Kufilisika kwa mabenki Tanzania: Ni kukua au kuanguka kwa uchumi?

hata hizo CRDB ,NMB zilianza kwa kuwa benki za vichochoroni
Enzi hizo ushindani ulikuwa mdogo benki hazikuwepo na uhitaji wa benki ulikuwa mkubwa

Tofauti na sasa benki lukuki ,ushindani mkubwa na benki zenye brand kubwa ndio zinazokimbiliwa na wateja wengi
 
Enzi hizo ushindani ulikuwa mdogo benki hazikuwepo na uhitaji wa benki ulikuwa mkubwa

Tofauti na sasa benki lukuki ,ushindani mkubwa na benki zenye brand kubwa ndio zinazokimbiliwa na wateja wengi
watu hawaangalii brand, wanaangalia huduma inayotolewa...kuna benki ndogo zinafanya vizuri kupita hizo kubwa benki kama CRDB unadhani mwananchi wa halli ya chini anaweza kumudu masharti ya mikopo?...kuchukua fomu tu ya mkopo laki mbili
 
Hii ni moja wapo ya sababu ya wabunge , madiwani , katambi , tumbili nawengine wapinzani kuachana na nafasi za uwakilishi ,uongozi na uanachama ili kumuunga mkono mtukufu rais
Kati ya wote hao hakuna hata mmoja ambae anaweza kuitwa mpinzani, wapinzani bado wapo 'mtaa wa kiumeni' wamekomaa na wanachokiamini.
 
Ni ujuha kuweka pesa zako au kuweka amana yako kwenye vibenki vya uchochoroni,binafsi sioni kama ni kuteteleka kwa uchumi labda hizo benki walishindwa kwenye soko na sababu za kufilisika zipo nyingi

Ila yote kwa yote kweli uache NBC ,NMB japo siwakubali ,crdb na diamond ,kcb nk uende vibenki vya uchochoroni,?

Haki yao
Ondoa tusi la kuita benki za uchochoroni zisingetambuliwa na BOT tema mate chini ukiona baba ako anaongeza kununua viwanja ili khali ana nyumba tunasema baba ana maendeleo ila ukiona anaanza kuviuza apate hela ya kula ujue amefilisika na nitakushangaa sana ukisema alinunua viwanja vya nn?
 
Kufilisika kwa mabenki Tanzania ni kukua kwa uchumi au kuanguka kwa uchumi?, mjadala huu unaweza kutazamwa kwa namna yoyote kutokea upande wowote, lakini unaweza kuvurugika au kuimarika kama siasa na mihemko inaweza kutumika kujadili hili..

Mimi sio mtaalamu wa mambo ya uchumi, mimi tafsiri yangu ndogo ya kijinga hasa kwa mie mjinga mkuu mwerevu mkulima wa bamia Mbutu Kigamboni, huwa ni idadi ya milo yangu na waleti yangu inasomaje. Haijalishi utanipa siasa gani za uchumi, kama sijashiba milo yangu mitatu kwa siku na kuhakikisha kwa macho yangu ya nyama kwamba pochi yangu haina pesa ya ugoro, basi mie nitasimamia kwamba uchumi umeyumba.

Wiki ya mwisho, masaa ya mwisho na dakika za mwisho za Gavana Beno Ndulu zineshuhudiwa bank tano zinazotambuliwa na Bank kuu Tanzania zinatangazwa rasmi kufilisika na kwamba wateja wake watakwenda kulipwa amana za benki hizo pale Bot.

Baada ya miaka ya 90 Bank ya Meridian kufa baadae ikafa Bank ya Greenland, BOT walituhakikishia kwamba kuanzia wakati ule bank binafsi zitakuwa zinaweka Amana BOT na kila wakati watakuwa wanazikagua, Wateja wasiwe na wasiwasi na Amana zao, hii inamaana kama katika binki flani unapesa kiasi cha bilioni moja, benki hiyo ikifilisika, bilioni moja yako itarudishwa kwako kupitia Bot.

Leo hii Bot wasema kwamba Wateja wa Benki zilizofilisika watalipwa fedha zao na Bodi ya Bima ya Amana huku kiwango cha mwisho cha malipo kikitajwa kuwa ni shilingi Milioni 1.5 bila kujali mteja alikuwa na akiba ya shilingi ngapi? Huku wale wenye akiba ya chini ya shilingi Milioni 1.5 watalipwa zote.

Hii inamaana kwamba kama ulikuwa na milioni miatano katika akaunti yako basi jiandae kulipwa milioni 1.5. Na kama kuna mteja mwingine kwenye akaunti yake alikuwa na milioni moja tu, huyu atalipwa yote bila kuugulia maumivu

Ukweli mchungu ni kwamba Sera za nchi hubuniwa na huenezwa na chama, kisha chama hicho kikishinda uchaguzi kinaunda serikali ambayo inaanza maramoja kusimamia sera za chama hicho katika kutawala.

Kwa Tanzania sera za ccm ndizo zilishinda na ndi yenye sera zote, hivyo mambo yakiharibika au yakiwa mazuri sifa au lawama ni za ccm bila kukukwepesha sifa hizi,

Muhimu cha kujua benki hizi zimenguka kutokana sababu za mdodoro wa kiuchumi iwe Tanzania au dunia vyovyote watakavyotaka kujitetea watetezi wa sera, chama na serikali.
Mdororo huu unasababishwa na sera mbovu za uchumi. Ukosefu wa ajira na kupungua kwa uwekezaji.Hii imesababisha kuweka pesa benki (deposit) kupungu, mikopo kupungua na uwezo wa kulipa mikopo kutoweka. Haya ni ndani ya miaka miwili tu.

Nini kifanyike? Wanauchumi karibuni.....

NB: Wanasiasa uchwara mtupishe na omo zenu midomoni, tunajadili kitaaluma mambo haya.....

Na Yericko Nyerere
View attachment 668959
Mtaalam wa majungu, safari hii umekuja na kitu kinachofikirisha.
Hili ni bomu la mkono Profesa Ndulu amelitupa kwa wale wanaodai uchumi unakua na Takwimu zilizo wekwa sawa kutetea figisu za Dr Mpango.
 
Ukishakua na Baba mwenye mawazo ya kimaskini tegemea familia iwe maskini.tuna mtu anawaza matajiri waishi kama maskini unategemea nini?anataka waliokuwa wanaishi kama malaika waishi kama mashetani unategemea nini? Labda niwaulize hivi wale waliokuwa wanaishi kama malaika je wanaishi kama mashetani au maskini ndo wanaishi kama mashetani?ile usemi WA mwenye nacho huongezewa haujabadilika...so wee ambae huna utaendelea kukosa tuu...kwa kifupi kama upo kazini tunza kazi ulionayo maana biashara hazifanyiki waliopo sokoni wanafunga wewe unaebuni kuingia tumia akili kubwa Sana...wenzio wanarudi kujipanga..na tatizo sio aina ya biashara tatizo nini wanunuaji hawapo... Kila mahali vinekaza labda biko Tu ndo bado Wako vizuri
 
Sidhani ni uamuzi sahihi kufunga Benki zote hizo kwa mpigo ndio sheria zinaruhusu kufanya hivyo lakini, hizo hizo sheria ambazo tumecopy na kupaste kwa wazungu, hao wazungu wakati wa Banks crisis ya 2008 na mabenki mengi kufilisika Ulaya na US hawakuzifuata bali walikuja na stimulus package kuzisupport Banks.

Banks, Stocks Exchange Markets strengths zina umuhimu mkubwa sana katika modern economy pamoja na umuhimu wa prudential controls, far reaching consequences zinatakiwa ziangaliwe kwa kina kabla ya kufanya maamuzi.

kufunga Banks zote hizo kunavunja confidence ya wateja katika mfumo wa banks na kucreate unnecessary financial system panic sasa sijui tunataka watu waweke hela majumbani mwao au ktk informal systems.

Haya maamuzi hauhitaji kuwa economist kujua madhara yake.

Hizo Banks walau zingalikuwa ktk usimamizi wa GVT mpaka zistabilize na kutafutiwa solution nyingine sio kuzifuta kabisa.

Ingalikuwa Banks moja au mbili hilo sawa ili kuweka discipline ktk systems but not 5 Banks at once
 
Ni ujuha kuweka pesa zako au kuweka amana yako kwenye vibenki vya uchochoroni,binafsi sioni kama ni kuteteleka kwa uchumi labda hizo benki walishindwa kwenye soko na sababu za kufilisika zipo nyingi

Ila yote kwa yote kweli uache NBC ,NMB japo siwakubali ,crdb na diamond ,kcb nk uende vibenki vya uchochoroni,?

Haki yao

Wewe ni una mapungufu tu.Kila mtu anafuata benki kulingana na mahitaji au huduma tofauti na pengine. Kwa taarifa yako hizi benki ndogo ndogo ndiyo rafiki kwa wajasirimali ambao ndiyo wengi TZ ..unategemea muuza mboga mwenye mtaji wa laki 1 aweke fedha KCB? Sasa wewe unaujua mtaji wa CRDB? unajua kwa nini Kimei katimka? unajua kinachoendelea NBC? subiri kidogo utaona kivumbi.
 
Mimi siamini kuwa benki hizi zimekufa kwa sababu ya mdororo wa uchumi; nachoamini huenda Benki kuu walitoa leseni bila ya hizo benki kufikia vigezo vya kimtaji
Toka wamesajiliwa hizo benki sheria iliwataka wawe na amana isiyopungua 2 billion, kwa mujibu wa bank kuu...bank zilizotangazwa kufutiwa leseni ziliandikiwa barua mwaka 2016 kujirekebisha na kutimiza masharti ya leseni.....lakini kufikia june 2017 walikuwa bado hawajatimiza hayo masharti kabisa na wakaomba kupewa muda tena na wakapewa tena hadi mwezi wa 12....lakini hadi jana walikuwa hawajatimiza kabisa hivyo wakafutiwa leseni.
Inabidi muwe makini mnapochukua habari jf maana kwa hivi karibuni kuna wapotoshaji wengi sana...
 
Kumbe benki ikifilisika hata kama umeweka akiba mil 100 unaambulia mil 1 na lak5. Sheria za Tz ni za maajabu. Tunahitaji kutafuta sehemu salama ya kuhifadhi amana yako.
Sheria ya amana ina zitaka kila bank wawe wanaweka kiasi fulani kwenye bodi ya bima ya amana ambacho kiasi hicho hutumika kuwafidia wateja kama bank inapo pata tatizo kama zilizo zikutaka bank hizi.Sheria inaelekeza wazi kuwa fidia ya amana kutoka bodi ya amana haitozidi million moja na nusu...
Hivyo basi kama kwenye bank ulikuwa na million 10 basi bima hii itakulipa million 1 na nusu na kiasi kilicho baki utasubiri kulipwa baada ya bank kukusanya mali zake na madeni kutoka kwa wateja na kuuza mali zake ili kuwalipa ninyi mnao dai,....
Hivyo hakuna hela yako itapotea.....
 
Sheria ya amana ina zitaka kila bank wawe wanaweka kiasi fulani kwenye bodi ya bima ya amana ambacho kiasi hicho hutumika kuwafidia wateja kama bank inapo pata tatizo kama zilizo zikutaka bank hizi.Sheria inaelekeza wazi kuwa fidia ya amana kutoka bodi ya amana haitozidi million moja na nusu...
Hivyo basi kama kwenye bank ulikuwa na million 10 basi bima hii itakulipa million 1 na nusu na kiasi kilicho baki utasubiri kulipwa baada ya bank kukusanya mali zake na madeni kutoka kwa wateja na kuuza mali zake ili kuwalipa ninyi mnao dai,....
Hivyo hakuna hela yako itapotea.....
Sawa Rutta, what if mali zao ziko over priced kiasi kwamba wakati wa kuuza hawatapa kiasi kilichoonyeshwa kwenye hesabu zao? Deposit inawekwa benki kuu haina uhusiano na kulipa amana za wateja kama benki ikifilisika?
 
Wao wanafikiri kuwekeza kwenye miundombinu na kununua treni na ndege ndio uchumi wa nchi utaimarika.

Narudia kwa mara nyingine, bila uchumi wa mifukoni mwa watu kuwa mzuri kwa maana ya kuwa na biashara zinazofanya vizuri na watu kuwa na ajira, miundombinu hii ni kazi bure.

Watu hawana fedha na hawana biashara/ajira na hivyo hawakopesheki,miundombinu hii na hizi ndege na treni ndio zitawapa mitaji?

Kama watu hawakopesheki,benki zitapataje faida kama hazifanyi biashara ya kukopesha?

Kama biashara zinafungwa na zingine zinakufa kutokana na bomoabomoa,hela za watu kupeleka benki zitatoka wapi?

Benki gani leo hii itakuwa na uhakika kuwa mikopo ya malori na hata mabasi itaweza kulipika vizuri wakati treni ya kisasa itayofika mpaka bandarini na mikoani inabisha hodi?

Nini kinafanyika kuhakikisha sekta ya usafirishaji kwa maana ya mabasi na malori haitathiriwa na ujio wa treni za kisasa na kutishia utoaji wa mikopo kwa sekta hii ya usafirishaji?

Benki hizi bila kutoa mikopo, zitatengeneza vipi faida?

Watu wanaposikia mabenki yanafilisiwa huku kiwango cha juu cha mtu kulipwa ni milioni 1.5 bila kujali amana uliyokuwa nayo,watu watakuwa na moyo wa kuweka fedha zao katika benki zenye mitaji midogo?

Watu wakiamua kuhamisha fedha kutoka benki ndogo ndogo na kupeleka fedha zao katika mabenki makubwa kwa hofu ya benki hizi nazo kufilisika,tutakuwa tunajenga au tunabomoa uchumi wa nchi na wa taasisi hizi za fedha?

Nikiwaza ya mbele naona giza tupu mwenzenu!!
Aiseeee !!!!
 
Fiduciary line kwa Banks ni very narrow decision makers lazima wafanye calculated weighing between reinforcement of Banking financial disciplines na eroding cofindence in Banking industry.

Banks ni very delicate maamuzi yisiyo sahihi yanaweza kucreate Bank runnings massive withdrawals of funds from Banks na collapse of Banks.

Tuna overseeing nzuri ya BOT ambao wanaweza kureinforce discipline, ni rahisi zaidi kureinforce compliance to Banks by BOT.

Na vile vile rahisi sana sana kuathiri Banks kwa tactical errors kama hizi, with growth of digital media platforms information goes viral in short time, wengi wataangalia namba ya Banks siyo ukubwa wa Banks.

Kuna hela nyingi sana iko nje ya mfumo wa Banks lazima tuzijengee Banks zetu mazingira ya kuaminika ili wananchi wazidi kudepot pesa zao
 
MIMI KWA UELEWA WANGU, KUFILISIKA NA KUFUNGWA KWA MABENKI NI DALILI MOJA KUBWA YA KUANGUKA KWA UCHUMI.

HATA UKISOMA HISTORIA YA GREAT DEPRESSION YA MWAKA 1929-32 DALILI NI HIZOHIZO
 
uchumi umekua ,bank zinafilisika

uchumi umekua,wananchi wanalalamika

uchumi umekua, mishahara ya watumishi wa umma inacheleweshwa na malimbikizo juu

uchumi umekua ,wawekezaji wanazidi kupungua

uchumi umekua, ajira hakuna kila siku matamko

naamini kabisa zimeanza hizi ndogo zitafuatia kubwa kama juhudi na jitihada hazitafnyika

safu yako ya uongozi imejaa maprofesa madokta lakini work done zero

Mungu ibariki Tanzania
Na wao wameona bora wagonge meza na cheers kwa kila kitu maana jamaa keshasema huwa ukimshauri ndiyo hakusikilizi kabisa sasa wanaokoa muda kwa kukunja mamilion ya mishahara na posho kwa mwezi maana hata hali iwe ngumu haitafika kwao na ikifika kwao jua TANZANIA itakuwa imeitwa mufilisi
 
MIMI KWA UELEWA WANGU, KUFILISIKA NA KUFUNGWA KWA MABENKI NI DALILI MOJA KUBWA YA KUANGUKA KWA UCHUMI.

HATA UKISOMA HISTORIA YA GREAT DEPRESSION YA MWAKA 1929-32 DALILI NI HIZOHIZO

Wenyewe wanaita ukuaji wa uchumi kwa maneno ya Benno Ndulu mwenyewe!

I am so worried about loss of public confidence in the current financial institutions! Kuanguka kwa benki tano kwa mkupuo mmoja is not a joke! Hata kama hizo benki ni ndogo kiasi gani!

Huyu MKEMIA wetu kila kitu anajua yeye! Acha tu tuanguke ili tujifunze kwa vitendo!
 
Ni kuanguka vibaya kwa uchumi wa Tanzania.

Ni Ishara mbaya kwamba tuna hahaha kiuchumi.

Kwa Mujibu wa Gavana Nduru. Sababu moja wapo ya kuanguka kwa mabank hayo ni wigo mdogo wa Biashara. maana yake biashara tanzania imepolomoka, hakuna mikopo na hakuna watu wa kuwauzia bidhaa. hakuna msisimko wa Biashara kabisa watu wanabaki kuuza mahindi na nyanya.
 
Ni ujuha kuweka pesa zako au kuweka amana yako kwenye vibenki vya uchochoroni,binafsi sioni kama ni kuteteleka kwa uchumi labda hizo benki walishindwa kwenye soko na sababu za kufilisika zipo nyingi

Ila yote kwa yote kweli uache NBC ,NMB japo siwakubali ,crdb na diamond ,kcb nk uende vibenki vya uchochoroni,?

Haki yao
Bab nasikia kcb wanalipa kwa Mpesa ....
 
Nadhani kulikuwa na haja ya kuzipa muda wa kutangaza mufilis kwa banki hizo au kuthibitisha uwezo wao wa kujiendesha huku wateja wake wakipata mwanya wa kuangalia usalama wa pesa zao na kuchukua hatua.


Anyway,siyo mtaalamu wa masuala ya uchumi.....lakini dalili si njema.
 
Back
Top Bottom