Kufukuzwa kwa akina Mdee ni dili

Kufukuzwa kwa akina Mdee ni dili

NTIGAHELA

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
368
Reaction score
257
HABARI YA MBOWE KUMTAFUTIA KAZI MBADALA MDEE NI #KUWEWESEKA

Mmmh! Hizi #hekaya hizi hazina sababu, kwamba Halima amekataa kazi ya mshahara wa 15,000USD aliyotafutiwa na Mbowe kwasababu ya mshahara wa 5,000USD bungeni kweli but also inazua Maswali mengi Sana;

1. Kwanini Mh. Mwenyekiti ahangaike kutafuta kazi "Kubwa" Kwa ajili ya "Msaliti wa chama" ili aachie ubunge?

2. Mwenyekiti alikuwa na maslahi gani na Mdee pekee ilhali Wabunge wateule wapo 19?

3. Mwenyekiti alikuwa na sababu gani za kumbembeleza Mdee Kwa #kumuhonga kazi ilhali alikuwa ameshafukuzwa chama?

4. Hekaya hii ya mwenyekiti inayoendelea kusambazwa mitandaoni na wapambe wake inalenga kuarchieve nini hasa katika hatua hii?

5. Mwenyekiti anaamini kilichomuweka bungeni Mdee ni shida ya Kipato/ kazi?

6. Why Mdee, Mdee, Mdee ?

Mie nadhani ukweli ni kwamba Mwenyekiti anaweweseka na kujaribu kuonesha huzuni yake kutokana na kuondoshwa Kwa wanawake hao mahiri kutokana na ushabiki wa makundi ya ndani na nje ya chama kuushinda uhalisia mbowe anajua mchezo aloufanya kwa MDEE na wenzake ila anajaribu kuwapa matumaini ili nao wasimuanike hadharani kwa hiyo anacheza na akili za wajumbe kwa umakini huku akisubiria joto lipungue awarudishe kundini

Kimsingi si kazi rahisi na ni gharama kubwa ya Hali na Mali kugroom watu wa Kariba ya Mdee, Bulaya, Matiko etc. Mh. Mbowe akikumbuka safari hiyo inamuumiza kwasababu anaiona hasara yake kuliko washabiki wa mitandaoni.

Hii ni #bid_loss Kwa siasa za upinzani

mwanahapa
 
HABARI YA MBOWE KUMTAFUTIA KAZI MBADALA MDEE NI #KUWEWESEKA

Mmmh! Hizi #hekaya hizi hazina sababu, kwamba Halima amekataa kazi ya mshahara wa 15,000USD aliyotafutiwa na Mbowe kwasababu ya mshahara wa 5,000USD bungeni kweli but also inazua Maswali mengi Sana;

1. Kwanini Mh. Mwenyekiti ahangaike kutafuta kazi "Kubwa" Kwa ajili ya "Msaliti wa chama" ili aachie ubunge?

2. Mwenyekiti alikuwa na maslahi gani na Mdee pekee ilhali Wabunge wateule wapo 19?

3. Mwenyekiti alikuwa na sababu gani za kumbembeleza Mdee Kwa #kumuhonga kazi ilhali alikuwa ameshafukuzwa chama?

4. Hekaya hii ya mwenyekiti inayoendelea kusambazwa mitandaoni na wapambe wake inalenga kuarchieve nini hasa katika hatua hii?

5. Mwenyekiti anaamini kilichomuweka bungeni Mdee ni shida ya Kipato/ kazi?

6. Why Mdee, Mdee, Mdee ?

Mie nadhani ukweli ni kwamba Mwenyekiti anaweweseka na kujaribu kuonesha huzuni yake kutokana na kuondoshwa Kwa wanawake hao mahiri kutokana na ushabiki wa makundi ya ndani na nje ya chama kuushinda uhalisia.

Kimsingi si kazi rahisi na ni gharama kubwa ya Hali na Mali kugroom watu wa Kariba ya Mdee, Bulaya, Matiko etc. Mh. Mbowe akikumbuka safari hiyo inamuumiza kwasababu anaiona hasara yake kuliko washabiki wa mitandaoni.

Hii ni #bid_loss Kwa siasa za upinzani

mwanahapa
Kumuelewa Mbowe unapaswa uwe na akili njema.Laa Sivyo,utabaki na maswali yako hivyohivyo ya kitoto.(Calibre=kaliba)
 
Why Mdee? Hata Mimi sijui vya ndani. Ila huyo Halima Mdee ndo flagship ya hao 19. Je, ukimuondoa yeye, hao 18 wangeweza kusimama na kufanya kilichofanyika?
So, mwenyekiti alitummia akili za kawaida kabisa.... ukitaka kuondoa mchwa kwa kichuguu, piga malkia
 
Mleta uzi asome kwa umakini ulichoandika na aelewe.Nyoka hapigwi mkiani,kwa kuanzia.
 
Kuna mambo ya siri ya Chadema ambayo Halima Mdee anayafahamu akiyatoa Mwenyekiti Mbowe anaweza kuyumba! Ndio maana kulikuwa na hizo jitihada za kumtafutia kazi huko nje ya nchi!
 
Wanaosema hao akina mdee wangesamehewa hao hao ingetokea hivyo wangeanza kuinanga cdm kwamba wameshindwa kuwafukuza simply mchakato uliowaingiza bungeni ulikuwa na mkono wa Mbowe so acheni uamuzi uliofanywa na baraza ni wa kupongezwa sana na ulikuwa wa kidemokrasia sana na lazima watu wenye mapenzi mema na chadema lazima wauheshimu.Hao akina Mdee wamechagua fungu walilolipenda waache tuwaone kama wataendelea kuwa maarufu hata wakiwa nje ya chadema.Hapo cdm wengi wamepita na walijimwambafy kwamba ni maarufu kulko taasisi wako wapi nowdays?
 
Mbowe badala ya kuwaripoti polisi wahalifu waliogushi signature ya katibu mkuu yeye anakula nao bata Nairobi na kutaka kumpatia mhalifu mmoja kazi inayolipa zaidi huko nje ya nchi.

Mbowe na hawa madada kwenye hii ishu wanajuana, asituzingue
 
Wanaosema hao akina mdee wangesamehewa hao hao ingetokea hivyo wangeanza kuinanga cdm kwamba wameshindwa kuwafukuza simply mchakato uliowaingiza bungeni ulikuwa na mkono wa Mbowe so acheni uamuzi uliofanywa na baraza ni wa kupongezwa sana na ulikuwa wa kidemokrasia sana na lazima watu wenye mapenzi mema na chadema lazima wauheshimu.Hao akina Mdee wamechagua fungu walilolipenda waache tuwaone kama wataendelea kuwa maarufu hata wakiwa nje ya chadema.Hapo cdm wengi wamepita na walijimwambafy kwamba ni maarufu kulko taasisi wako wapi nowdays?
Wakati mtu wenu anabadili gia angani ilikuwa Demokrasia eti ?
 
Why Mdee? Hata Mimi sijui vya ndani. Ila huyo Halima Mdee ndo flagship ya hao 19. Je, ukimuondoa yeye, hao 18 wangeweza kusimama na kufanya kilichofanyika?
So, mwenyekiti alitummia akili za kawaida kabisa.... ukitaka kuondoa mchwa kwa kichuguu, piga malkia
Mdee yeye aliahidiwa na Mbowe kazi ya mamilioni nje ya nchi, Je Nusrat Hanje au mke wa Bananga aliahidiwa nini?. Mwenyekiti na Halima kuna kitu wanakijua kwenye hii ishu, time will tell
 
waumini wa siasa za jiwe wana wakati mgumu sana. They are fighting to be relevant. mama anataka aachane na siasa za chuki na uonevu tujenge nchi. Ila chawa ndo bado wanaishi kwenye ulimwengu wa jiwe.
Well said Mr.@Masanja
 
Kuna mambo ya siri ya Chadema ambayo Halima Mdee anayafahamu akiyatoa Mwenyekiti Mbowe anaweza kuyumba! Ndio maana kulikuwa na hizo jitihada za kumtafutia kazi huko nje ya nchi!

..Halima ni mjenga hoja mzuri na anayejiamini.

..kama ameshindwa kujitetea kuhusu uhalali wa yeye kwenda bungeni basi kuna tatizo kubwa upande wake.

..Nadhani Halima anaelewa kuwa amekiuka sheria kwenda bungeni ndio maana amepatwa na kigugumizi.

..Halima Mdee sio mtu wa kuenenda namna hii kama anaamini jambo analolisimamia ni la HAKI na HALALI.
 
Back
Top Bottom