Kufungiwa Kanisa la Gwajima, Uhuru wa Kuabudu na Hatima Yetu

Kufungiwa Kanisa la Gwajima, Uhuru wa Kuabudu na Hatima Yetu

Vyamavingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Posts
5,980
Reaction score
5,797
Tafadhali mods naomba muuache uzi huu ili tuulizane na kupata majibu ya maswali yanayohusu hatima yetu.

Wadau wa JF na Watanzania wote. Ni juma la tatu sasa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Gwajima limefungwa na kusababisha Waumini kunyimwa haki yao ya Kikatiba juu ya uhuru wa kuabudu. Awali kulikuwa na mkanganyiko wa taarifa kuhusu kufungwa kwa Kanisa hilo. Taarifa za awali zinadai lilifungwa kufuatia madai kuwa kiongozi wa kanisa anahubiri siasa kanisani, uongo mkubwa! Gwajima hakugusia habari za itikadi wala sera za Chama chochote cha siasa bali kuonya, na kukumbusha wajibu wa watawala kulinda maisha ya watu dhidi ya utakeji, kutoweshwa na kuuwawa wakati serikali na watawala wakiangalia bila kukemea wala kuwasaka wanaofanya hayo kwa kutumia mgongo wa vyombo vya dola!

Ajabu ni kuwa Kanisa/Waumini wameadhibiwa kwa kunyimwa haki yao ya kuabudu, polisi kuwazuia waumini kukusanyika hata nje ya kanisa lao ili kufanya ibada.

Mbaya zaidi, katika 'kesi' hii serikali imekuwa mlalamikaji kwa upande mmoja na pia kujipa mamlaka ya kuhukumu; uko wapi utawala bora? Hii sio kuingilia majukumu ya Mahakama?

Ukimya wetu Watanzania, Waumini, Taasisi za kiraia, na Watetezi wa haki za binadamu ni kucheza na hatima yetu na haki za raia kuabudu, kukusanyika, na kutoa maoni. Kwa viongozi wa dini kukalia kimya hii hatua ya serikali kulifungia kanisa ni kuipa nguvu serikali kuchezea haki ya watu kuabudu; inashangaza sana Gwajima 'afanye kosa' halafu wahukumiwe waumini wa kanisa lake; kwa nini wasimshitaki mwenyewe? Haki iko wapi, mzazi afanye kosa halafu adhabu iende kwa watoto! Hiyo haipo popote.

Kwamba Gwajima yuko huru, hajakamatwa wala kutakiwa aripoti polisi kwa mahojiano ni ishara kuwa hakuna kosa lolote amefanya. Hata leo watawala na machawa wameshindwa kujibu hoja hata moja aliyotoa Gwajima zaidi ya kumbagaza yeye binafsi na Kanisa.

Viongozi wetu wa dini, nawakumbusha maneno ya majuto ya Padre Martin enzi za utawala wa Hitler karne ya 20. Fr. Martin alisema haya:
"Walikuja na kumchukua
mwanaharakati wa haki za wafanyakazi, nilikaa kimya kwa sababu sikuwa mwanachama wa chama cha wafanyakazi. Wakaja tena na kumchukua Myahudi, nilikaa kimya kwa kuwa mimi sio Myahudi. Mwisho wakaja na kunichukua mimi-hatimaye hakukuwa na mtu wa kunisemea".
Ukimya wenu viongozi wa dini, wanaharakati wa haki za binadamu, taasisi na asasi za kiraia ni hatari sana kwa mustakabali na ustawi wa taifa na utawala bora. Imani ya Watanzania kwenu itakapotoweka taifa litakuwa linazama, ikifikia mahali wataamua kushinikiza mabadiliko kwa kutumia nguvu ya umma mtakuwa mmechelewa na damu zao zitakuwa juu yenu.

Yanayotokea Kenya ni somo zuri, vijana wa Gen. Z wanajiendea-endea tu na maandamano barabari bila uongozi wala maelekezo, na matokeo yake ni vifo, uharibifu na upotevu wa mali, wanachotaka hakieleweki, hata watawala hawajui waongee na nani. Ole wetu!

Vv
 

Attachments

  • VID-20250630-WA0049(1).mp4
    6.6 MB
  • VID-20250630-WA0050.mp4
    14.3 MB
Janaribu ku-imagine kama haya wanayofangiwa wafuasi wa Gwajima ingelikuwa wanafanyiwa waislam wa dhehebu lolote lile. Tungesikia hadi Afghanistan wanaandamana kuilaani Serikali ya Tanzania
 
Niongee tena kama mkristo kuhusu hili sakata linalomhusu Gwajima na kanisa lake. Iko hivi, kuna mambo mengi ya ajabu yanaendelea katika dini ya kikristo na madhehebu yake. Kuna wahubiri wengi wa ajabu mno baadhi ni wa kutoka nje kama yule jamaa "kiboko ya wachawi" tuliyemfukuza juzi na wengi zaidi ni wazawa kama akina Mwamposya n.k. Kwa muda mrefu sana na kwa kuheshimu kwamba binadamu hana uwezo wa kuamua ipi ni dini ya kweli na ipi ni practice sahihi ya dini serikali na sisi watu binafsi tumekuwa tukifumbia macho taasisi hizi za dini na kuacha raia watumie utashi wao na akili.l zao kadri wanavyoona inafaa. Mtu kuanzisha au kuchagua dini au dhehebu lipi la kusali vibaki kama mtu anavyoamua mke au mme wa kufunga nae ndoa. Chungu na raha za dini na madhehebu yao na wachungaji wao watajijua waumini wenyewe.

Ila pale ambako dini au wenye dini wenyewe watavuka mipaka na kuanza kuingilia "anga' zingine, kwa aidha kujisahau kuwa umaarufu wao kwa waumini wao haumaanishi kwamba vitu vyao vinakubalika kwengineko na kuanza kujifanya "majasusi wa mbinguni" kwenye himaya za wengine, au iwapo wenye dini wenyewe watafanya vitu vinavyotafsirika kama uhalifu kwenye tafsiri za kiserikali, kama huyu nabii hapa mtaani kwangu anayepiga ramli chonganishi kwa kisingizio kuwa anawatabiria watu, mmh hapo sasa ni kuiamsha mizimu ya waliolala.

Gwajima anajua nini anachokifanya na anajua nini anapaswa kufanya hili kanisa lake lifunguliwe.
 
Back
Top Bottom