TCRA: Hatutawalipia fidia wenye simu feki

Bailly5

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
16,402
35,083
Geita. Wakati siku ya kuzimwa kwa simu feki ikikaribia,Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA),imesema haina mpango wa kuongeza siku za kuzima simu hizo wala haitahusika kulipa fidia kwa watakaoathirika baada ya simu zao kuzimwa.

Jana Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Vijana CUF(JUVICUF),Mahamoud Mahinda,aliitaka serikali kubeba mzigo wa kushindwa kuwajibika ipasavyo kwa kuruhusu uingizaji wa simu feki nchini.

Mahinda,alisema serikali ilishindwa kutimiza wajibu wa kuhakikisha simu hizo haziingizwi nchini,hivyo inapaswa kuwajibika,na kuwaacha wananchi kununua simu feki siku za nyuma bila ya kudhibiti uingizwaji wake nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi,mara baada ya semina ya kwa umma juu ya ufahamu wa mfumo wa rajisi wa namba za utambulishi wa simu za kiganjani mkoani Geita,Meneja wa TCRA nchini Innocent Mungy alisema mamlaka hiyo haina mpango wa kuwalipa fidia wenye simu feki. Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa TCRA James Kilaba,Mungy, alisema ifikapo Juni 16 simu hizo zitafungwa.

"Kipindi cha Mpito(Transition period) cha kuelimisha umma pamoja na zoezi la wateja kuhakiki simu walizo nazo au wakati wanataka kununua simu mpya lilianza mwezi disemba mwaka jana wakati huo mfumo ulipozinduliwa na itamalizika Juni 16"alisema Mungy.

Alisema,ikifika saa 6 usiku Juni 16,mwaka huu simu hizo zitafungwa,na wala TCRA haikusudii kuongeza muda wa kuzima simu hizo ,na mtu atayekaa na simu feki akikamatwa atachukuliwa hatua za kisheria.
1464098141044.jpg

Chanzo: Mwananchi
 
Hakuna ushauri bali tunasubiri wazime tu hizo simu feki, waharakishe ili sokoni tukute simu Original peke yake
 
Wakuu napenda kuwajulisha kuwa wale wenye simu feki muda si mrefu zitazuiwa kwenye mawasiliano, ila mjue hizi simu ambazo kwa asilimia kubwa zinaitwa feki zitazimwa endapo zilipita kwa njia ya panya ata kama ni original, kuna wafanyabiashara uwa wanaingiza bidhaa toka nnje bila kufuata utaratibu wa nchi, kama mtu aliingiza contena la tecno T580 na hakuzisijali kwa sasa tunaziita simu feki na tutazifungia kwa majibu wa sheria, lakini kama uliingiza simu ata kama ni second hand na zilipata kipali cha usajili kuuzwa nchini kwa kawaida tutaziita original na hazitafungiwa. Kwa maana hiyo hapa sio feki zinafungiwa bali zitafungiwa zilizoingia nchini kinyume na utaratibu. Sasa tujiulize kama tunaokoa jahazi ama tunazamisha jahazi
 
Back
Top Bottom