Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,639
- 22,490
Mie ndadhani mara nyingine hawa viongozi wa nje wanapotutembelea tunawakuza kupita kiasi wanachostahili. Alikuja Mfalme wa Morocco hapa, tukawa omba omba hadi wa kujengewa viwanja na misikiti. Kaja Mturuki tunamuomba mkopo wa kujenga reli ya standard gauge. Kwanza tujiulize, hivi tunajua gharama ya kujenga reli? Na huyo Mturuki, ana uchumi gani wa maana wa kutupa sisi mkopo wa masharti nafuu ili tujenge reli? Kwamba hiyo hela ni ya serikali au ya benki za uturuki? Serikali ya Uturuki ina fedha za kutoa misaada au hata mikopo ya kiasi hicho?
Ukweli ni kwamba kama kuna taifa lenye uwezo wa kutoa mkopo wa masharti au riba nafuu kwa ajili ya ujenzi wa reli hii basi ni China. Ndio maana nchi kama Ethiopia na Kenya reli na barabara zao zimekamilika haraka kwa sababu waliliona hilo. Tusisahau sasa hivi China anamfukuza Marekani katika kuwa economic power of the world, baada ya kumpiku Japan.
Sasa ni nini kimekorofisha katika suala zima la kujenga reli ya standard gauge kwa kupitia mgongo wa China hadi tuanze kuwa omba omba kwa nchi ndogo kama Uturuki? Tusiahau kwamba mara nyingine katika mambo ya uhusiano wa kimataifa huwezi kuepuka msemo wa beggars can't be choosers. Kama China wanataka kampuni yao ndio ijenge reli wakitupa huo mkopo, tatizo ni nini ikiwa China inajulikana duniani kuongoza kwenye mambo ya ujenzi wa reli? Hivi mnajua kwamba mfumo wa treni za chini za Washington ulijengwa na Wachina? Na reli ya Addis hadi Djibuti inayosifiwa si China? Na TAZARA je?
Tusipoangalia, hili suala la reli standard gauge hapa Tanzania litakuwa ni ndoto tu, wakati jirani zetu wanapeta! Mara nyingine tusijifanye tuna akili kuliko vile tulivyo.
======
Tazama Mjadala kuhusu hoja hii ukisomwa JamiiLeo