Kufunga vituo vya mafuta ni dharau kwa wananchi

Kufunga vituo vya mafuta ni dharau kwa wananchi

Ww ni hufuatilii mambo ya msingi serikal walishatoa Maelezo tokea mwaka jana had tare 1/7/2017 kila kituo wafunge mashine hizo
leta kumbukumbu hayo mambo ya mwaka jana ndio ya muumize mwananchi asiye husika na migogoro ya serikali
 
Nchi imefitinika sana hii yaani tunateseka kwa ajili ya mijitu inajiita mawaziri
 
Wazir hana akili mzuri utawala wa chuki tu kwenda mbele tizama raia wanateseka na kupata HASARA wakipiga hatua moja mbele mnawarudisha hatua tano nyuma

Yaani siku yao inakuja..
 
Lengo zuri...lkn namna ya kulifanya lengo la kukusanya kodi ndo wakati mwingine linakosa utaratibu....hivi alternatives zote zimekosekana ?

Sent from my SM-J105F using JamiiForums mobile app
Puma amefanya biashara ya kufa MTU. Wakati mnapiga unyende mjuvi anaagiza mzigo wa mafuta tena kwa Bei elekezi.
 
Huwezi kutatua tatizo dogo kwa kutengeneza tatizo kubwa. Kwa kukosa mafuta vituoni na foleni ndefu kwenye vituo kuna matatizo yatakayojitokeza kama vile magari kuzima kwa kuishiwa mafuta, wagonjwa kuchelewa matibabu, uchumi kuyumba, nyumba kuungua moto nk wachilia mbali wafanyakazi kuchelewa kazini. Kwanini basi tusifunge vituo kwa awamu kama vile Wilaya, Mikoa au Kanda kama vile tulivyozima tv za analog
Kipi kianze kufungwa na kipi kiachwe? Mianya ya rushwa.
 
Wazir hana akili mzuri utawala wa chuki tu kwenda mbele tizama raia wanateseka na kupata HASARA wakipiga hatua moja mbele mnawarudisha hatua tano nyuma
Mmetuibia hela zetu sana.Kwenye mafuta tunalipa na kodi, nyie mnazikalia hela zetu.
 
Ukimzoea sana mbwa atakufuata hadi msikitini. Wenye vituo vya mafuta walikuwa hawalipi kodi hiyo ili kufidia hela walizoombwa kuchangia kampeni, sasa tunashituka nini? Ukiwachunguza wenye vituo hivyo wengi ni wanachama wa chama fulani cha siasa. Kiongozi mmoja aliwahi kuwaambia kama mnataka biashara zetu ziende vizuri changieni kampeni zetu
Magu aliwaambia" kama kuna mfanyabiashara aliyenichangia hata shs Moja asimame" Waende kwa waliowachangia.
 
Na wewe akili zako kama za wazir hiyo fine umeona au Vituo vinefungiwa? Wanateseka wananchi kwa hasara
Hasara IPI? Mafuta yapo puma total kwa Bei halali. Ni ujinga wenu kulanguliwa kwenye madumu
 
Leo wakwepa Kodi wanatetewa kwa nguvu zote. Vituo vya mafuta kutolipa Kodi sio dharau kwa Taifa? Wao kukuibia wewe unaona sawa ila wao kubanwa wasiibe sio sawa. Kuwaelewa wapinzani watanzania ni kazi sana, sasa naelewa kwanini madiwani wa Arusha wanaukimbia upinzani wwmechoka kupinga kila kitu hata chenye manufaa kwao
 
wale Wananchi ambao watapoteza wagonjwa wao kwa kuchelewa kupata matibabu kulikosababishwa na ama kutowahishwa hospitali au daktari kuchelewa kufika kazini kutokana na ukosefu wa mafuta hawatafikiria kiboya namna hiyo
 
Hospital zisizo na ubora, shule za chini ya viwango, miundombinu mibovu yote inachangiwa na wakwepa kodi tena wakubwa kama Hawa wamiliki wa vituo vya mafuta.

Hakuta taifa limeendelea bila kuwa na uthibiti wa ukusanyaji wa mapato.

Kwanini wao hawakufunga EFD mapema bila shuruti kama vituo vingine Kama total na GBP.

Sababu kazi ya upinzani ni kupinga kila kitu basi Leo mnapinga ukusanyaji mapato na kutetea wahujumu uchumi kama mlivyotetea acacia.
 
Ongea point kwahiyo kama walichangia kampeni ndiyo wafanyaje sasa waachwe tu na muda wa kufunga hizo mashine walipewa tokea mwaka Jana . dunia kote uchumi hutegemea zaid kodi kutokana na vyanzo mbali mbali ,tena nchi za ulaya ukikwepa kodi ni kosa kubwa sana na adhabu yake ni kubwa sana vile vile.

Walipe kodi tu huo
Aaah, angalau basi mngetoa taarifa kwa wananchi ambao ndio waathirika wakuu wa zoezi hilo ili wajiandae kwa hali kama hiyo. Hii ingeonyesha kuwa mnawajali na mnajali maumivu watakayoyapata katika kipindi hiki muhimu cha kutafuta kodi. Lakini wananchi walishitukia vituo vimefungwa bila kupatiwa utaratibu wowote, hizi ni dalili za kutojali wananchi
 
Magu aliwaambia" kama kuna mfanyabiashara aliyenichangia hata shs Moja asimame" Waende kwa waliowachangia.
Yeye alikuwa mgombea tu, kampeni zilifanywa na chama, chama kilikuwa na mwenyekiti, katibu, mweka hazina na wengine walioratibu shughuli, gharama za kampeni na vyanzo vya mapato, yeye angewajuaje waliokichangia chama kwenye kampeni zile?
 
Aaah, angalau basi mngetoa taarifa kwa wananchi ambao ndio waathirika wakuu wa zoezi hilo ili wajiandae kwa hali kama hiyo. Hii ingeonyesha kuwa mnawajali na mnajali maumivu watakayoyapata katika kipindi hiki muhimu cha kutafuta kodi. Lakini wananchi walishitukia vituo vimefungwa bila kupatiwa utaratibu wowote, hizi ni dalili za kutojali wananchi
Wananchi wanaathirika au ninyi wakwepa kodi ndio mmeathirika.? Weka mashine uuze mafuta.
 
7bcb63a5c01275cd915fe994d05521f5.jpg

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom