Hakuna asiyetaka watu walipe kodi kwani kazi ya kodi inafahamika. Lakini sayansi iko wapi kwenye kuutekeleza mpango huu wa kufunga vituo vya mafuta? Hakukuwa na udharura wowote kwenye jambo hili maana wafanyabiashara hao wa mafuta ndio waliokuwa wakichangia hela za kampeni za vyama vyetu kwa miaka mingi sana. Rais Kikwete aliweza kujenga barabara zote nchi nzima, aliweza kujenga UDOM, Hospitali ya Moyo, nyumba za askari, shule, viwanja vya ndege, uwandishi wa katiba, vitambulisho vya taifa nk kwa vyanzo vya mapato hivihivi, sasa kuna udharura gani kwenye kutoa risiti kiasi cha kusababisha foleni ndefu kwenye sheli kiasi hiki? Sayansi iko wapi hapa? Kwani wangepewa muda wa mwezi mmoja kutekeleza ingekuwaje?