Kufundisha Kiswahili, Afrika Kusini

Kufundisha Kiswahili, Afrika Kusini

Ligogoma

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2010
Posts
3,502
Reaction score
6,460
Habari JF,

Leo nimegutuka baada ya Mkenya mmoja anafundisha shule ya watoto hapa Dar kumkuta anawasiliana kwa bidii na Mkenya mwenzie aliyepo Afrika Kusini (AK) kwa mchongo wa kwenda kufundisha lugha ya Kiswahili ambayo inasemekana imeshaingia kwenye mtaala wa nchi hiyo.

Mimi na yeye tuliongea machache tu ila aliniambia kwa sasa akipata senti zake (mshahara) anakwenda kujaribu bahati yake huko AK, keshapata njia ya kumfikisha huko na mchongo mzima ulivyo hivyo anataka kuwahi mapemaa.

Vipi kwa sisi Watanzania?? Hebu waTZ mliopo AK, mliopo kwenye mabalozi na mashirika mengineyo na tuliopo hapa kupitia nyuzi kama hizi tuanze kupeana hizo ramani za kufundisha Kiswahili huko. Nadhani pia iwe ni sehemu ya kupeana moyo ili tuondoe ile homa ya woga wa kuthubutu kwa Watanzania wengi.

Naamini katika hili la kufundisha Kiswahili Afrika Kusini, Watanzania tuna nafasi kubwa zaidi kuliko wengine wote ila kutothubutu kutatuacha nyuma tena.

Nawasilisha
 
Mkuu ubaya wa nchi ytu huwa hatupeani njia na opportunity ila hii issue ya kiswahili inalipa mno hata Rwanda hapo kuna wadau wapo wanapiga pesa
 
Watanzania wakusaidie zaidi ya kukukatisha tamaa...

Roho za Viongozi wetu ni Kama za Raia wao hakuna tofauti....

Mkuu we pambana utafanikiwa... Fanya application Kama mwehu ktk shule na vyuo mbalimbali... Utajibiwa watakuelekeza jinsi ya kufanya... Wala sio kosa kutuma application ktk email zao za office zinazo patikana ktk websites zao... Fanya hivyo...

Nakumbuka nilifanyaga hivi nchi za EU
 
Mkuu ubaya wa nchi ytu huwa hatupeani njia na opportunity ila hii issue ya kiswahili inalipa mno hata Rwanda hapo kuna wadau wapo wanapiga pesa

Uchoyo mwingi na hii ni ili ukirudi bongo upate zile sifa mtaa na ukoo kwamba huna wa kucompete nae kimafanikio!
 
Watanzania wakusaidie zaidi ya kukukatisha tamaa...

Roho za Viongozi wetu ni Kama za Raia wao hakuna tofauti....

Mkuu we pambana utafanikiwa... Fanya application Kama mwehu ktk shule na vyuo mbalimbali... Utajibiwa watakuelekeza jinsi ya kufanya... Wala sio kosa kutuma application ktk email zao za office zinazo patikana ktk websites zao... Fanya hivyo...

Nakumbuka nilifanyaga hivi nchi za EU

Mi sina shauku na ufundishaji mkuu, nilishaukataa kitambo.
 
Yap mkuu wanasahau watu wao ila kuna wengine wapo tofauti....chamsingi kuwa na connection na wazawa wa fani husika (walimu) nchi tofauti ili tuwe tunaulizia jinsi ya kupata nafasi

Connections ndiyo kila kitu mtu wangu. Tutatoboa hata kwa mbinde
 
Sana, shida yetu kuzubaa na kulalamika kwingi!! Sijui nani katuloga
Nadhani hata serikali nayo ingefanya mpango wa kuwaunganishia walimu wa kiswahili huko au hata kuhamasisha watu kuomba hizo nafasi ingerahisisha zaidi.
 
Nadhani hata serikali nayo ingefanya mpango wa kuwaunganishia walimu wa kiswahili huko au hata kuhamasisha watu kuomba hizo nafasi ingerahisisha zaidi.

Kuitegemea serikali?? Mtumishi tu wa kawaida kutoka nje ya nchi kwa mambo binafsi tu kimbembe itaweza kuhamasisha watu wakatafute ajira nje kweli??
 
Back
Top Bottom