Kufunga mageti ya ofisi saa moja na nusu kwa miundombinu hii!

Dec 16, 2015
13
1
Wadau,

Nimeliangalia hili swala la waheshimiwa kufunga mageti ya ofisi saa moja na nusu wakati miundombinu yetu ni ya kutumia masaa manne kwa mwendo wa km 1! Kwa maoni yangu naona si sahihi kabisa!

Kikubwa si umefika ofisini saa ngapi bali kikubwa ni kuangalia mtu kafanya kazi masaaa mangapi kwa nchi za wenzetu ofisi za serikali zina attendance card mfanyakazi anapoingia kazini anaswap kadi yake na anapotoka vilevile so inakuwa rahisi kujua mtu kafanya kazi kwa masaa mangapi na mshahara unatoka kutokana na masaa aliyofanya kazi kwa mwezi!

Waheshimiwa jipangeni kwa technology za kisasa sio kuamka unafikilia kubeba mnyororo wa kwenda kufunga geti la ofisi kuna watu wanaamkia mahospitali kuna watu wanacheleweshwa na miundombinu yetu mibovu na sababu nyingine kibao kuwahi ofisini sio kufanya kazi swala ni kuboresha utaratibu na mtu afanye kazi kutokana na masaa ambayo anatakiwa kufanya kazi kama mkataba wake unavyomtaka.
 
Kama huwezi kuamka mapema kwenda job, endelea kulala. Kuna vijana wengi tu hawana kazi, wanaweza kujaza nafasi yako na si lazime wewe tu uendelee na kazi.
 
Du hii itatutesa tumezoea kupitia pale kinondoni kwa bonge kugonga ngumi asubui kabla hatujaingia na wakati huo foleni inapungua sasa itakuwaje .Bonge punguza kiasi jpm kashaharibu
 
Hawana jipya ni umbayuwayu tuu, haiwezekani kuwe na miundombinu ya hovyo, nyumba za watumishi wa seikali mmeuza ambazo ziko karibu na maofisi then leo hii muwatake wawahi maofisini,
hii si sawa kabisa
 
Ukiambiwa ndege itaondoka JNIA saa 12 asubuhi na reporting time saa 11 alfajili, unawahi na ukiambiwa basi litaondoka Ubungo Bus Terminal saa 12 asubuhi, unawahi kwa miundombinu hiyohiyo lakini kuwahi kazini saa moja na nusu miundombinu inakuwa mibovu.

Kama alivyo comment maso pa ngupi, namnukuu "Kama huwezi kuamka mapema kwenda job, endelea kulala.
Kuna vijana wengi tu hawana kazi, wanaweza kujaza nafasi yako na si lazime wewe tu uendelee na kazi" mwisho wa kunukuu.

Acheni kufanya kazi kwa mazoea, fanyeni kazi kwa kufuata taratibu za kazi zinavyosema. Ulipokubaliana na masharti ya ajira yako hukuhoji miundombinu, maana ulijua ukihoji tu, watamwita mwingine aliyeko kwenye waiting list.
 
Matukio uliyoyatolea mfano Ni tofauti kabisa..kusafiri Ni matukio au jambo linalotokea Mara chache lakini kwenda kazini Ni kila siku Na Kuna changamoto nyingi Tu za kibinadamu lazima tuziangalie..sawa mkuu Dr.Mwaaa..aah sorry
 
WaTz tumezidi mno kulalamika, mwaka huu tutaona mabadiliko ya kweli na lazima tubadilike maana hakuna jinsi
 
Back
Top Bottom