lil wayne
JF-Expert Member
- Apr 15, 2016
- 992
- 904
Beyonce na Jay Z waliamua kufanya uamuzi wa pamoja wa kuzusha tetesi za kuachana kwa lengo la kutengeneza pesa.
Uamuzi huo ulihusisha kuuza kopi nyingi za Album mpya ya Beyonce #Lemonide yenye nyimbo ambazo zinaeleza jinsi gani Jay Z amekuwa si muaminifu kwenye Ndoa yao.
Inasemekana kuwa wawili hao hawana mkwaruzano wowote ule ila lengo lilikuwa ni kuuza kopi nyingi za Album hiyo mpya.
Pia inasemekana kuwa Jay Z alihusika/alihusishwa kwenye kila Lyrics za kila nyimbo kwenye hiyo Album, na yeye pia ndiye aliyekuwa akitoa idhini ya kila nyimbo kujumuishwa kwenye Album.
Hivyo basi hata kabla ya Album kuwa released wote walikuwa wanajua lengo la album hiyo.
Mauzo ya Kopi ya Album hiyo inayoitwa Lemonide yamefikia kiasi cha £150 Millioni ambazo ni sawa na pesa za Madafu ya Bongo Kiasi cha Bilioni 357.