Kufungia Simu feki: TCRA msiwaumize wanyonge!

Sadoseba

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
243
91
WATUMIAJI wa simu wapatao milioni nane wapo
hatarini kufungiwa simu .Tanzania Daima limebaini.

Watanzania wazalendo hulipa kodi TRA wanapoingiza bidhaa nchini. Simu pia zikiwa imported hulipiwa ushuru.

Sijui TCRA wanakuwa wapi kuruhusu importation ya bidhaa feki & mwisho wa siku wanadai kuzifungia.
Itambulike kuwa Watanzania wengi hawawezi kugundua ikiwa simu in feki au la kwa kuiangalia kwa macho. Inampasa mtu kutuma IMEI TCRA ili kugundua software content ya simu husika, kwa sababu simu feki zina appearance na majina original.
Hivyo; kwa Mtanzania wa kawaida analazimika kununua simu KWANZA, kuweka lain na kuverify TCRA.
Hapa TCRA inamlindaje mteja? Inamlindaje mfanyabiashara?

Ikiwa kadirio la chini la gharama ya kila simu in 100,000 ; kwa simu 8,000,000 = 800,000,000,000#. This is misusage of resources!

MAPENDEKEZO:-

1. TCRA itengeneze sheria haraka kuruhusu KILA MWENYE SIMU FEKI airudishe kwa aliyemuuzia & abadilishiwe Bure (akiwa na receipt)

2.TCRA isubiri mizigo yote iliyomo nchini iishe, ili kuwanusuru wafanyabiashara waliokwisha kulipa kodi serikalini na bado wana mzigo.

3. TCRA iweke mkakati wa kuzuia importation ya simu feki. Iwakague wafanyabiashara wakubwa walaghai badala ya kuwafungia simu wananchi wanyonge wasio na uelewa
 
Mbona point namba 1 na point namba 2 zinapingana sana?
Yaani wananchi wenye simu feki wazirudishe madukani, na wafanyabiashara wenye simu feki wamalizie kuziuza kwa wananchi?
 
Suluhisho la kuondoa simu feki ni kumfungia tu mtumiaji ili wafanyabiashara waache kuleta nidhaa feki. Itaathiri watu wengi sana lakini mi naona ndio suluhisho.
 
Suluhisho ni hiyo namba 3! ingawa siungi mkono hilo zoezi lao kwa kuwatesa wanunuaji ilhali kosa ni la kwao na hao wauzaji wao. Kuna kauonevu flani hivi watafanyiwa wateja wa simu ambao hawana utaalam wowote wa kuigundua simu feki.
 
Suluhisho la kuondoa simu feki ni kumfungia tu mtumiaji ili wafanyabiashara waache kuleta nidhaa feki. Itaathiri watu wengi sana lakini mi naona ndio suluhisho.
Itakua ngumu maana watu 80% hawajui simu feki. Kikubwa ni ku deal na wafanya biashara. Kama ilivyo kwa wauza madawa ya kulevya
 
Wafanyabiashara wana mbinu nyingi za kuingiza bidhaa feki kama ambavyo wauza madawa walivyo. Madawa yanapigwa vita kila siku lakini bado yapo na yataendelea kuwepo milele.
Ili kuipunguzia serikali headache solution ni kuweka mitambo ya kuzuia simu feki zisifanye kazi na si kukimbizana na wafanyabiashara wenye mbinu nyingi.
Labda iombwe muda uongezwe mpaka mwezi wa 12. Bila maamuzi magumu kama hayo maendeleo kwenye nchi hii tutayasikia tu kwa wenzetu.
 
Kufunga simu feki sio maendeleo. Maendeleo ni kuwa na viwanda vya kuzalisha simu. Ni kuwaongezea mzigo wananchi wasioelewa chochote. Kwanini walisubili mpaka watu wazinunue. Si wangefunga kabla hazijanunuliwa
 
Sasa hivi zimeingia simu OriginalFeki kibao na hazifungiki....chezea bongo people weyeee TCRA mumekula wa chuya.
 
Kufunga simu feki sio maendeleo. Maendeleo ni kuwa na viwanda vya kuzalisha simu. Ni kuwaongezea mzigo wananchi wasioelewa chochote. Kwanini walisubili mpaka watu wazinunue. Si wangefunga kabla hazijanunuliwa
Maendeleo yapo ya aina nyingi. Kufungia simu feki ndio tunaelekea kwenye maendeleo kwasababu tutakuwa tunanunua simu bila kuwa na wasiwasi kama ni feki au la. Ni jukumu la wananchi (wewe ukiwemo) na serikali kuanzisha hivi viwanda. Hakuna mtu anayependa kununua bidhaa feki..zifungiwe tu kwa kweli hata kama nitakuwa mmoja wa wahanga.
 
sababu hasa ya kuzifungia hizo simu ni nini? Au wamefungua maduka ya simu original ili wapige hela? Kama ni athari, mbona sigara zina athari zaidi ya hizo simu lakini zina kibali.? Kwakua mpini wanao wao, acha wazime tu
 
Kwanini uuze simu feki? Kama wamefungua maduka ya simu original ndio hasa tanzania tu ataka. Ili mradi kodi ilipwe. Kwanini ununue simu feki ukae nayo muda mfupi wkt unaweza nunua original ukakaa nayo muda mrefu? Madhara ya simu feki yapo mengi.
Sigara na yenyewe ni jipu. Haimaanishi kwasababu imeruhusiwa basi na vingine feki viruhusiwe. Tunaenda pole pole kuondoa bidhaa feki nchini.
Issue ya sigara tuwaeleze wizara ya afya. Tcra na wizara ya mawasiliano wameamua yanayowahusu.
 
Kuzimwa lazima zizimwe. Ila wataumia watanzania wengi. Na bei za original zilivyo juu ndo itafahamika
 
Mkuu ungejiuliza simu feki anaeumia ni nani, Hizi simu feki zinaathari kubwa kwa mtumiaji, hutoa radiation ambazo nyingi kuzidi kiwango cha kawaida kwa mtumiaji, TCRA kuziondoa kwenye matumizi ni kuwasaidia watumiaji,
Nakushangaa eti mzigo uishe sokoni kwahyo watu waendelee kuumia? Hapa haujafikiria vizuri.
 
Nunueni org bana na hii kasi ya magufuli lazima wafungie tu kila mtu anataka sifa hivi sasa
 
Bado suluhisho la simu faki halijapatikana mm nna tecno feki Ukituma sms TCRA Ina jibu ila jina la Company tofauti syo Tecno means kwamba imesajiliwa kihuni
 
TCRA wazime tu matumizi ya simcard ktk simu feki.

ila waaziache ztumike upande wa radio, memory card, camera na vingne visivyotumia mtandao(joke!).
 
Ila mbna izi simu znauzwa madukanibkweupeee tofautibna madawa yanayouzwa kwa kificho.kwa nini tcra wasishirikiane na police kufanya ukaguzi kwenye maduka ya siku feki wazikamate ili wananchi wasiendelee kuumizwa.maana bado zipo madukani nyingi sana na znauzwa adi leo
 
Hilo nalo neno mkuu..
 
alafu cha kushangaza hizo simu feki zimelipiwa kodi na ushuru.
 
Back
Top Bottom