Kufilisika kwa mabenki Tanzania: Ni kukua au kuanguka kwa uchumi?

Kufilisika kwa mabenki Tanzania ni kukua kwa uchumi au kuanguka kwa uchumi?, mjadala huu unaweza kutazamwa kwa namna yoyote kutokea upande wowote, lakini unaweza kuvurugika au kuimarika kama siasa na mihemko inaweza kutumika kujadili hili..

Mimi sio mtaalamu wa mambo ya uchumi, mimi tafsiri yangu ndogo ya kijinga hasa kwa mie mjinga mkuu mwerevu mkulima wa bamia Mbutu Kigamboni, huwa ni idadi ya milo yangu na waleti yangu inasomaje. Haijalishi utanipa siasa gani za uchumi, kama sijashiba milo yangu mitatu kwa siku na kuhakikisha kwa macho yangu ya nyama kwamba pochi yangu haina pesa ya ugoro, basi mie nitasimamia kwamba uchumi umeyumba.

Wiki ya mwisho, masaa ya mwisho na dakika za mwisho za Gavana Beno Ndulu zineshuhudiwa bank tano zinazotambuliwa na Bank kuu Tanzania zinatangazwa rasmi kufilisika na kwamba wateja wake watakwenda kulipwa amana za benki hizo pale Bot.

Baada ya miaka ya 90 Bank ya Meridian kufa baadae ikafa Bank ya Greenland, BOT walituhakikishia kwamba kuanzia wakati ule bank binafsi zitakuwa zinaweka Amana BOT na kila wakati watakuwa wanazikagua, Wateja wasiwe na wasiwasi na Amana zao, hii inamaana kama katika binki flani unapesa kiasi cha bilioni moja, benki hiyo ikifilisika, bilioni moja yako itarudishwa kwako kupitia Bot.

Leo hii Bot wasema kwamba Wateja wa Benki zilizofilisika watalipwa fedha zao na Bodi ya Bima ya Amana huku kiwango cha mwisho cha malipo kikitajwa kuwa ni shilingi Milioni 1.5 bila kujali mteja alikuwa na akiba ya shilingi ngapi? Huku wale wenye akiba ya chini ya shilingi Milioni 1.5 watalipwa zote.

Hii inamaana kwamba kama ulikuwa na milioni miatano katika akaunti yako basi jiandae kulipwa milioni 1.5. Na kama kuna mteja mwingine kwenye akaunti yake alikuwa na milioni moja tu, huyu atalipwa yote bila kuugulia maumivu

Ukweli mchungu ni kwamba Sera za nchi hubuniwa na huenezwa na chama, kisha chama hicho kikishinda uchaguzi kinaunda serikali ambayo inaanza maramoja kusimamia sera za chama hicho katika kutawala.

Kwa Tanzania sera za ccm ndizo zilishinda na ndi yenye sera zote, hivyo mambo yakiharibika au yakiwa mazuri sifa au lawama ni za ccm bila kukukwepesha sifa hizi,

Muhimu cha kujua benki hizi zimenguka kutokana sababu za mdodoro wa kiuchumi iwe Tanzania au dunia vyovyote watakavyotaka kujitetea watetezi wa sera, chama na serikali.
Mdororo huu unasababishwa na sera mbovu za uchumi. Ukosefu wa ajira na kupungua kwa uwekezaji.Hii imesababisha kuweka pesa benki (deposit) kupungu, mikopo kupungua na uwezo wa kulipa mikopo kutoweka. Haya ni ndani ya miaka miwili tu.

Nini kifanyike? Wanauchumi karibuni.....

NB: Wanasiasa uchwara mtupishe na omo zenu midomoni, tunajadili kitaaluma mambo haya.....

Na Yericko Nyerere
View attachment 668959
Nimekuelewa vizuri.
 
hili la bank kufilisika sio jambo dogo ni kubwa sana. serikali imetangaza tangazo baya sana kwa mabank mengine!! tusitegemee wananchi kuweka pesa zao kwenye mabank yasio na majina na wengine hawataweka kabisa. yaan niweke 100 million nije kulipwa 2.5 million si kuuana huku?? asant JPM tunyooshe baba. baadaye tutaelewana kwamba uchumi umekua ikulu ila huku uraian ni 0
Labda tuweke mambo sawa kidogo. Kwanza benki yoyote inayopata leseni ya BOT inatakiwa kulipa 1% ya jumla za amana zake zote kama bima kwa wateja wake. Kutoka kwenye bima hii ndipo mteja wa benki husika atalipwa maximum ya TZS 1.5 million kwa sheria ya sasa ambayo inaweza kubadilika kulingana na kukua kwa uchumi na mambo mengine yatakayopelekea mabadiliko katika sheria hiyo. Pesa hizi hulipwa na mfuko unaoitwa DIB ulioko BOT.
Lakini wanabodi tuzingatie kwanza ukweli kuwa benki ni taasisi ya kibiashara yenye mizania yake. Mizania ya Benki ina pande mbili za Raslimali (assets) na dhima (liabilities). Kwa kawaida pande hizi zinafanya mizania ambayo lazima pande hizi zijisawazishe (balancing). Yaani kwa wakati wowote assets zilingane na liabilities. Sasa twende pamoja.
Benki inapopata matatizo wateja wenye amana zisizozidi 1.5m watalipwa woote kupitia DIB kama bima ya wateja wa benki zote hapa TZ. Sasa kama mteja alikuwa na kiasi kinachozidi TZS 1.5m atalipwa na raslimali za benki husika baada ya kuzithamanisha katika pesa. Tukumbuke kitu kimoja cha msingi kwamba raslimali za benki ni pamoja na mikopo iliyotolewa kwa wateja ambao wameweka dhamana ya mali zao kwa benki iliyopata matatizo. Hivyo wakati wa ufilisi, DIB itawadai wakopaji woote na watalipa wakishindwa DIB itauza dhamana za wateja na kupata pesa. Pesa hizo zitatumika kulipa depositors. Hata kama mchakato huu utachukua muda lakini hakuna haki ya mteja aliyeweka pesa benki ikapotea. Tujikumbushe tu kuwa benki kama za Meridian Biao, FBME, Greenland Bank, First Adili, Trust Bank na hata Bank M hakuna aliyepoteza pesa zake.
Jamii Forum lazima ichambue mambo kwa mtizamo sahihi na chanya. Tusikae hapa kuwalisha matango pori wanajamii ni vibaya tuna create panic isiyokuwepo ndugu zangu.
Tuendelee kuamini mifumo ya kifedha kwamba iko salama mpaka sasa. Tunapolilia uchumi ukue lazima banking system iwe strong. Pesa ulizoweka kwenye pillow kule chumbani hazina madhara chanya kwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi kwa sababu haziingii kwenye real sectors zikatoa mikopo kwa wawekezaji, wajasiriamali na hata wanaohitaji mikopo kwa ajili ya matumizi. Tukumbuke tu kwamba Production inakuwa stimulated by consumption na uwepo wa purchasing power. Na kwa upande wa consumers, purchasing power inaweza kuwa stimulated by personal finances kutoka kwenye taasisi za fedha. Uzalendo kwanza.
 
Back
Top Bottom