Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Siku chache zilizopita mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) wametangaza kuwa wamezima namba tambulishi (IMEI) 603,000 sawa na asilimia 2.9 ya vifaa vya mawasiliano ikiwa ni pamoja na simu feki zinazotumika nchini.
Kuzimwa kwa vifaa hivyo ni utekelezaji wa agizo la serikali la kuondoa bidhaa feki za mawasiliano kuanzia Juni 2016.
Ofisa Uhusiano wa TCRA, Innocent Mungy, alisema vifaa vya mawasiliano vilivyozimwa ni pamoja na simu za mkononi, ipad, tableti na modemu.
Katika hali inayothibitisha kuwepo kwa aidha hujuma au udhaifu wa kimtandao katika uzimaji wa simu feki, mtu mmoja ambaye mkoani Geita ameripotiwa kutiumia simu yake feki licha ya kwamba awali ilikuwa imezimwa.
Usiku wa uzimaji simu, alikuwa ameweka line ya tigo na voda na simu yake ilizimwa mpaka sasa haifanyi kazi kwa line zote isipokuwa kupitia line ya halotel.
Katika kusimamia maamuzi ya serikali kupitia TCRA, ni wakati wa kuchunguza zaidi kuhusiana na jambo hili kusudi taratibu zote zifuatwe na ikibidi simu zote zilizo feki zizimwe.