JAY Z: Malumbano ya familia/ Kumpiga kaka yake RISASI / Usaliti kwa Beyonce/ Msamaha na Funzo kwa mabaharia wote

anonymousafrica

JF-Expert Member
Aug 24, 2016
611
639
maxresdefault.jpg

Nampenda Jay kwasababu anaimba na kuandika maisha yake halisi.

Ukisikiliza nyimbo yake ya You Must Love Me na Kill jayz, amewahi kutaja kisa cha kumpiga risasi kaka yake, akiwa na umri wa miaka 12. Walipitia maisha magumu na familia yake na ni msimu ambao hata baba yake aliitelekeza familia.

Kaka wa Jay Z, Erick alikua mraibu (addict) wa dawa za kulevya. Jay alimwona kaka yake kama anaongeza mzigo kwenye familia, kwasababu maisha yalikua magumu na bado alikua anaiba vitu ndani, siku aliyompiga risasi alikua ameiba pete ya Jay. Bahati nzuri kaka alipona na kumsamehe mdogo wake. Jay alikiri kupagawa na kuhisi angeishia jela, na alimpiga risasi kaka yake ili WANAFAMILIA wamwone kuwa anaweza kuijali familia yake. Aliwahi kuulizwa kama amewahi kuua maishani mwake, alikataa na kusema HATA KAMA INGEKUA KWELI, ASINGESEMA
0ec1a6730afc67d0d80c065bd41348b5.jpg

Alipoulizwa , bunduki ya kumpiga kaka yake aliitoa wapi? alijibu " Niliiba nyumba ya jirani"

Tuachane na hili

Tuje kwenye album ya 4.4.4, hii album Jay ni kama alimtungia Beyonce hahahahaaa (natania, ila ameimba mengi kuhusu familia/ndoa yake). Hivi unajua kwanini Jay Z anaitwa elevator punching bag? Majanga yalianza mwaka 2014 ambapo Bwana Jay Z alipigwa na shemeji yake Solange (Mdogo wa Beyonce). Video clip ilivuja kutoka mtandao wa tmz, ikionyesha jinsi jayz anavyoshambuliwa na shemeji yake kwenye lift hotelini. Beyonce alikua pembeni na hakujitikisa hata kidogo. Haikujulikana sababu ni nin.
Jay+Z+Concert+Hammerstein+Ballroom+P8vFrE29nNVx.jpg

Mwaka 2016, Beyonce alitoa album ya Lemonade na katika kibao chake cha sorry, alimpiga vijembe mume wake kwa kusema, “ananihitaji anaponimis” “ila mara zote hufurahi akiwa na Becky Yule mdada mwenye Nywele nzuri”. Kila mtu aliuliza huyo Becky ndio nani? Mambo yalionekana sio mazuri kwenye ndoa ya Jay na Beyonce (ambao walifunga ndoa ya siri mwaka 2008)
19-beyonce-lemonade-screenshot-2016-billboard-650-compressed.jpg

Ghafla baada ya nyimbo ya sorry ya Beyonce kukick na kusambaa kwa yale maneno ya Becky. Mwanamitindo Rachel Roy ambaye aliwahi kuwa msimamizi wa biashara za nguo za jay z (ROCKAWEAR) Toka miaka ya 1996, alipost instagram picture akiwa anajibu maneno ya Beyonce kuhusu Becky mwenye nywele nzuri, na kiukweli Rachel Roy ni mwanadada mwenye nywele nzuri na huzitunza nywele zake, hivyo baada ya ile post, watu walitia sahihi kuwa Becky with good hair ni Rachel Roy.
Jayonce-Rachel-Roy-Sorry-Becky.jpg

Baadae ilionekana ndio sababu ya Solange (Mdogo wa Beyonce) mwaka 2014, kumvamia Jay Z kwenye lift huku dada yake akiwa anatazama bila kusaidia chochote. Na kabla ya hapa inasemekana walianza kugombana na Roy (BECKY).

Mwaka 2017 ambapo Jay Z alitoa album ya 4:44, alikiri kumcheat Beyonce na kusema “nilimlaumu Solange kwa kusema alifanya utoto, ila kwakweli nilimkosea”. Na Kukiri ule ndio mtiti pekee uliowahi kutokea baina yake na mke wake, waliamua kukaa chini na kuyamaliza. (aligusia machache kwenye nyimbo ya KILL JAY Z)
1200px-4-44_album_cover.png

Album ya 4:44 ilikua ni sehemu ya majuto na kukiri makosa yake huku bila kusita amekua ameomba msamaha live na kwa siri mara nyingine.




Family Feud na video yake inaongea bila vificho na anamtaja Becky amwache na familia yake/asije kumuharibia "Yeah, I'll f*ck up a good thing if you let me/Let me alone, Becky. A man that don't take care of his family can't be rich."

wp1835622.jpg


Kill Jayz, amezungumzia kisa chake na Solange kwenye Lift na kuwataka wanaume wote wasiende nje ya ndoa (You egged Solange on

Knowin' all along, all you had to say you was wrong

You almost went Eric Benét

Let the baddest girl in the world get away

I don't even know what else to say

Nigga, never go Eric Benét)

Never go Eric Benet anawataka watu wasiwe waraubu kwa nje ya ndoa kama yaliyowahi kumkuta Eric Benet)
dish-063017-jz-eric-benet.jpg
 

Attachments

  • Jayonce-Rachel-Roy-Sorry-Becky.jpg
    Jayonce-Rachel-Roy-Sorry-Becky.jpg
    103.1 KB · Views: 10
Dah! Umenikumbusha mbali last time nilipokutana jay z nilimchana kuhusu kumcheat beyonce japo alijitetea kua ilikua ni inshu ya business nyie wabongo mnaita kiki
hhahahahahhaa ile haikua kick.. ndomana alikua/walikua hawataki kuiongelea.... yule mwanamke katembea na Jay z kabla hajamwoa Beyonce 2008
 
Kumbe hadi Beyonce ana salitiwa, mmmmh basi kucheat n nature ya mwanaume.


Mimi binafsi sio honest kivile kwa Mama Gaude wangu, sema ninachofanya siendekezi Sana mpaka akashtukia. Wazee inabidi tutumie mahesabu ya hali ya juu, yaani unapiga unaondoka usitake kusikilizia utamu, ni noma. Halafu kitu kingine hata machale yanamcheza never confess, kikao cha mabaharia kitakutenga.
 
Mimi binafsi sio honest kivile kwa Mama Gaude wangu, sema ninachofanya siendekezi Sana mpaka akashtukia. Wazee inabidi tutumie mahesabu ya hali ya juu, yaani unapiga unaondoka usitake kusikilizia utamu, ni noma. Halafu kitu kingine hata machale yanamcheza never confess kikao cha mabaharia kitakutenga.

It wasnt me- Shaggy(2002)

Hata ukamatwe juu ya kiuno usije thubutu kukiri😁😁
 
Nampenda sana rihanna,lakini beyonce ananichanganya sana hasa yale macho yake..yaani ana macho flani hivi akikuangalia yaani yapo kama makengeza yaani dah beyonce ana macho flani hivi amaizing
 
Mimi binafsi sio honest kivile kwa Mama Gaude wangu, sema ninachofanya siendekezi Sana mpaka akashtukia. Wazee inabidi tutumie mahesabu ya hali ya juu, yaani unapiga unaondoka usitake kusikilizia utamu, ni noma. Halafu kitu kingine hata machale yanamcheza never confess kikao cha mabaharia kitakutenga.
Duuuuuh aseeeeh hatareeeh sana.
 
Back
Top Bottom