Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Baada ya Jay Z kumsaliti Beyonce mashabiki wameandaa kampeni ya kumuombea msamaha.
Ni baada ya albamu ya Beyonce ‘ Lemonade’ kuweka wazi kuwa Jay Z aliwahi kumsaliti na mwanamke aliyemtaja kwa mstari ‘He better call Becky with the good hair’ kwenye wimbo Sorry . Lakini mwanamke huyo aliyehisiwa kuwa ni Rachel Roy alikana kuwahi kutoka na Jay Z.
Mashabiki wa Jay Z wamepanga kufanya kampeni ya kumuombea msamaha Jay Z ili Queen Bey amsamehe bosi huyo wa Rock Nation.
Lakini mtu wa karibu wa familia hiyo aliliambia jarida la US Weekly kuwa rapper huyo, 46, anarekodi nyimbo zitakazoeleza upande wake wa kilichotokea kwenye ndoa yake na Beyonce.
Source: Bongo 5