ndio uhusika na kuscan hiyo barua na kutuma moja kwa moja utumishi , haipiti mwezi utapata mshahara wako. Achana na afisa Elimu au mkuu wa shule,hawahusiki kwa hili suala, wala usiwe mpole komaa nao, nilifanya hivyo na nilifanikiwa
 
Siku 20 ufiki kazini...unachangia kushuka kwa elimu Tanzanua...
Wewe ulitakiwa kutimuliwa tu iwe fundisho kwa wenzio
 
Chukua barua yako uliyosamehewa na kupewa onyo kutoka TSD, wafuate watu wawili tu Afisa utumishi anayehusika na Idara yako , na wa pili ni mtu anayehusika na LAWSON wapo hapo na hujificha ndio uhusika na kuscan hiyo barua na kutuma moja kwa moja utumishi , haipiti mwezi utapata mshahara wako. Achana na afisa Elimu au mkuu wa shule,hawahusiki kwa hili suala, wala usiwe mpole komaa nao, nilifanya hivyo na nilifanikiwa
Hawo LAWASON wanahusika na nini hasa maana sijawahi kuwasikia katika halmashauri zetu hizi
 
Back
Top Bottom