Kufungiwa google adsense (disable/deactivate )na malipo kwa cheki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufungiwa google adsense (disable/deactivate )na malipo kwa cheki

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Apr 20, 2011.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Taarifa hii ina wahusu wale wenye blogu au tovuti ambazo zinatangaza bidhaa mbalimbali kutumia google adsense kwenye kurasa zao mbalimbali ambao kwa bahati mbaya Akaunti zao zimefungiwa na Google ( Deactivate ) kutokana na sababu kadhaa .
  Sababu za Kufungiwa
  1 – Labda waliclick ( gonga ) matangazao wenyewe wakati hawatakiwi kufanya hivyo .
  2 – Labda waliomba watu wao waclick ( gongo ) matangazo ya adsense hii nayo haitakiwi .
  3 – Walitumia programu maalumu kudanganya Mtandao wa Google kuhusu idadi ya watu wanaotembelea na kugonga matangazo hayo .
  4 – Walibadilisha Code za Adsense walizopewa na Google au walificha Matangazo ya Adsense ili kulaghai watembeleaji .
  5 – Kufanya udanganyifu wa aina yoyote dhidi ya Google bidhaa zake na Watangazaji wa Bidhaa kutumia Adsense .
  6 – Walijiunga na Huduma zingine za Matangazo zinazolipwa kwa Kugonga ( Ppc ) Pay Per Click na kuweka huduma hizo kwenye kurasa zilizokuwa na Adsense .
  7 – Ameweka maandishi au chochote ambacho si chake kwenye kurasa bila kuweka Chanzo au Nukuu na Maelezo ya ziada .
  UKIFUNGIWA AKAUNTI YAKO YA ADSENSE CHA KUFANYA ( Deactivate )
  1 – Unatakiwa uchunguze yote hayo juu niliyoyataja kama kweli ulifanya au ulijihusisha nayo soma maelezo ya Adsense vizuri na Sheria zake Upya .
  2 – Kama uliingiza Huduma zingine za Matangazo kama ClickBank au Chitika kwenye kurasa zako tafadhali soma maelezo vizuri kama zinaendana na Masharti ya Adsense .
  3 – Tembelea appeal form. ili uweze kufanya maombi upya na kuwapa Adsense Taarifa zaidi kuhusu Blogu na Tovuti yako na Uombe msamaha .
  4 – Kukusamehe na kurudisha Akaunti yako ya Adsense si lazima unaweza kufungiwa moja kwa moja kuanzia hapo mara nyingi tunaomba misamaha na kukata rufaa mara 2 tu .
  UKIFUNGIWA ADSENSE – SUALA LA MALIPO YA CHEKI YAKO
  Kama ulifungiwa Akaunti yako mwezi wa 5 Mwishoni utapata Cheki yako ya mwezi wa 4 kama mapato yake yalizidi dola 100 au Euro 70 lakini cheki hiyo haitoweza kulipwa na Google Adsense hela zote zitarudishwa kwa wale watangazaji wako .
  Ukipokea CHEKI YA GOOGLE ADSENSE wakati Akaunti yako imeshafungiwa Usiingize kwenye Akaunti yako ya Benki kwa sababu haitolipwa na itaonekana CHEKI Hiyo ni Batili ( FORGED ) Unaweza kupata matatizo na benki yako .
  Hata hivyo benki yako itakukata pesa na Gharama nyingine za Cheki hiyo kama uliingiza kwenye Benki yako .
  KWA WAFANYAKAZI WA BENKI NCHINI TANZANIA
  Tafadhalini kama mumepokea CHEKI za Google Adsense kwanza thibitisheni toka kwa mleta CHEKI kama Akaunti yake iko ACTIVE ndio muanze kufanya Taratibu zingine za Malipo , msipofanya hivyo mtaweza kupata hasara na kuijiingiza kwenye matatizo na mengine ya kuchafua benki zenu na huduma zenu wenyewe .
  Najua hii ni huduma mpya na Wengi hawana taarifa za kutosha kuhusu biashara za mitandao na malipo yake kwa ujumla haswa yanayohusiana na cheki .

  YONA F MARO
  0786 806028
  DAR ES SALAAM
   
 2. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  poa mkuu binafs nimekusoma vizuri.pia naomba uendelee kutupatia maelimu zaidi ya blog.
   
 3. khaliciouz

  khaliciouz JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2015
  Joined: Nov 12, 2013
  Messages: 656
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 60
  ahh kwa wale wanaotaka adsense aacc na template za kusaidia uweze kupost kiswahili au kuanzisha blog na website ili uweze kutengeneza pesa hadi dola 300 nicheki 0713774746
   
 4. Sijuti

  Sijuti JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2017
  Joined: Oct 20, 2014
  Messages: 1,963
  Likes Received: 1,193
  Trophy Points: 280
  Nimeikurupusha maana inataarifa muhimu
   
Loading...